Step by step nilivyo agiza bidhaa kutoka AliExpress

master09

JF-Expert Member
Aug 12, 2013
808
559
Habari JF.

Kwamtazamo wangu wengi tunaogopa kuagiza vitu kutoka hizi sites kama AliExpress,ebay,Amazon n.k
Baada ya kusoma nyuzi nyingi hasa za Mwl.RCT basi namimi nikaona nijaribu.

1.Nilianza na kufungua Sanduku la Posta .

2.Kufungua Account ya Bank Nitakayo tumia kufanya manunuzi hayo .

3.Application ya AliExpress kwangu mimi.

Baada ya kupata Sanduku la Posta nikafanya research hasa kwa kupitia nyuzi humu Bank nzuri yakufanya manunuzi option zikawa mbili Access Bank na Equity Bank upande wangu nikaona Equity Bank na kufungua account Equity Bank ilikuwa siku moja napata card ya visa na fomu ya kuruhusu online transactions nilijaza sikuhiyohiyo baada ya siku mbili nikapigiwa simu kama kila kitu kiko sawa naweza fanya manunuzi.

Basi kwa mara ya kwanza tar 30 june 2019 nikajaribu card kwa kununua screwdriver ya vitu vya electronics .

N.B
Nitaendelea kutoa Update mpaka pale mzigo utakapo fika .....mpaka sasa sijapata kikwazo sehemu yeyote
2019-07-01%2019.38.50.jpeg
2019-07-01%2019.41.46.jpeg
Screenshot_2019-06-30-19-42-15.jpeg
Screenshot_2019-06-30-20-33-53.jpeg


UPDATE:

Tarehe 30 june 2019 order ilikuwa received na baada ya siku nne yaani leo tar 4 july 2019 mzigo umekuwa dispatched ....utafika Dar around 28 july mpaka 22 august 2019.
 
Baada ya kusoma nyuzi nyingi hasa za @Mwl.RCT basi namimi nikaona nijaribu.

1.Nilianza na kufungua Sanduku la Posta .

2.Kufungua Account ya Bank Nitakayo tumia kufanya manunuzi hayo .

3.Application ya AliExpress kwangu mimi.
Hongera kwa hatua uliyofikia.

Haya ndio matumizi sahihi ya mitandao ya kijamii KUPATA ELIMU na KUITUMIA ELIMU kama ulivyo fanya.

Ukiwa na changamoto yeyote usisite kuliza na wana JF watakusaidia
 
Watanzania tuache uoga mimi nimesha agiza simu zaidi ya tano kwa kupitia alixpress tena sina sanduku la posta natumia posta makao makuu Mzigo ukifika naenda kuchukua
Nimeagiza vitu vingi sana na vimefika bila shida yoyote
Muhimu ujue ku track mizigo yako ili ikifika posta utambue mapema na kuifuatilia
Maana ukitegemea kupata msg kutoka posta mara nyingine msg hazifiki

Hizo ni baadhi ya simu nilizo agiza na zikafika bila shida yoyote
Kuna item zaidi ya 30 nimeagiza na zimefika
View attachment 1144110
Screenshot_20190701-204715~2.jpeg
 
Hongera kwa hatua uliyofikia.

Haya ndio matumizi sahihi ya mitandao ya kijamii KUPATA ELIMU na KUITUMIA ELIMU kama ulivyo fanya.

Ukiwa na changamoto yeyote usisite kuliza na wana JF watakusaidia
Asante sana Mwl.RCT nikipata shida naamini utanisaidia kwa uzoefu wako.
 
Mkuu Safi kabisa wewe umenifanya sasa niagize zaidi maana nilikuwa kama na test vile nione ......mimi nina sanduku la posta kawe kwahiyo mzigo utakuja hapo au makao makuu
 
Endelea kumiminika mkuu..na mimi nipate hamasa..ila natamani kujua zaidi kuhusu manunuzi kupitia mpesa mana huku chiungutwa hakuna hizo benki.
Jana nimefanya transaction nikiwa Mbingu i milimani just fanya uwe na kadi na internet unafanya manunuzi popote tanzania ...
 
Guys naombeni mnisaidie mm niliagiza vitu na nimewasiliana na seller akaniambia kuwa vitakuwa vimefika nchini kwangu kwasababu ni miez miwil sas imepita na ili mm nipate order yangu nilitakiwa nisubir 21-53 days zimepita sas na inanyosha mzigo umetua nchini shida posta nilienda na track number hawakuweza kunisaidia nifanyeje guys naombeni nielekezwe namna ya kuuchukua mzigo wangu
IMG_2891.JPG
 
Guys naombeni mnisaidie mm niliagiza vitu na nimewasiliana na seller akaniambia kuwa vitakuwa vimefika nchini kwangu kwasababu ni miez miwil sas imepita na ili mm nipate order yangu nilitakiwa nisubir 21-53 days zimepita sas na inanyosha mzigo umetua nchini shida posta nilienda na track number hawakuweza kunisaidia nifanyeje guys naombeni nielekezwe namna ya kuuchukua mzigo wanguView attachment 1144130

Ulitumia postal address ya wapi?
 
Ukitaka mzigo ufike posta makao makuu unaandika vipi kwenye adress. Kuna mzigo nimeagiza Ila nimejaza ufike. Posta, Tanzania, na adress zangu. Msaada WA maelekezo please
 
shida ya equity bank ipo kwenye refunds.....
kwanini pesa isingie automatic waki ku refund?
 
Back
Top Bottom