Hasara nyingine kwa serikali. Ama kweli usicheze na mwenye akili.
Kilichofanyika hapa ni sawa na mtu mwenye shamba la mahindi (dhahabu) lililokuwa na mashina machache yaliyopo hapa na pale ya mbaazi (copper) na alizeti (silver). Alikuwa anavuna kwa kutumia combine harvester iliyokuwa inachambua mahindi punje kubwa na kuacha mahindi yenye punje ndogo, yakiwa yamechanganyika na mbaazi na alizeti.
Mchanganyiko wa mahindi punje ndogo, mbaazi na alizeti ulikuwa unapelekwa kwenye kiwanda chenye uwezo wa kutenganisha. Lakini katika mchanganyiko huo, katika thamani, 80% yalikuwa ni mahindi yenye punje ndogo.
Baada ya kuzuiwa kupelekwa mchanganyiko wa mahindi yenye punje ndogo, mbaazi na alizeti kwenye kiwanda, mvunaji ameamua kutafuta harvester mpya ambayo sasa itakuwa na uwezo wa kutambua mahindi yote hata kama yana punje ndogo kwa ufanisi wa 80%. Anaamua kuvuna mahindi tu, na kuacha mahindi ya punje ndogo 20% pamoja na mbaazi na alizeti, vyote viozee shambani.
Kwa sababu mchanganyiko wa mahindi yenye punje ndogo, alizeti na mbaazi, katika thamani, 80% yalikuwa mahindi ya pune ndogo, sasa alizeti na mbaazi haviwezi kuvunwa na kupelekwa kiwandani kwa faida.
Ikumbukwe kuwa silver na copper katika ile Au-Cu-Ag ore, concentration yake haifiki hata 0.1%. Ilikuwa inaongezeka baada ya kufanya concentration. Sasa haitakuwepo concentration. Hivyo Cu na Ag havitaweza kuwa extracted kwa faida.
Nini maana yake?
1) Ag itabakia kwenye tailings za mgodi, na haitachenjuliwa tena na kuuzwa
2) Cu itabakia kwenye tailings, haitachenjuliwa wala kuuzwa tena
3) Fine Au 20% itabakia kwenye tailings, na haitaweza kuchenjuliwa tena. Ifahamike kuwa mgodi wa Buzwagi average grade per tone ni 4g. Ina maana 20% ya average grade ni 0.8g/t.
4) Contractor wa usafirishaji makinikia na wafanyakazi wake, mambo yameishia hapo
5) Vituo vya mafuta mapato yake yatapungua
6) Mapato ya bandari yaliyohusiana na usafirishaji wa concentrates yameishia hapo
7) Kodi iliyokuwa ikitokana na mauzo ya concentrate ya Au-Cu-Ag, yameishia hapo.
8) Hakutajengwa kiwanda cha kuchenjua concentrates
Tulichoongeza ni royalty ya gold bar, na furaha ya moyo kuwa hatuibiwi kwa sababu sasa dhahabu inayozalishwa tutaiona kwa macho yetu, haipo katika mwonekano wa mchanga.
Nimeamini mwenye akili hakosi jibu. Wakati wote huwa na jibu la kukabiliana na mazingira yanayomzunguka. Mjinga unaweza kudhani umepata kumbe umepatikana