PreGE2025 Stephen Wasira: Kaeni Kimyaaaa Kama Hamjui Nchi Ilikotoka

PreGE2025 Stephen Wasira: Kaeni Kimyaaaa Kama Hamjui Nchi Ilikotoka

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla)

Lucas Mwashambwa

JF-Expert Member
Joined
Jul 28, 2022
Posts
36,358
Reaction score
23,760
Ndugu zangu Watanzania,

Makamu Mwenyekiti wa CCM Taifa Mheshimiwa sana Stephen Wasira Ameunguruma na kuitetemesha Geita. Ametoa ujumbe Mzito Sana ulio wabubujisha watu machozi ya furaha.

Embu Soma hapa chini 👎KAENI KIMYA KAMA HAMJUI
NCHI ILIKOTOKA - WASIRA

MAKAMU Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Bara, Stephen Wasira amesema tangu kupata uhuru Tanzania imepata maendeleo makubwa na kwamba wanaosema hakuna kilichofanyika ni vema wakakaa kimya, wasiwe na tabia ya kasuku kukariri wasiyoyajua.

Wasira ameyasema hayo leo Juni 17, 2025 alipokuwa akizingumza katika mkutano wa hadhara Katoro, mkoani Geita akiwa katika ziara ya kukagua uhai wa Chama na kuzungumza na wananchi.

Akieleza kuhusu maendeleo yaliyofanyika nchini tangu kupatikana kwa uhuru alisema ni makubwa na wenye umri mkubwa wanajua vizuri nchi ilivyokuwa na wamekuwa wakishuhudia hatua mbalimbali zinazofanywa na serikali inayoundwa na CCM.

“Labda ninyi vijana hamwelewi lakini niwaambie wakoloni wa Kijerumani na wakoloni wa Kiingereza wamekaa Tanganyika miaka 75, Wajerumani wamekaa miaka 35, wamejenga reli kwa viboko bila malipo.

Waingereza wamekaa miaka 40 walitumwa na Umoja wa Mataifa (UN) watuendeleze tujitawalie, lakini miaka 40 ya Waingereza wametuacha na wahandisi wawili katika nchi isiyo na barabara.

“Wametuachia nchi hakuna daktari hata mmoja walikuwepo madaktari kutoka India na Pakistani nao walikuwa Dar es Salaam. Wakati tunapata uhuru akina mama walikuwa hawajifungui ila wanazaa maana hakukua na kliniki, hivyo walikuwa wanazaa kama ng’ombe anavyozaa ndama.

Ng’ombe umeona wapi ana kliniki (ya uzazi)? Hiyo ndio hali waliyotuacha nayo (wakoloni) wametuacha hatuna barabara.

“Leo anakuja mtu hajafikisha umri wa miaka 30 au miaka 40 anawaambia hakuna maendeleo. Wewe uliwahi kutembea kwa miguu, kuna maendeleo, hao wanaosema hakuna maendeleo ambayo yamefanyika akija muulizeni hivi kwako maendeleo ni kitu gani?.
Wasira amesema inawezakana wanaosema hakuna kilichofanyika anazungumza kama kasuku, maana kasuku huwa anakariri tu haelewi hata maana ya maneno anayosema na hao ndio wanasiasa wapya, sisi tumejitawala tulikuwa na msomi mmoja tu mwenye ‘Master’ (shahada ya uzamili) Julius Nyerere ndio alikuwa ameandaliwa na Wakoloni kwa miaka 75.

“Leo wala sio Tanganyika nilikuwa namuuliza Mkurugenzi wa Bukombe asubuhi anasema ana wahandisi 12, nikasema wewe ni tajiri kuliko Tanganyika ya mwaka 1970 maana kulikuwa na wahandisi wawili wewe unao 12. Namuuliza madaktari anasema wengi tu sisi hatukuwa na daktari.

“Hiyo ndio nchi tuliyorithi, leo unaweza kwenda mkoa wowote wa Tanzania kwa lami. Zamani wakati tunakabidhiwa nchi lami ilikuwa inatoka Dar es Salaam mpaka Morogoro kwa sababu kulikuwa na wazungu wanalima mkonge, ilikuwa inatoka Tanga mpaka Korogwe kwa sababu kulikuwa na wazungu wanalima konge.
Screenshot_20250618-113315_1.jpg


== ==

Kazi iendelee, Mama Ametufikia na kuwafikia watanzania kwa utumishi wake uliotukuka wa kugusa Maisha ya watanzania wanyonge wasio na Sauti.

Lucas Hebel Mwashambwa, Mama ANATOSHA kuendelea kuliongoza Taifa letu kwa muhula wa pili.
 
Tanzania haipaswi kupimwa kwa historia pekee bali kwa current impact. Yes, tulitoka mbali, lakini “how far have we moved now?” Vijana hawalalamiki kwa ujinga, bali kwa kuishi kwenye mfumo unaoshindwa kuwapa ajira, afya bora, wala elimu yenye tija. Don’t romanticize the past to mask present failures.
 
Kumbe wakoloni walitumwa na UN na hamkutufundisha shuleni badala yake mlituambia vingine
 
Tanzania haipaswi kupimwa kwa historia pekee bali kwa current impact. Yes, tulitoka mbali, lakini “how far have we moved now?” Vijana hawalalamiki kwa ujinga, bali kwa kuishi kwenye mfumo unaoshindwa kuwapa ajira, afya bora, wala elimu yenye tija. Don’t romanticize the past to mask present failures.
Ajira zinatolewa na serikali kila mwaka. Sasa sijui wewe unataka ajira zipi hizo.
 
Ajira zinatolewa na serikali kila mwaka. Sasa sijui wewe unataka ajira zipi hizo.
It’s a classic political move to win hearts, not a long, term plan.

Huelewi nini au kazi yako wewe ni kujizima data hata kwenye mambo yanayoonekana hata na kipofu????
 
Back
Top Bottom