...Kumradhi 'wataoguswa ndipo', lakini na maswali yangu kadhaa;
...hivi ni kwanini watu wafupi 'wengi' wanakuwa wabishi, wakorofi, wagomvi?
...au ni mgongano tu wa mawazo?
...hivi ni kwanini tuna serikali ya muungano, na serikali ya Zanzibar tu? Kwanini 'wengi' hawataki kuzungumzia muungano wa serikali moja, au angalau wa serikali tatu (ikiwemo ya bara?), bila kuleta porojo za gharama za uendeshaji?
...hivi 9/Dec 'kila mwaka' tunasherehekea uhuru wa nchi gani iwapo hakuna nchi inayoitwa Tanganyika?
...sijatumwa, ni mgongano tu wa mawazo!
...hivi ni kwanini wanawake wabaya 'wengi wao' wanariiiiiinga?
...hivi ni kwanini 'wengi' wasokuwa nacho, A.K.A masikini A.K.A 'mlalahoi' ufahari wake ni kuoa wake wengi na watoto wengiii (watano na kuendelea), wakati tajiri ufahari wake mtoto mmoja au wawili?...mgongano wa mawazoo bila kuangalia itikadi/imani za dini
Uzuri wao uko kwingine. Wengi wao shughuli zao ni pevu haswa!