Star TV, UKAWA wapo Millenium Tower Live

wenzio wanatupa kadi za ccm we unaokota toka hapa!!!!!!!!!!!!!!!!!
 
Dr ana mtaji wa kura 2010 ikiwemo ya kwangu ....
Mkiweka tamaa pembeni dr slaa anafaa sana tu
That is very true.

Hata hivyo tayari kule Zanzibar Chadema weshakubali kumwachia Maalim Seif agombee Urais na wao Chadema watampa full support na wao Chadema hawatasimamisha mgombea wa Urais kule.

Inaelekea wewe mleta post unataka tu kuleta 'chokochoko' tu za kutaka kuwagombanisha Ukawa.

Hivi kwa mawazo yako unaona imekaa fair kwa CUF iwe na wagombea 2 wa Urais kwa Zanzibar na Tanzania wakati Chama kikuu cha upinzani nchini ambacho ni Chadema kisiwe na mgombea yeyote?!
 

Chadema ndio wamiliki wa UKAWA na wana lazimisha Slaa aongoze jahazi wakati wanajua Slaa ni kiongozi wa dini na watanzania wengi hawato mpigia kura!
 
cuf wameamua kujimaliza huku bara

A cha fikra potofu za kuchanganya wapenzi wa ukawa. Ni sahihi kabisa kumsimamisha dk , na sababu zipo nyingi. Tatizo hufikirii kwa mapana na maslahi ya watanzania
 
Chadema ndio wamiliki wa UKAWA na wana lazimisha Slaa aongoze jahazi wakati wanajua Slaa ni kiongozi wa dini na watanzania wengi hawato mpigia kura!
Wewe Ruta umewaona Chadema tu kuwa ndiye wanaomng'ang'ania Dr Slaa kuwa mgombea wa Ukawa, unajifanya umesahau mgombea wenu wa CCM mzee wa mamvi ambaye 'timu Lowassa' waliapa kuwa iwe isivyo lazima mgombea wao ndiye atangazwe kuwa mgombea wa Urais, hadi wajumbe watatu wa CC wakiongozwa na Nchimbi kuutangazia Umma wa watanzania kuwa hawayatambui matokeo ya CC yao yaliyomuengua mzee wa mamvi?

Hadi ikasababisha mzee huyo wa mamvi 'awaoganaizi' wafuasi wake hadi watake kufanya 'uasi' ndani ya NEC yao.

Sasa hapo Rutta nikuulize ni nani hasa king'ang'anizi zaidi kati ya Dr Slaa na mtu wako Mzee wa mamvi?
 
Ushauri kwa viongozi wakubwa Wa vyama vyote Ukawa. Maanisheni muungano kwa maana:- Tunataka jina jipya LA chama litakalo unganisha watu wote Wa vyama mbalimbali ktk umoja wenu. Pili andikeni katiba ya chama hicho kipya itakayokuwa imepitishwa na wajumbe wote ktk chama Hii itaondoa utofauti wenu unaoonekana Leo. Tatu misingi ya udini ni hatari ktk umoja wenu wekeni Taratibu vizuri namna ya kuheshimiana na muwahakikishie wananchi juu ya hili kuwa si kigezo kutokumpa MTU madaraka ya kuongoza kwa utofauti Wa DINI.
 
Mkuu unajisumbua bure Chadema hawawezi kukubali bora kila mtu aingie kivyake kwenye uchaguzi wapate kura mbili mbili.

Ni kweli kwa urais wa JMT ni ngumu CDM Kukiachia chama kingine,ni ngumu mno
 
Hivi unadhani Wazanzibar wanafikiri kama wewe?unadhani watampa kura Dr Slaa?Nampenda sana Dr Slaa na nadhani ana sifa za kuwa rais,ila sina uhakika kama atashinda.Tundu Lissu anaweza kuwa chaguo salama.

Aliyewaloga bado yupo hai mtafuteni.
 
Kwa mtindo huo huo CUF waiachie CHADEMA nafasi ya kugombea urais wa Zanzibar na kwa kuwa CUF wana nguvu huko waipigie CHADEMA kampeni kwa nguvu.
 
Ccm washatumia hadi waganga wa jadi ukawa isambaratike ila wolaaaa
 
haya mauno ya ccm sitakubali ndugu yangu aende Dodoma
 
Tungepata serikali ya mseto presider magufuli,pm Dr slaa,elimu mbatia kwingine wajae ccm
 
Padri slaa arudishe kwanza mke wa mtu,awarudie watoto wake aliowatelekeza na apate sakramenti ya kitubio kwa dhambi ya usaliti ya upadri ndo agombee uraisi
 
Magufuli ni mkristo dhabiti kuliko huyo dk. Slaa, ka taarifa yako kama ulikuwa hujui


kwa hiyo magufuli aliwahi kuwa Padre !... ? ukristo wake sio shida kwetu ! historia yake hakuwahi kuwa kiongozi wa kanisa, hajasoma canon laws ... usimfananishe Dr. JM na Dr. feki Slaa! ...
 

Similar Discussions

Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…