Star TV wanafundisha jinsi ya kunawa mikono bila maji

Shoctopus

JF-Expert Member
Dec 29, 2015
3,434
1,985
Assalamualaikum WanaJf!

Baada ya kupata reaction tofauti toka kwa WanaJf kuhusu taarifa yangu juu ya upotofu wa taarifa ya BBC kwamba umbali kati ya dunia na jua ni kilometers 150; nimeona niwaletee kiroja kingine cha vyombo vya habari kinachoendelea hapa hapa bongoland.

Kama ilivyo kawaida siku hizi za COVID-19 leo Tena (tarehe 24/01/2022) saa tatu hivi, usiku kabla na baada ya matangazo ya BBC ktk Star Tv wameonyesha animation video kuhusu jinsi ya kunawa mikono kama njia mojawapo muhimu ya kujikinga na COVID-19.

Cha kushangaza ni kwamba wanaonyesha watoto wakinawa. Lakini mikono inaonyeshwa ikinawa chini ya bomba lisilo na maji!

Swali langu kwa waandaaji wa video hii walikuwa na haraka gani hadi kuonyesha kitu kisicho na uhalisia?

Kuwepo kwa MAJI TIRIRIKA ni jambo muhimu sana katika zoezi zima la KUNAWA MIKONO; imekuwaje STAR TV watunge video yenye maneno 'matamu' ikionyesha watoto wakinawa mikono kwenye bomba bila ya maji TIRIRIKA?

Kuna mtu atasema kuna umakini katika uandaaji wa audio video hii? Na kwakuwa imekuwa ikirudiwa rudiwa wiki au miezi kadhaa sasa, wahusika huko Star Tv hawajaona kasoro hii?

Najua kuna watu humu watasema kwani ujumbe haujafika? Lakini baadhi yetu tunaojali umuhimu wa TV graphics lazima tujiulize kama wahusika walipata real value for the money spent in this case kupitia tangazo hili?

Pamoja na ujumbe kufika ni muhimu ujumbe uwe kamili, usio na dosari za kiufundi kama hapa juu!

Nipo hapa, nasubiri waje waleee!
 
Siku zinavyozidi kusonga mbele, basi na usirias kwa Watanzania unazidi kushuka.

Usipokuwa na msimamo, unaweza kuwa sirias sana Tanzania, lakini baada ya miaka kadhaa na wewe unawaiga wengine kukosa usirias!
 
Kuwepo kwa MAJI TIRIRIKA ni jambo muhimu sana katika zoezi zima la KUNAWA MIKONO; imekuwaje STAR TV watunge video yenye maneno 'matamu' ikionyesha watoto wakinawa mikono kwenye bomba bila ya maji TIRIRIKA?
Labda ni kijembe kwa mtu
 
Moja kati ya tv niliyoipenda mno, hususani upande wa sports, local news and international news wako vizuri mno.....kwa upande wa redio, RFA naikubali kuliko redio yoyote ile hapa nchini and east Africa kwa ujumla.
HONGERA MKUU, MIMI ILIKUWA ENZI HIZOO LABDA
 
ZIMAMOTO (fire) nahisi hata hawa wanafanyiwagwa majaribio/mazoezi bila ya kuwa na maji ndio maana wanajikuta wanaenda kwenye tukio bila ya maji na wakienda na maji wanashindwa kuyatumia kwa kuwa hawajajua jinsi gani kuzima moto kutumia maji ya presha.. wanawaharibu KISAIKOLOJIA
 
Back
Top Bottom