STEALTH (LOW OBSERVABLE) TECHNOLOGY | Teknolojia ya ndege kutoonekana/kutotambulika na rada (RADAR)

Japan ni miongoni mwa mataifa machache yenye mpango wa uundwaji wa ndege mahususi za stealth ambapo uzalishwaji wake utaanza mwaka 2031, miaka takribani 11 ijayo.

Wizara ya Ulinzi ya Japan imekwisha tenga dola za Kimarekani milioni 102 katika bajeti ya mwaka huu sawa na shilingi za Kitanzania takribani bilioni 237 kwa ajili ya utekelezwaji wa mpango huo sambamba na gharama zingine. Ndege hizo zitaanza kutumika rasmi panapo mwaka 2035 baada ya uzalishwaji wake.

View attachment 1503728
Mbona ela ndogo sana iyo.F-22 mpaka imekamilika imetumia Dola bilion 57 na Su-57 ya warusi imetumia dola bilioni 11.sasa iyo ela si ya kuunda kiti chake tu bado ndege yenyewe
 
Kiasi hicho cha fedha ni katika bajeti ya mwaka huu pekee (2020) kwa ajili ya hatua ya mwanzo (basic design).

Baada ya hapo kuna hatua zitakazofuata kabla ya kuanza uzalishaji. Maana yake ni kwamba, kutakuwa na fungu jipya la fedha katika bajeti ijayo na baada ya hiyo.
 
Hivi wazee wa sumbawanga idea zao haziwezi kutoa kitu cha 'Stealth'?
Hakivile ni kama tunasindikiza tu wenzetu kwenye masuala ya technology.
Kuna mtu mmoja aliwahi kusema, "everyone is good at something."

Mimi naongezea kwamba, everyone is good at something under certain circumstances.

Kila mtu, kuna kitu ambacho anaweza kukifanya kikaleta impact na faida kubwa katika jamii lakini ni katika mazingira fulani yenye kuwezesha hilo kutokea ama kufanyika.
 
Mradi wa ndege ya stealth wa Japan unaofahamika kama F-X unakadiriwa kuwa utafikia dola za Kimarekani bilioni 40 mpaka kukamilika kwake huku ndege zipatazo mia (100) zikiwa katika mpango wa uzalishwaji.

Kampuni ya Mitsubishi (Mitsubishi Heavy Industries) ya nchini Japan ndio kampuni yenye kuunda ndege hiyo huku pia kukiwa na uwezekano wa 'kolabo' (collaboration) na kampuni zingine za kimataifa hususani kutoka Marekani (Lockheed Martin, Boeing, Northrop Grumman) pamoja na Uingereza (BAE Systems).
 
Lockheed Martin hawa jamaa naona wana research za maana aisee. Maana huwa wanakuja na vitu vya maana.
 
Hao si walikataliwa na Japan kutengeneza redesign ya F-22 + F-35. Japan ilichagua kutumia teknolojia ya nyumbani ili iwe na maaamuzi zaidi juu ya mradi huo na kuzungusha hela zake. Ndege hizo tutarajie ziwe na gharama kubwa mno.
 
Yeah! Wako vizuri.

Bila kuwasahau pia wengine kama vile Northrop Grumman, Boeing pamoja na General Dynamics.

Pia, kuna wengine maarufu nao walikuwa wakiitwa United Technologies na mwingine Raytheon ambao wameungana juzijuzi. Kwa sasa ni kampuni moja, inaitwa Raytheon Technologies.
 
Hao si walikataliwa na Japan kutengeneza redesign ya F-22 + F-35. Japan ilichagua kutumia teknolojia ya nyumbani ili iwe na maaamuzi zaidi juu ya mradi huo na kuzungusha hela zake. Ndege hizo tutarajie ziwe na gharama kubwa mno.
Ndio. Hata Boeing na BAE Systems pia waliwasilisha designs, Japan ikazikataa miezi michache iliyopita.

Mazungumzo bado yanafanyika maana kuna masuala mengi yanayotakiwa kufanyiwa kazi likiwemo suala la suppliers wa components mbalimbali pamoja na hilo suala la collaboration ambalo bado liko mezani.
 
1594677289723.png

1594677516385.png

An In-Depth Analysis of how Serbs Were Able to Shoot Down An F-117 Stealth Fighter during Operation Allied Force - The Aviation Geek Club
 
Ndio. Hata Boeing na BAE Systems pia waliwasilisha designs, Japan ikazikataa miezi michache iliyopita.

Mazungumzo bado yanafanyika maana kuna masuala mengi yanayotakiwa kufanyiwa kazi likiwemo suala la suppliers wa components mbalimbali pamoja na hilo suala la collaboration ambalo bado liko mezani.
Sasa BAE hawajatengeneza za Ulaya wakishirikiana na MBDA watawezaje kutengeneza za Japan. Yote yaleyale bora Japan amchukue Mitsubishi.
Lockheed Martin watoe components tu basi. Kina P&W au General Dynamics watoe engine.
 
Uwezekano upo. Hao BAE Systems ni wazuri katika sekta ya defence pamoja na aerospace na wameshafanya collaborations na kampuni zingine mbalimbali katika masuala hayo. Isitoshe, nao wapo katika project yao mpya ya sixth-generation fighter maarufu kama 'Tempest'.

Japan ina mpango wa kupunguza costs za mradi pamoja na muda hivyo kuna possibility ya mkataba wa partnership ama ushirikiano na kampuni moja ya kigeni au zaidi kabla ya mwaka huu kuisha. Tusubiri, tuone kile kitakachojiri.
 
Kumuachia mradi BAE Systems hakuna faida yoyote ya haraka au uzoefu. Hawajawahi kutengeneza stealth, the same na Mitsubishi. Wanatengeneza components za ndege, Mitsubishi wanatengeneza ndege tangu WW2 zile kina Zero zilizosumbua mwanzoni mwa Pacific theater.
Ukimpa mradi Lockheed Martin tunajua unataka kuwahisha na ufanisi pamoja na gharama pungufu, ukimpa BAE ni kwenda kupambana. Kwa kuwa ni masuala ya kuwa huru kwenye silaha acha waongoze wao mradi. Ndio maana wanataka watengeneze na shore based missile defense wakati THAAD na Aegis wanapewa na US.
Wanataka kujitegemea kwenye ulinzi.
 
Mradi unasimamiwa na kampuni za ndani lakini kunakuwa na partnership na foreign contractor mmoja au zaidi. Pia, partnership hiyo si katika masuala ya stealth designing pekee, bali kuna zaidi ya hapo. Kuna masuala mengine kama vile mission systems, electronic support (ES) pamoja na electronic systems kwa ujumla wake. BAE Systems ni wazuri katika hayo hata kampuni zingine kama vile Northrop Grumman huwa inawatumia katika masuala mbalimbali.

BAE Systems pia ni major partner katika mradi wa F-35 Lightning II stealth fighter wa Lockheed Martin na imekwisha fanya na inaendeleza projects zake mbalimbali zinazohusiana na unmanned aerial vehicles (UAVs) zenye uwezo wa stealth. Uzoefu huo unaweza kuwasaidia Wajapan na pengine ndio sababu ya wao kujaribu kujielekeza kwao. Hata hivyo bado maamuzi hayajafanyika kuhusiana na hao foreign contractors.
 
Back
Top Bottom