Stars wang'ang'aniwa Uwanja wa Ndege Bangui | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Stars wang'ang'aniwa Uwanja wa Ndege Bangui

Discussion in 'Sports' started by kilimasera, Jun 9, 2011.

 1. kilimasera

  kilimasera JF-Expert Member

  #1
  Jun 9, 2011
  Joined: Dec 2, 2009
  Messages: 3,073
  Likes Received: 17
  Trophy Points: 135
  WACHEZAJI na viongozi wa timu ya taifa ya Tanzania, Taifa Stars waliwasili juzi usiku wakitokea Bangui walipokuwa wakicheza mechi ya kuwania kufuzu Fainali za afrika zitakazoanyika mwakani.

  Katika mchezo huo, Stars ilijiweka pabaya baada ya kukubali kipigo cha mabao 2-1, mchez uliofanyika Jumapili kwenye Uwanja wa Barthelemy Boganda.

  Hata hivyo, baada ya kuwasili kwenye Uwanja wa Ndege wa Julius Nyerere baadhi ya wachezaji na kocha Jan Poulsen pamoja na baadhi ya wachezaji walilalamikia kuwa mechi yao haikuchezeshwa kwa haki na mwamuzi ndiyo maana walipoteza.

  Hata hivyo, kabla ya kuondoka kwenye Uwanja wa Ndege wa Bangui Mpoko, wachezaji wa timu hiyo walizuiwa kwa zaidi ya saa moja wakitakiwa kulipa kodi ya uwanjani hapo ambayo ni dola 20 (sh30,700)

  Kitendo hicho kiliwashangaza baadhi ya viongozi wa Stars waliokuwa na timu kwa sababu walikuwa wakidhani kodi hiyo ilishalipwa wakati walipokata tiketi za ndege jijini Dar es Salaam.

  Askari wa Idara ya Uhamiaji na maofisa kutoka Wizara ya Fedha kwenye uwanja huo wa Bangui Mpoko walikuwa wakitaka kila mtu aliyekuwa kwenye msafara huo kulipa dola hizo ndipo waruhusiwe kuendelea na safari.
  .
  Hali hiyo ilisababisha viongozi wa Stars kutoelewana na askari hao wa uhamiaji na maofisa wa Wizara ya Fedha kwa kile kilichoelezwa kutokuwa na taarifa juu ya suala la kodi ya uwanja wa ndege na wakala wao Shirika la Ndege la Kenya na wenyeji wao, Shirikisho la Soka nchini Jamhuri ya Afrika ya Kati kwamba wakati wa kutoka nchini humo watatakiwa kulipa kodi.

  Baada ya mvutano huo, viongozi wa Stars walimtafuta Meneja wa Shirika la Ndege la Kenya uwanjani hapo ambaye alikuja na kuwaambia utaratibu huo wa kulipa kodi ni wa kawaida na wanatakiwa kulipa na wao hawahusiki na hilo.

  Pia viongozi hao wa Stars waliwapigia simu wenyeji wao Shirikisho la Soka la Jamhuri ya Afrika ya Kati, ambao walidai watafika kwenye uwanja wa ndege katika muda wa dakika 10, lakini hawakutokea.

  Baada ya kuona hivyo, mmoja wa viongozi wa msafara wa Stars, Saad Kawemba pamoja na Meneja Mkuu wa Idara ya Uhusiano na Mawasiliano wa Kampuni ya Bia ya Serengeti, Teddy Mapunda waliamua kwenda benki na kutoa dola 700 (sh1,078,000) na kulipa ndipo taratibu nyingine za msafara wa Stars kukaguliwa zikaendelea.

  Awali kabla kuanza safari ya kurudi Dar es Salaam, pia uongozi wa Hotel de Centre ambayo walikuwa wamefikia Taifa Stars waliwashangaza wachezaji na viongozi walipowaeleza kuwa wanatakiwa kulipia kifungua kinywa kabla ya kuondoka hotelini hapo.

  Kuona hivyo, Mbunge wa Kondoa, Juma Nkamia ambaye alikuwa akiiwakilisha serikali ya Tanzania katika msafara wa Stars, alipinga kitendo hicho na kuwaambia wawapigie simu Shrikisho la Soka la Jamhuri ya Afrika ya Kati ambao ni wenyeji wao kuwaeleza hivyo kwa sababu anachofahamu katika hoteli kubwa kama ile lazima kifungua kinywa kitolewe kwa watu waliolala kwenye hoteli hiyo.

  Baada ya kupigiwa simu viongozi wa Shirikisho la Soka Jamhuri ya Afrika ya Kti walikubali kulipia gharama za kifungua kinywa hicho.

  Kambi ya Taifa Stars ilivunjwa jana rasmi kwa ajili ya wachezaji kurudi kwenye klabu zao, huku wachezaji wa kulipwa wa Stars, Athuman Machupa, Nizar Khalfan, Mbwana Samatta na Idrisa Rashid wakisema watakuwa nchini kwa mapumziko ya siku kadhaa kabla ya kurudi kwenye klabu zao za nje ya nchi.
   
 2. Crashwise

  Crashwise JF-Expert Member

  #2
  Jun 9, 2011
  Joined: Oct 23, 2007
  Messages: 22,172
  Likes Received: 862
  Trophy Points: 280
  pole zao..
   
 3. Lambardi

  Lambardi JF-Expert Member

  #3
  Jun 9, 2011
  Joined: Feb 7, 2008
  Messages: 10,313
  Likes Received: 5,605
  Trophy Points: 280
  Hicho ki nchi kina rushwa na masikini zaidi yetu kwa hiyo kama ka nchi corrupt tegemea hata hewa unayovuta utailipia wakiamua maana hakuna haki wala atakaekuelewa!!ukibanwa unalipa maana hata ubalozi hakuna nani atakufundisha jinsi kugomea kulipa au wakilishi dola yetu ungekuwepo ungepiga kelele.......
   
 4. Papa Mopao

  Papa Mopao JF-Expert Member

  #4
  Jun 9, 2011
  Joined: Oct 7, 2009
  Messages: 3,353
  Likes Received: 387
  Trophy Points: 180
  inavyoonekana hiyo nchi imeharibika kwa rushwa! kumbe tz tuna afadhali!
   
Loading...