Stendi mpya ya mabasi Nyegezi yaanza kazi, ni zaidi ya Airport

Stendi mpya ya mabasi ya Nyegezi jijini Mwanza imeanza kazi rasmi leo tarehe 5/6/2023 huku uzuri wake ukiwaacha hoi wananchi na kusema iko vizuri zaidi ya viwanja vingi vya ndege.

Ikumbukwe jiwe la msingi la ujenzi wa stendi hii liliwekwa na aliyekuwa Rais wa awamu ya tano Hayati Magufuli, hivyo wananchi wamemlilia tena kwenye uzinduzi wa stendi hii na kusema bila Magufuli kuwa Rais huenda ingewachukua miaka 50 kwa jiji la Mwanza kujengewa stendi nzuri kiasi hiki.

Ingejengwa tu. Uwanja wa ndege Mwanza
 
RIP JOSEPH POMBE JOHN MAGUFULI watashindanaaaaa kufuta Lagacy lakini hawataweza labda wapige mabomu ya Nyuklia kufuta alama zako. Wenye Akili tunaendelea kukukumbuka Daima.
Zitajengwa nyingi na nzuri kuliko hiyo. Subiri.
 
Hicho unachosema ni matazamio ya huyo mkurugenzi wako! Mimi kila siku napita hapo kwa maana nasafirisha abiria ndo kazi yangu! Kwa sasa mkurugenz wako anapanga kurudisha magari madogo ya magu na sumve yaanzie buzuruga halaf unajifanya unajua kumbe hujui! Abiria wanakwepa tozo ya tsh 200 za pale terminal wanakimbilia kisesa! Tata nyingi zinaanzia kisesa.
Kurudi Buzuruga haitawezekana, labda afute tu hiyo tozo ya 200
 
Daaah ila MSAMVU ishakuwa historia kwa hii mistendi ya Sasahivi Tz
Msamvu itabaki kuwa stemdi bora kabisa ,Nyege wameinenga kwenye korido,ilitakiwa ijengwe nyuma ya Usagala,na Buzuluga ingejengwa mbele ya Kisesa
 
Hizo stendi hazijajengwa miji yote. Tembea uone au wewe unasafiri kwa ndege tu.
Mimi sijawahi panda hizo ndege na pia sikuzungumzia stendi tu. Kipindi cha JPM miji mingi midogo midogo ilichipukia na kukua kwa kasi na hii ni kwa sababu alipeleka huduma za kijamii kama hospitali, pia aliweka lami na taa za barabarani kwenye vimiji vidogo vidogo mfano Katoro, Buseresere, Magugu, Igawa nk hii ilisaidia wafanyabiashara hasa wamachinga kufanya kazi hadi usiku.
 
Msamvu itabaki kuwa stemdi bora kabisa ,Nyege wameinenga kwenye korido,ilitakiwa ijengwe nyuma ya Usagala,na Buzuluga ingejengwa mbele ya Kisesa
Msamvu stend au banda la kuku stend Nzuri itabaki kuwa Magufuri Mbezi tu then inafuata Dom, Mwanza na stend nyengine mpya Msamvu ilipendelewa kipindi hiko inahitaji ijengwe ya kisasa
 
Mimi sijawahi panda hizo ndege na pia sikuzungumzia stendi tu. Kipindi cha JPM miji mingi midogo midogo ilichipukia na kukua kwa kasi na hii ni kwa sababu alipeleka huduma za kijamii kama hospitali, pia aliweka lami na taa za barabarani kwenye vimiji vidogo vidogo mfano Katoro, Buseresere, Magugu, Igawa nk hii ilisaidia wafanyabiashara hasa wamachinga kufanya kazi hadi usiku.
Uko sahihi
 
Back
Top Bottom