Stephen Wassira umemwachia nani ofisi? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Stephen Wassira umemwachia nani ofisi?

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by segwanga, Mar 22, 2012.

 1. segwanga

  segwanga JF-Expert Member

  #1
  Mar 22, 2012
  Joined: Mar 16, 2011
  Messages: 2,790
  Likes Received: 37
  Trophy Points: 145
  Naomba wanabodi mnijuze sababu zinazo mfanya mtu kama wassira kuiacha ofsì yake na kwenda kwenye kampeni za chama kwa muda mrefu.Yeye ni waziri akiwa ni sehemu ya serikali,huko aliko mi navyoona hafanyi kazi ya serikali lakini nina uhakika atakuwa na gari la serikali na analipwa per diem kama waziri akiwa nje ya kituo cha kazi.Nashindwa kuelewa kazi zake za uwaziri anazifanya lini au ndo hayo mambo yake ya KUFANYA BUNGE KAMA SLEEPING ROOM?
   
 2. mopaozi

  mopaozi JF-Expert Member

  #2
  Mar 22, 2012
  Joined: Nov 17, 2010
  Messages: 3,290
  Likes Received: 105
  Trophy Points: 160
  Ndo maana tunataka katiba mpya ipige marufuku wabunge kuwa mawaziri tunataka mawaziri wasiwe wabunge kutoka vyama vya sihasa tuwe kama wenzetu walioko mbele jamani itaongeza nafasi za ajira kuliko sasa mtu mmoja ajira mbili na bado za chama tena!!
   
 3. Wambugani

  Wambugani JF-Expert Member

  #3
  Mar 22, 2012
  Joined: Dec 8, 2007
  Messages: 1,755
  Likes Received: 47
  Trophy Points: 145
  Labda amemwachia William Lukuvi kwani wote kazi zao ni SERA na URATIBU.
   
 4. Kimbunga

  Kimbunga Platinum Member

  #4
  Mar 22, 2012
  Joined: Oct 4, 2007
  Messages: 13,012
  Likes Received: 1,817
  Trophy Points: 280
  Mkuu hivi Wasira ana Ofisi? Katibu Mkuu wake ni nani vile?

  Kama ulikuwepo miaka ya 80 utakumbuka mawaziri wasiokuwa na wizara maalumu! Kama hukuwepo basi kulikuwa na Mawaziri wanaitwa Waziri asiyekuwa na wizara maalumu au kwa lugha ya Malkia Minister without Portfolio. Ilikuwa ni kupeana tu kwa kuwa wizara zilikuwa zimejaa; sijui na Wasira alistahili kuwa waziri asiye na wizara maalum.
   
 5. m

  mtengwa JF-Expert Member

  #5
  Mar 22, 2012
  Joined: Aug 20, 2011
  Messages: 1,745
  Likes Received: 225
  Trophy Points: 160
  Yule ni janga la kitaifa
   
 6. TIMING

  TIMING JF-Expert Member

  #6
  Mar 22, 2012
  Joined: Apr 12, 2008
  Messages: 21,837
  Likes Received: 125
  Trophy Points: 160
  na per diem anachukua wizarani
   
 7. Ndahani

  Ndahani JF-Expert Member

  #7
  Mar 22, 2012
  Joined: Jun 3, 2008
  Messages: 14,333
  Likes Received: 1,795
  Trophy Points: 280
  Kwani huyu bwana amepewa kazi gani? Maana yeye kazi yake ni mahusiano sasa kuna Taifa lina waziri wa wahusiano au ni sisi tu for the reasons good to ourselves. Pengine ndo anatimiza wajibu wake akienda kuongeza shamra shamra kwenye kampeni. Tingatinga si unajua hayupo tena kwenye hiyo biashara.
   
 8. Michese

  Michese JF-Expert Member

  #8
  Mar 22, 2012
  Joined: Feb 9, 2008
  Messages: 371
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  wizara kama hii ya wassira ndio zinatutia umaskini,anatumia pesa zetu kufanya kampeni za magamba bila hata aibu
   
 9. MAMA POROJO

  MAMA POROJO JF-Expert Member

  #9
  Mar 22, 2012
  Joined: Nov 22, 2007
  Messages: 4,966
  Likes Received: 27
  Trophy Points: 135

  Kwenye red kunahitaji ushahidi endapo kaonekana anatumia gari la serikali Arumeru na kama analipwa per diem na serikali japo inawezekana lakini habari sahihi zinaweza kutusaidia kutoa hukumu kwa wassira na serikali kwa usahihi zaidi.
   
 10. MAMA POROJO

  MAMA POROJO JF-Expert Member

  #10
  Mar 22, 2012
  Joined: Nov 22, 2007
  Messages: 4,966
  Likes Received: 27
  Trophy Points: 135
  Tuhuma hizi za kukurupuka dhidi ya wassira zina tofauti gani na za Wassira kwamba Dk Slaa alikwiba kanisa katoliki.
   
 11. MAMA POROJO

  MAMA POROJO JF-Expert Member

  #11
  Mar 22, 2012
  Joined: Nov 22, 2007
  Messages: 4,966
  Likes Received: 27
  Trophy Points: 135
  Jembe likikukata unakimbilia hospitali kupata tiba naona Wassira amekuwa mwiba Arumeru

  ....... wafuasi wa chadema wanakimbilia Jf kurusha mawe hovyo hovyo.

  halahala msitupopoe tusiohusika!!!!!!!!!.
   
 12. MAMA POROJO

  MAMA POROJO JF-Expert Member

  #12
  Mar 22, 2012
  Joined: Nov 22, 2007
  Messages: 4,966
  Likes Received: 27
  Trophy Points: 135

  MaKatibu Mkuu pia hufanya kazi kwa utaratibu huo kama waziri hayuko.

  Vivyo hivyo, kutokana na maendeleo ya teknolojia Wassira anaweza kufanya kazi za ofisi akiwa Arumeru hasa ambazo zinahitaji maamuzi yake kama waziri.
   
 13. Memo

  Memo JF-Expert Member

  #13
  Mar 22, 2012
  Joined: Jan 17, 2011
  Messages: 2,147
  Likes Received: 17
  Trophy Points: 135
  Hivi waziri wa MAHUSIANO maana yake nini?

  Kwa mfano tunaweza kumfananisha na MSHENGA kwenye mambo ya mahusiano ya ndoa na mambo kama hayo??
   
 14. Memo

  Memo JF-Expert Member

  #14
  Mar 22, 2012
  Joined: Jan 17, 2011
  Messages: 2,147
  Likes Received: 17
  Trophy Points: 135
  Wewe hapa upo Face book au JF?
  hapa unatupa mawe au unatafuta hawara?
  Naona ****** makuuubwa kwenye avatar!!!
   
 15. B

  Bangoo JF-Expert Member

  #15
  Mar 22, 2012
  Joined: Nov 3, 2011
  Messages: 5,594
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 135
  Raisi wetu ana vituko! Eti waziri wa mahusiano na uratibu!. Hapo hamna waziri ni janga. Tunajua mnapeana uwaziri kiskaji tuache haya mambo jamani ndo maana ufisadi hauishi!.
   
 16. Kimbunga

  Kimbunga Platinum Member

  #16
  Mar 22, 2012
  Joined: Oct 4, 2007
  Messages: 13,012
  Likes Received: 1,817
  Trophy Points: 280
  Mkuu mimi hayo mahusiano hata siyajui. Nilidhani ni mahusiano ya vyama na serikali lakini sasa kama yuko upande mmoja anafanya mahusiano gani?
   
 17. s

  sawabho JF-Expert Member

  #17
  Mar 22, 2012
  Joined: Feb 25, 2011
  Messages: 4,502
  Likes Received: 948
  Trophy Points: 280
  Hivi Ofisi zake ziko jengo gani ? na Katibu Mkuu wake ni yupi ?
   
 18. Komeo

  Komeo JF-Expert Member

  #18
  Mar 22, 2012
  Joined: May 3, 2011
  Messages: 2,396
  Likes Received: 423
  Trophy Points: 180
  Kwani ana kazi yoyote muhimu huyo? Sasa unapoona mtu hayupo "ofisini" kwa mwezi mzima, na mambo yanaenda kama kawaida hakuna kinachoharibika, unafikiri kuna umuhimu wa yeye au ofisi yake tena hapo? Upuuzi tu!
   
 19. segwanga

  segwanga JF-Expert Member

  #19
  Mar 22, 2012
  Joined: Mar 16, 2011
  Messages: 2,790
  Likes Received: 37
  Trophy Points: 145
  haya ndo madhara ya kuingia madarakani,jk alilazimika kuacomodate mazee ya mtandao kama tyson ili mradi liwemo tu kwenye system
   
 20. N

  Ngonini JF-Expert Member

  #20
  Mar 22, 2012
  Joined: Sep 1, 2010
  Messages: 2,024
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 135
  Hivi hapa hamna jinai ya matumizi mabaya ya ofisi ya umma? wanasheria tusaidieni maana huyu jamaa si mara ya kwanza kuaacha ofsi kwa mwezi mzima akiwa kwenye shughuli za chama ili hali akilipwa mshahara kwa kodi zetu. kwa taratibu za ajira hapa kuna kesi ya kujibu mimi ninavyoona. Chadema hebu ulizeni hili kwenye kampeni wananchi wa AruMeru wapime wenyewe kama ni sahihi kwa wasra kuacha kazi tuliye mwajiri kwa mwezi mzima na huku anaendelea kuchukua mshahara na posho.
   
Loading...