Stephen Curry afikisha Ppints 4000 NBA

Stephen Curry afikisha Ppints 4000 NBA

Dalton elijah

JF-Expert Member
Joined
Jul 19, 2022
Posts
783
Reaction score
1,831
Nyota wa Golden State Warriors Stephen Curry amekuwa mchezaji wa kwanza kufikisha pointi 4,000 za pointi 3 katika katika historia ya NBA na kuongeza wasifu wake wa mchezaji bora wa Kikapu kuwahi kutokea katika NBA.

1741935969482.png
Wakati Stephen Curry alianza uchezaji wake, hakuna mchezaji katika historia ya NBA aliyewahi kutengeneza alama 3,000 za pointi 3 katika maisha yake ya soka, kwa sasa jambo limekuwa kawaida kwake ambaye amefikisha pointi 4,000 katika mchezo vs Sacramento Kings.

Hii hapa Orodha ya wachezaji vinara wa NBA ambao wamefunga pointi 3 nyingi.

1. Stephen Curry Pts 4,000
2. James Harden Pts 3,123
3. Ray Allen Pts 2,974
4. Damian Lillard Pts 2,794
5. Klay Thompson Pts 2,667
6. Reggie Miller Pts 2,560
7. Lebron James Pts 2,542
 
Hasheem Thabeet wetu alikuwa draft namba 2 wakati Stephen Curryy akiwa draft namba 9 kwenye mwaka wao. Mabadiliko makubwa sana yametokea.
Kipaji bila ya nidhamu ya maisha huwa hakidumu.
 
Nyota wa Golden State Warriors Stephen Curry amekuwa mchezaji wa kwanza kufikisha pointi 4,000 za pointi 3 katika katika historia ya NBA na kuongeza wasifu wake wa mchezaji bora wa Kikapu kuwahi kutokea katika NBA.

Wakati Stephen Curry alianza uchezaji wake, hakuna mchezaji katika historia ya NBA aliyewahi kutengeneza alama 3,000 za pointi 3 katika maisha yake ya soka, kwa sasa jambo limekuwa kawaida kwake ambaye amefikisha pointi 4,000 katika mchezo vs Sacramento Kings.

Hii hapa Orodha ya wachezaji vinara wa NBA ambao wamefunga pointi 3 nyingi.

1. Stephen Curry Pts 4,000
2. James Harden Pts 3,123
3. Ray Allen Pts 2,974
4. Damian Lillard Pts 2,794
5. Klay Thompson Pts 2,667
6. Reggie Miller Pts 2,560
7. Lebron James Pts 2,542
Ni sahihi zaidi kusema amefikisha mitupo 4000 ya pointi -3 na siyo pointi 4000, hiyo mitupo pekee imetengeneza pointi 12,000 kati ya zaidi ya 25,000 alizonazo mpaka sasa
 
Mnatakiwa kuacha huo ushamba wa kizamani sasa.
Ni kweli mkuu huo mchezo unahitaji kuwa na nguvu,stamina,pumzi maana kila muda ni kukimbia kimbia tu sasa hao matozi au mabishoo wanao wasema watachezaje sasa na wao wanachukuliwa ni watoto wa mama. Mimi ni mpenzi wa mpira wa miguu ila ukiniwekea mpira wa miguu na NBA nichague kuangalia,nitachagua NBA maana huku watu wanashindana kutafuta points muda wote yaani mchezo haupoi sio kama mpira wa miguu unakuta games zimepoa unakuja na matarajio mengi unakuta futuhi tupu plus kupoteza muda na usingizi.
 
Miaka ya 2014 kuna jamaa yangu alikuwa anacheza basketball pale Taifa indoor. Siku hana mechi na ikiwa ni weekends sijaenda job tunaenda nae kucheki mechi zingine ananipa taarifa na namna basketball inavyochezwa, points zinavyopatikana na kuhesabiwa, faul na vitu vingine.
Tokea hapo nimetokea kuipenda basketball vibaya sana.
 
Ni kweli mkuu huo mchezo unahitaji kuwa na nguvu,stamina,pumzi maana kila muda ni kukimbia kimbia tu sasa hao matozi au mabishoo wanao wasema watachezaje sasa na wao wanachukuliwa ni watoto wa mama. Mimi ni mpenzi wa mpira wa miguu ila ukiniwekea mpira wa miguu na NBA nichague kuangalia,nitachagua NBA maana huku watu wanashindana kutafuta points muda wote yaani mchezo haupoi sio kama mpira wa miguu unakuta games zimepoa unakuja na matarajio mengi unakuta futuhi tupu plus kupoteza muda na usingizi.
Kweli Mkuu. Halafu huo mtazamo ulikuwa zamani kwa sababu access ya kuangalia mchezo huo ilikuwa ni finyu kwa watu wa uswazi. Lakini sasa hivi hata kwenye simu yako tu unaweza kuangalia NBA na mashindano mengine ya kikapu.
 
Ni kweli mkuu zamani watu walikuwa wanaangalia uvaaji wa Denis Rodman wakawa wanachukulia mchezo huo niwa mabishoo na ukichukulia kipindi hicho uswazi kuvaa nguo mpya na kupendeza inachukuliwa ni kama ubishoo na hiyo mentality ipo mpaka humu if ila basketball ikipata wazamini wa kweli bongo tatasahau huu mpira wa magumashi wa simba na yanga
 
Back
Top Bottom