Startimes Tanzania: Support thread (maswali, maoni na ushauri)

Hongera sana na ahsanteni statimes.

Mmenitendea haki sana leo.

1. Jana nilifanya malipo ya kifurushi cha 21000 bahati mbaya nikakosea tarakimu ya mwisho ya smatcard. Kwa vile nililipia kwa nmb mobile niliona ujumbe wa nmb mobile kuwa nimelipia kifurushi cha ststimes ila bado chanels hazikufunguka.

Leo jumapili nikawapigia na wakapokea haraka. Baada ya kukagua akaunt yangu ikaonekana haijaingia pesa yoyote. Basi muhudumu akaniambia huenda nimelipia akaunti isioyenyewe, basi kweli ikabidi nirudi kwenye statement za malipo ya nmb na kugundu nilifanya kosa la namba moja ya mwisho haikuwa sahihi.

Kuwapigia mara ya pili nikapokelewa haraka, na kujibu maswali kadhaa na kuahidiwa kurudishiwa malipo kwenye akaunti yangu.

Haikupita dk 10 watoto wanachekelea wananiambia baba tayari!

Big up bazee ba statimes
Karibu sana startimea
 
Startimes hamna majibu humu hivi kwanini msiwe specific mpaka kupigiana simu,mfano nataka kuunga kifurushi mpaka mpigiwe, nadhani kuwe na chaguo katika mfumo wa ulipaji kifurushi, mfano kwa m-pesa nikisha ingiza namba ya smart card ije viwango vya kulipia na majina ya vifurushi,mwisho naomba kufahamu kifurushi cha wiki cha smart ni shilingi ngapi.
tunafanya maboresho kwenye njia za malipo hivi karibuni kutakuwa na mabadiliko
 
Kuna ndugu yangu kung'amuzi chake ni Cha zamani,ila ghafla tu hakionyeshi,yaani hakipitishi moto kabisa,anauliza mnatengeneza Bure au mpaka alipie,au akirudisha Cha zamani Ili apate kipya Kuna punguzo?
 
Back
Top Bottom