Kuondolewa Kwa Channel ya Emmanuel Tv Katika Kingamuzi cha Startime... | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Kuondolewa Kwa Channel ya Emmanuel Tv Katika Kingamuzi cha Startime...

Discussion in 'Entertainment' started by PISTO LERO, Aug 23, 2012.

 1. PISTO LERO

  PISTO LERO JF-Expert Member

  #1
  Aug 23, 2012
  Joined: Mar 8, 2011
  Messages: 2,821
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 135
  Itakumbukwa kuwa katikati ya mwezi huu wa nane TBC kupitia Star Media Group ( Startime) waliongeza chanel ya Emannuel Tv.
  Lakini baada ya muda wakaiondoa na kuweka chanel nyingine kitendo hicho kiliwaudhi watu wengi haswa haswa waumini wa kikristu ukizingatia wengi wao walikuwa wakiisubiri kwa hamu na wengi walishukuru sana baada ya startime kuiweka.

  Kitendo cha chanel hiyo kuondolewa kilipelekea wapenzi wa chanel hiyo kwenda kwa wingi na wengine kupiga simu kutaka kujua kulikoni.

  Mmoja wa watu hao ni mimi mwenyewe nikifatana na watu wengine kama wanne hivi,lakini cha kushangaza na kufurahisha zaidi baadi ya kufika Startime tulikutana na watu wengine nao walikuwa na maswali hayohayo.

  Tuliungana na kuanza kumuliza mwenyeji wetu nini sababu ya kuiondoa chanel hiyo kwani ilivutia watu wengi kununua ving'amuzi na pia ilikuwa ni faida kwao kwani wengi tuliokuwa hatutumii tena ving'amuvi tulivutiwa na chanel hiyo na kuanza kuvitumia tena.

  Majibu tuliyo pewa yana shangaza sana kama siyo kustaajabisha,kwanza mwenyeji huyo alituomba radhi kwa kitendo hicho na kusema kulitokea matatizo na usumbufu kwa baadi ya watu hivyo wakaamua kuiondoa.

  Baada ya kumbana sana kwa maswali akageuza kibao na kutuambia kuwa wao ndio wanaoongeza chanel na kuiondoa pale wanapoona inafaa na hakuna wa kuwaingilia, mwenyeji huyo aliondoka na kutuacha na maswali yetu, kasha baada ya kama dakika mbili alirudi na kutuamba amemaliza hivyo akatutaka kuondoka.

  Lakini kabla hatujaondoka alikuja mhudumu mwingine na baada ya kutukuta tunalalamika akatuuliza nini tatiza,tulimwaleza kwakuwa alionekana kidogo mstaarabu na hapo ndipo ukweli ukawekwa wazi ila alikuwa na wasiwasi sana na aliomba kutusindikiza nje ya jingo hilo huku akitutonya nini kilicho tokea.
  Alitueleza kuwa lilitoka shinikizo kutoka kikundi Fulani na baada ya kuzozana nao kwa muda juu ya kuiondoa hiyo chanel kwa sababu ambazo kijana huyo aligoma kutueleza,watuhao waliondoka na kurudi tema kama mara tatu na hoja yao ilikuwa hiyohiyo.

  Tulipo muuliza ni watu gani hao mvujisha siri huyo hakuwa tayari kueleza,anasema baada ya muda kupita bila kuwaona watu hao wakajua upepo umepita lakini kumbe sivyo kwani walipokea shinikizo linguine kwa barua kutoka serikalini na sasa ilikuwa siyo ombi tena bali ni lazima.

  Tukamuuliza barua hiyo imesainiwa na nani kama anaweza kutueleza lakini kama kawaida hakusema bali alituambia sehemu ya barua hiyo ilieleza kuwa chanell hiyo si salama kwa usalama wa taifa hivyo iondolewe mara moja nao ikabidi waidoe kuepusha shari.tuliishia hapo na kuangana

  KWA MAWAZO YAKO WEWE MTANZANIA UNAPATA PICHA GANI KATIKA HILI.JE NINI KIFANYIKE.
   
 2. PakaJimmy

  PakaJimmy JF-Expert Member

  #2
  Aug 23, 2012
  Joined: Apr 29, 2009
  Messages: 16,236
  Likes Received: 309
  Trophy Points: 180
  Du, hii kali.
  Naipenda sn Tv Emmanuel na TBJoshua.
  Nashindwa kuunganisha dots hapo jamani, sababu ya UwT kukataa hii channel isionyeshwe!
  Inavuruga matajiri wakuu serkalini ambao ni mafree-mason nn?
   
 3. bibikuku

  bibikuku JF-Expert Member

  #3
  Aug 23, 2012
  Joined: Feb 16, 2011
  Messages: 828
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 35
  Unawawakilisha akinanani hao WENGI unaowasema? na wamekutuma au umejituma kusema? Nadhani ungeandika kwa binafsi yako. By the way, Inachosha kusoma, unaonaje ukiweka paragraphs mkuu?
   
 4. Edson

  Edson JF-Expert Member

  #4
  Aug 23, 2012
  Joined: Mar 7, 2009
  Messages: 9,202
  Likes Received: 720
  Trophy Points: 280
  ni kweli haifai na mwisho ni tareh 31 november.......
   
 5. only83

  only83 JF-Expert Member

  #5
  Aug 23, 2012
  Joined: Oct 15, 2010
  Messages: 5,252
  Likes Received: 445
  Trophy Points: 180
  Mimi sio mpenzi wa TB Joshua, ila nashindwa kupata muunganiko wa Immanuel TV na usalama wa Taifa...nadhani kama ni kweli ifike kipindi serikali iwe serious kidogo na mambo yake, sasa kuna uhusiano gani wa Immanuel TV na umoja na mshikamano wa Taifa..mbona hapa nchini tuna Radio na TV station nyingi tu za kidini? Lakini pia mleta thread nadhani na wewe tupe data vizuri na jaribu kuiweka thread yako kisomi.
   
 6. matungusha

  matungusha JF-Expert Member

  #6
  Aug 23, 2012
  Joined: Dec 29, 2010
  Messages: 596
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 35
  duh kweli mwendawazimu haaachi kuhaha!!!! sioni sabab za kuiondoa hii channel alaf radio ya majungu thidi ya ukristo bado wanaendelea kutangaza propaganda zao
   
 7. hendeboy

  hendeboy JF-Expert Member

  #7
  Aug 23, 2012
  Joined: Nov 5, 2010
  Messages: 219
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  kwa mawazo yangu nahisi wanasubiri zoezi la sensa lipite
   
 8. Zogwale

  Zogwale JF-Expert Member

  #8
  Aug 23, 2012
  Joined: Jul 10, 2008
  Messages: 11,613
  Likes Received: 825
  Trophy Points: 280
  Kweli Tanzania inahitaji maombi sana!!! But tunasema eti Tanzania haina dini na viongozi wake wanatakiwa wasiendeshe Taifa hili kwa udini? But Tanzania baadhi ya viongozi wake wanatuongoza kwa udini. Haya mambo ya udini hayakuwepo awamu ya kwanza; yakaibuka awamu ya pili: yakazimika awamu ya tatu: na sasa yakaibuka awamu ya nne. Wenye mapenzi mema na nchi hii, tujifunze kwa awamu hizo na tuamue sasa upande unaofaa. Huu mwingine unatuyumbisha live.
   
 9. Raia Fulani

  Raia Fulani JF-Expert Member

  #9
  Aug 23, 2012
  Joined: Mar 12, 2009
  Messages: 10,219
  Likes Received: 83
  Trophy Points: 145
  kwa hiyo hili Taifa si secular tena?
   
 10. M

  Msendekwa JF-Expert Member

  #10
  Aug 23, 2012
  Joined: Mar 11, 2012
  Messages: 440
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 35
  Iko wz sababu ya kuizuia hiyo TV.
  Huyo TB si ndo alimtabiria EL kuwa Rais wa 5 wa Tz?
  Hamuoni kuwa EL anaweza kuwa anaitumia kuutangaza utabiri huo kila siku via TV hiyo, kuaminisha waTZ kuwa yeye kuwa Rais ni kutimiza unabii?
  Bila shaka wapinzani wa EL wasingekuwa tayari kuona hilo linatimia.
   
 11. Tora Bora

  Tora Bora Member

  #11
  Aug 23, 2012
  Joined: Aug 18, 2012
  Messages: 10
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  tanzania ni yetu sote.
   
 12. naumbu

  naumbu JF-Expert Member

  #12
  Aug 23, 2012
  Joined: Oct 28, 2010
  Messages: 3,322
  Likes Received: 3,840
  Trophy Points: 280
  There we go again
   
 13. o

  oyaoya JF-Expert Member

  #13
  Aug 23, 2012
  Joined: Mar 4, 2012
  Messages: 277
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  Watu kama nyie ndiyo mnaosababisha vichwa maji wengine wa upande wa pili wenye akili kama zako waendelee kugomea hata sensa, badala ya kuwa objective wewe unaegemea uliko. Kungekuwa na option ya kuporomosha pii za members humu ungetoka kwenye hiyo gold yako hadi mchanga...
   
 14. Njowepo

  Njowepo JF-Expert Member

  #14
  Aug 23, 2012
  Joined: Feb 26, 2008
  Messages: 9,296
  Likes Received: 381
  Trophy Points: 180
  Bifu zao na EL tuu si unajua huyu mmasai alishaenda safisha njia kwa nabii
   
 15. Donnie Charlie

  Donnie Charlie JF-Expert Member

  #15
  Aug 23, 2012
  Joined: Sep 16, 2009
  Messages: 6,577
  Likes Received: 846
  Trophy Points: 280
  Nahisi hujamwelewa jamaa!
   
 16. Mshuza2

  Mshuza2 JF-Expert Member

  #16
  Aug 23, 2012
  Joined: Dec 27, 2010
  Messages: 4,115
  Likes Received: 1,744
  Trophy Points: 280
  Kwi kwi kwi kwi.....punguza jazba!
   
 17. Ruttashobolwa

  Ruttashobolwa JF-Expert Member

  #17
  Aug 23, 2012
  Joined: Feb 22, 2012
  Messages: 43,747
  Likes Received: 12,829
  Trophy Points: 280
  Mshana ni mtu muoga sana!
   
 18. Zogwale

  Zogwale JF-Expert Member

  #18
  Aug 23, 2012
  Joined: Jul 10, 2008
  Messages: 11,613
  Likes Received: 825
  Trophy Points: 280
  Mkuu nimeshampeleka sehemu inayohusika. Ataheshimu hii JF. Ni huru kwa uhuru wa mawazo ambayo hayatumii lugha chafu kwa namna yoyote ile. Huu ni mwaka wangu wa 5 hapa sijawahi kutumia lugha mbaya wala kupewa karipio maana nafuata taratibu.
   
 19. Arushaone

  Arushaone JF-Expert Member

  #19
  Aug 23, 2012
  Joined: Mar 31, 2012
  Messages: 14,366
  Likes Received: 621
  Trophy Points: 280
  Mungu tunusuru na janga la udini hapa tanganyika, na watu wote semeni 'amen.'
   
 20. Mohamedi Mtoi

  Mohamedi Mtoi R I P

  #20
  Aug 23, 2012
  Joined: Dec 11, 2010
  Messages: 3,326
  Likes Received: 44
  Trophy Points: 0
  Kwa mujibu wa mkataba wa mbovu startimes ni kwamba "Wana haki ya kuongeza au kuondoa channel yoyote bila kutoa taarifa"

  Hapa wa kulaumiwa sio startimes bali mapoyoyo walio kubali kuingia mkata mbovu kama ule.
   
Loading...