Steve Harvey na mkewe wakanusha, tetesi za kuachana

Intelligent businessman

JF-Expert Member
Sep 6, 2022
26,227
53,040
HARVEY: MIMI NA MKE MAMBO SUPA BULL BULL

Mara baada ya kutawala kwa habari zakuachana na mkewe, Marjorie Harvey katika mitandao ya kijamii, mchekeshaji na mshauri wa mambo mbalimbali, Steve Harvey ameibuka na kusema kwamba yeye na mkewe mambo mazuri kama kawaida.

Tetesi hizo ambazo zilianza kusambazwa kwenye mitandao mbalimbali ya kijamii zilidai kwamba Harvey alimfumania mkewe akiwa kwenye mapenzi motomoto na mlinzi wake na hivyo kufanya uamuzi wa kumuacha na mwanamke huyo kudai kiasi cha dola milioni 200 kama tu angepewa talaka.

“Kabla sijaanza naomba niseme nipo poa. Sijajua mnataka nini kwenye ndoa hii ila niwaambie tu kwamba tupo sawa na hakuna lolote lile, hizo taarifa zote kuhusu kuvunjika kwa ndoa hii ni uongo. Bado nang’ara,” alisema Harvey katika video aliyoweka Tiktok.

Kukanusha kwa uvumi huo haukuishia kwa Harvey tu kwani hata mkewe naye alichukua nafasi kwenye Mtandao wa Kijamii wa Instagram na kukanusha uvumi huo.

👉Je wame amua kuli zima swala hili, ndani kwa ndani??
👉Au ilikuwa ni kutafuta Kiki, wazidi kuongelewa??
FB_IMG_16933033513599981.jpg
 
Hivi kwanini...picha hazifunguki..ina maana moderator hawasikii kilio chetu
 
Back
Top Bottom