Startimes ipo nyuma ya nani?

Startimes ipo nyuma ya nani?

TRACE

Senior Member
Joined
Jul 4, 2008
Posts
120
Reaction score
46
Ndio wanajamvi, nimeonelea niliweke hapa ingawaje yawezekana limeshawahi kujadiliwa.

Nilikuwa naangalia UBC TV na nikaona tangazo la StarTimes na nikashtuka kwa kuona lile tangazo eti labda kwa mawazo yangu nilidhani ni part ya TBC na labda kungekuwa na mechanism nyingine ya kuwafikishia products za TBC.

Na nikawaza kama ni mali ya TBC kwanini wasingetumia nembo ya TBC kutangaza hivyo ving'amuzi ili TBC ijulikane zaidi na kwanini wachina wako mbele kwenye hiyo StarTimes kuliko Wa TZ hasa katika top layer?

Ni kweli kadili ya maelezo waliyokuwa wanatupatia TBC tununue ving'amuzi ili tufurahie WorldCup 2010 na wakati 90% ya mechi au karibu zote twaziona TBC1 sio kuwahadaa walionunue bila kupata extra benefits?

Wanaandaa mazingira ya kumtajirisha nani au wamekuja kwa mgongo wa nani? Wapo kwa ajili ya Watanzania na wakitufanya kama GTV kuna sehemu ya kwenda kudai haki zetu au watauacha kama GTV?

Kama kuna sehemu nimepotoka ila kila lenye wanzo lina mwisho naomba nieleweshwe.
 
Kweli watu wengi wananung'unika, kwamba wamenunua ving'amuzi lakini michezo yote inaoneka TBC1 kama kawaida! Aliyenunua haoni tofauti! Nadhani ni kuibiwa tu na wachina, maana hakuna hata serikali ya kulinda maslahi ya mwanachi!
 
Awali ilikuwa games zote zionekana TBC2 lakini naona baadhi ya vigogo wakaingilia kati kuwa mechi zionyeshwe TBC1 ili wasio na uwezo wa kununua hivyo vinini sijui na wao waweze kuona.
 
Kweli watu wengi wananung'unika, kwamba wamenunua ving'amuzi lakini michezo yote inaoneka TBC1 kama kawaida! Aliyenunua haoni tofauti! Nadhani ni kuibiwa tu na wachina, maana hakuna hata serikali ya kulinda maslahi ya mwanachi!

Jamani ving'amuzi si kwa ajili ya kombe la dunia pekee. Kuna vipindi vingine vizuri ambavyo having'amuliki kwa antena ya kawaida lakini nyie mtaving'amua...
 
Watanzania ni rangi mbili, mwanzo kulikuwa na malalamiko mengi humu ndani ya JF kuwa kwanini mechi hizo za soka zisioneshwe TBC1 kwa kuwa wao TBC1 walipewa bure na FIFA haki ya kuonesha michuano hiyo, TBC1 wamesikia kilio hicho (?), sasa malalamiko mengine eti kwa nini sasa mechi hizo zote zinaonekana TBC1 wakati kuna watu wamenunua ving'amuzi vya TBC2! sasa lipi jema?
 
Tatizo nilinunua ving'amuzi viwili kimaja nyumbani na kingine offisini; ajabu cha offisini (mitaa ya posta) ZERO signal kabisa antena ipo juu ya ghorofa. sasa natumia chadema tu. Nahisi hivi ving'amuzi vinatumia minara ya TCB kisarawe.kama ingekuwa satelite isingekuwa tabu
 
Nyie mlinunua ving'amuzi kwa ajili ya kuangalia mechi za wc tu? Kwahiyo michuano ikiiisha mtavitupa hivyo ving'amuzi?
 
Naona kweli nililisema hapa juu limeeleweka na kwa kutoa maelekezo kidogo ni kuwa wote hatujakataa TBC1 kuonyesha WC kwa mechi zote kama ilivyo sasa ila kwa upande wangu ni kitendo chao kwenda TBC1 kutueleza kwamba watu wasiponunua hawataweza kuona WC2010 na wakati siyo.Walitumia hela yetu kutudanganya na sasa hakuna mtu anayeweza kuwahoji au kuwawajibisha.

Mimi nilipenda iwe hivi ilivyo sasa na kama mtu angependa kununua hicho king'amuzi chao na kupata Channel za ziada na sijui hiyo quality ya picha wanayoisema angeenda na siyo kudanganya Watanzania ambao wangeweza kuangalia kupitia antenna zao walizozizoea na kuelekeza Tshs.70,000/= kwenye matumizi mengine ya muhimu zaidi.

Najua kuwa Wa Tanzania ni wepesi kuhadaiwa ila kwa michezo hii tutafika kweli au siku akili zetu zitarudi na kujua mchele ni upi na pumba ni zipi? Tido kweli umeweza kuwahadaa wenzako kiasi hiki?

Nilisita kununua king'amuzi eti sijui cha StarTimes na kubakia na cha Easy Television kwani yaliyonikuta kwa GTV sitaki yanikute tena.Na nafaidi WC 2010 kupitia TBC1 na vile vile UBC pamoja na kufaidi channel nyingine nyingi tu.

Nini kifuatacho au ndio wameliwa tena? Watakuja kuwaomba msamaha Wa TZ kwa kuwadanganya au watakaa kimya??
 
kaka lakini ukumbuke kuna swala la channel zote kulipiwa siku zijazo, so aliyenunua decoder anakuwa ameshamaliza kila kitu, kitakachotakiwa ni appropriate cards za kuingiza kwenye decoder whether uwe, gtv, startimes, easy times etc.

Nadhani tatizo hapani je serikali inamlinda vipi huyu mnunuzi, na sio kuwalaumu watanzania kuwa wanadanganywa!
 
Mimi nilipenda iwe hivi ilivyo sasa na kama mtu angependa kununua hicho king'amuzi chao na kupata Channel za ziada na sijui hiyo quality ya picha wanayoisema angeenda na siyo kudanganya Watanzania ambao wangeweza kuangalia kupitia antenna zao walizozizoea na kuelekeza Tshs.70,000/= kwenye matumizi mengine ya muhimu zaidi.
Inapendeza tu kuwa na hiki king'amuzi kwani unapata channels za ziada kwa ubora zaidi. Nilikuwa nampango wa kununua Dish la futi 8 ambalo lingenighalimu takribani Tshs. 400000/- (dish, Bomba, Jeki, LNB's, Cable na ufundi). Vile vile ada yao sio kubwa sana kulinganisha na GTV au hiyo DSTV iliyo hai. Hongera TBC. Hongera Muhando kwa hili.
 
attachment.php
 
Ukiacha mbali mambo ya WC, mi napenda sana programmes zingine zinazorushwa na hawa Star times, na hivyo sijuti kununua king'amuzi hiki!...Pia watoto wanafurahia sana programmes bomba za kitoto kama Kid-co etc!..kwaujumla imejazia kila idara!..I dont care to which dog its behind!
 
Uko sahihi PakaJimmy maana kilamara huwa tunajadili watu badala ya HOJA.. Kama hii kampuni inakosea, ama kuna ufisadi tujadili bila kujali majina.
 
.I dont care to which dog its behind!

Hapa ndipo wadanganyika taabu yetu ilipo. kwani unaposema hujali aliye nyuma ya mradi huu hujui kwamba aliye nyuma ya mradi huu inawezekana kwamba alikwapua fedha za umma, au anatumia shirika la umma kwa faida yake?

kama hutaki kujua aliye nyuma ya mradi unaishi kwa kufuata mantiki au una mantiki ya kufuata kuishi!!
 
Ni ukweli usiopingika kuwa kuwaishwa kwa kuhamia digitali kulikuwa na dhana ya kiulaji, kifisadi na kutengenezea watu fulani nafasi za kazi.Vinara na waratibu wa mpango huu ni Star Times. Kuna mambo mengi ya kiudhahifu yanayothibitisha haya.1. StarTimeswmeshindwa kurusha signal zenye ubora wa kiditali. Ni madudu tu.2. Wamekuwa na miolongo mingi kuhusu upokeaji wa matangazo yao ikiwa ni pamoja na kutoa maelekezo ya kugeuza antena nk3. Star TV sasa wamejitoa na kusababisha lazima sasa ya kununua king'amzi cha Continental . Nao ITV wako njiani kujitoa ili wauze digitek.Knachochukiza sasa ni kwanini serikali ilituhakikishia kuwa free TVs zitaendelea kupatikana kupitia StarTimes na sasa wamejitoa. Hivi StarTimes wanawajibika vp?Tujadili.
 
Startimes = TBC = CCM.
Hapo usitegemee ubora wowote since wanahusiana na CCM!!
 
Dah! Kwa kweli hapa tumefanyiwa usanii Ina maana ili uone local Chanel's unahitaji kununua vingamuzi 4 kila local Chanel na king'amuzi chake!
Je Huyu mtanzania maskini ataweza kweli?
Chukua hatua!
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom