Stars yalipa kisasi kwa Msumbiji | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Stars yalipa kisasi kwa Msumbiji

Discussion in 'Sports' started by JuaKali, Nov 20, 2008.

 1. JuaKali

  JuaKali JF-Expert Member

  #1
  Nov 20, 2008
  Joined: Nov 14, 2007
  Messages: 785
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 35
  Timu ya taifa ya Tanzania, Taifa Stars, jana ililipa kisasi baada ya kuifunga Msumbiji `The Mambas` kwa bao 1-0 katika mchezo wa kimataifa wa kirafiki uliofanyika kwenye uwanja mkuu wa taifa jijini Dar es Salaam.

  Stars ilipokea kipigo kama hicho kutoka kwa Msumbiji wakati timu hizo zilipokutana Septemba 8 mwaka jana kwenye uwanja huohuo mkuu wa taifa.

  Baada ya kukukuruka kwa dakika 78 ikitafuta bao katika mchezo huo wa jana, Stars hatimaye ilifanikiwa kuona mwezi katika dakika ya 79 baada ya Kigi Makassi kufunga akipokea pasi kutoka kwa Mrisho Ngasa aliyeuwahi mpira uliopigwa na Abdi Kassim.

  Dakika 22 Msumbiji ilikosa bao kupitia kwa Alimiro Lobo baada ya krosi safi iliyopigwa na mchezaji mmoja wa timu hiyo na kuokolewa na Godfrey Bonny wa Stars na kumkuta Lobo aliyeshindwa kufunga licha ya kuwa katika nafasi nzuri.

  Jerry Tegete dakika sita baadae naye alishindwa kufunga akiwa ndani ya mita 18 baada ya beki wa Msumbiji Antonio Gravata kuuwahi mpira na kuokoa hatari katika lango la Msumbiji.

  Idd Moshi Boban nusura aipatie Stars bao katika dakika ya 35 lakini alishindwa kumalizia kazi nzuri iliyofanywa na Juma Jabu baada ya kupiga shuti dhaifu na kuokolewa na beki wa Msumbiji Guilherme Manhique.

  Msumbiji ilifanya shambulio jingine la nguvu katika dakika ya 44 lakini Antonio Gravata alishindwa kuifungia bao baada ya kupaisha mpira juu ya goli akiunganisha vibaya krosi ya Ticotico.

  Stars kupitia kwa beki wake Shadrack Nsajigwa nusura ifunge baada ya mchezaji huyo kupanda na kupiga shuti kali lakini kipa wa Msumbuji Marcelino Cumbane alifanya kazi nzuri kuokoa mpira huo kabla haujatinga wavuni.

  Kocha wa Stars, Marcio Maximo alisema baada ya mchezo huo, kuwa mchezo ulikuwa mgumu kama alivyotarajia na Msumbiji walicheza vizuri licha ya kufungwa kwani walipata nafasi nyingi lakini walishindwa kuzitumia.

  Alisema kuwa ushndi huo utawaongezea ari wachezaji wake kwa ajili ya pambano lijalo dhidi ya Sudan litakalofanyika Novemba 29 jijini Dar es Salaam kusaka kufuzu kwa fainali za Mataifa ya Afrika kwa wachezaji wanaocheza soka katika ligi za nyumbani tu.

  Naye kocha wa Msumbiji, Mooij Martinus alisema kuwa ushindi huo ni zawadi tosha ya Krismas kwa Stars pia aliweapongeza wapinzani wao kwa ushindi huo, ambapo alisisitiza kuwa kwa sasa timu yake inajifua kwa ajili ya hatua ya pili ya kufuzu kwa mashindano ya Mataifa ya Afrika na Kombe la Dunia.

  Timu zilikuwa; Taifa Stars: Shabaan Dihile, Shadrack Nsajigwa, Juma Jabu, Nadir Haroub `Cannavaro`, Salum Sued, Godfrey Bonny, Mrisho Ngassa/Mussa Hassan Mgosi (dk.89), Henry Joseph/Nurdin Bakari (dk.74), Jerry Tegete/Nizar Khalfan (dk. 59), Haruna Moshi `Boban`/Abdi Kassim (dk.71) na Athumani Iddi `Chuji\'/Kigi Makassi (dk.63).

  Msumbiji: Marcelino Cumbane, Antonio Gravata, Gonclaves Fumo/Momed Hagi (dk. 59), Elias Pelembe, Manuel Bucuane, Dario Monteiro/Lus Muchue (dk.55), Guilherme Manhique/Nasser Carimo (dk.77), Carlos Parruque/Carlos Chimomole (dk.89), Francisco Massinga, Alimiro Lobo na Fanuel Massingue
   
 2. RR

  RR JF-Expert Member

  #2
  Nov 20, 2008
  Joined: Mar 17, 2007
  Messages: 6,719
  Likes Received: 206
  Trophy Points: 160
  Kwa sababu hawa Nyoka weusi walitukandamiza kwenye mechi ya kimashindano na kutuharibia safari (kama ilikuwepo) yetu ya kwenda Bondeni 2010 (na Angola), basi hatuwezi kusema tumelipiza kwa kuwafunga kwenye mechi ya kirafiki.
  Tusubiri tukutane nao kwenye mechi ya kimashindano.
  BTW: Viva Stars kwa ushindi, yaweza kutusaidia kupanda kidogo (labda hadi kwenye top 100) kwenye chati ya FIFA.
   
 3. Next Level

  Next Level JF-Expert Member

  #3
  Nov 20, 2008
  Joined: Nov 17, 2008
  Messages: 3,159
  Likes Received: 17
  Trophy Points: 135
  Bora umeliona hilo......jana hatatungeshida bao kumi na moja, ilikuwa si venue ya kulipiza kisasi, ilikuwa ni mechi ya kirafiki kwaajili ya kujipima nguvu tu!

  Stars wakitaka kulipiza kisasi wasubiri mashindano ya kufuzu tena world cup...hope itakuwa Brazil 2014, ndipo tulipize kisasi au hata mshindano ya kufuzu Kombe la Africa ...sio mchezo wa kirafiki!

  Tufungue macho na ubongo jamani ...eeeh!
   
 4. africa6666

  africa6666 JF-Expert Member

  #4
  Nov 20, 2008
  Joined: Aug 18, 2008
  Messages: 281
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 35
  Kwa records za FIFA, wanahesabu mchezo wowote wa kimataifa kuwa ni sawa friend match or otherwise, ndio maana ktk mechi kama za jana ambazo zimechezwa kote barani africa, FIFA wanazitumia kutathmini ubora wa timu husika.
  Please don't comment some thing you are not sure of.
  Ile ni mechi muhimu sana mbali na kulipiza kisasi pia inatusaidia fifa kwa records
   
 5. Next Level

  Next Level JF-Expert Member

  #5
  Nov 20, 2008
  Joined: Nov 17, 2008
  Messages: 3,159
  Likes Received: 17
  Trophy Points: 135
  Mkuu sijakuelewa vyema hapa, ubora gani unaosema hapa kwa stars ambayo perfomance yake iko very inconsistence hivyo? jana mko nafasi ya 90, leo 102 keshokutwa 104 for what? Tunacho comment hapa, ni kusherekea kuifunga Black Mambas kwenye friendly mechi halafu unasema umelipiza kisasi! Kwanza kikosi kilicho ifunga stars last year sidhani ndo hicho kilicheza jana, pili sidhani split ya timu yao ya jana sidhani inafanana na ile ilioyotufunga kwenye qualifying match!

  Therefore unavyozungumzia kulipiza kisasi mimi sikubali ukiwa unazungumzia mchezo wa jana, cause malengo ya michezo hiyo miwili ilikuwa tofauti kabisa!
   
Loading...