Kumbe hujui unalolisema. Wassira kajenga nyumba nzuri ya kuishi yenye hadhi yake hapa Bunda eneo la Chiringe "A" karibu na Shule ya Sekondari Bunda Day. Haitaji kuwa na nyumba zaidi ya hiyo kwa sababu utamaduni wa kujilimbikizia mali haujamkuza. Ni mwepesi kutosheka.
Sisi tunaoishi Bunda tunaona mabadiliko makubwa kiuchumi na kijamii ikilinganishwa na enzi za Jaji Warioba na wenzake wengine walipokuwa wabunge wa Bunda.
Bunda ya sasa imepiga hatua nzuri katika maendeleo ya Elimu, Afya, Maji, Barabara nk. Mfano, katika Afya, Wassira kaiwezesha Bunda kuwa na Hospitali ya Wilaya (Manyamanyama) lakini wakati huohuo bado serikali ina mkono wake katika Bunda DDH. Hapo Bunda tunakula double! Kuna mradi mkubwa wa maji wa Nyabehu utakaomaliza shida ya maji Bunda nk