Star TV should declare their interest

Star TV should declare their interest

emalau

JF-Expert Member
Joined
Apr 25, 2009
Posts
2,775
Reaction score
3,109
Nimekuwa nikiifuatilia Star TV kwa muda mrefu hata kabla mchakato wa uchaguzi haujaanza. Niliifurahia kwa sababu walikuwa wakiita wachambuzi ambao wanachambua kwa kutumia independent mind.

Toka mchakato wa uchaguzi uanze hii TV imeanza kupoteza credibility, wanaita wachambuzi huku wanawapangia nini cha kuongea, unawaona watu wazima wanaongea mambo ambayo hayapo kwenye nafsi zao. Nimejaribu kufanya utafiti kupata habari za ndani kulikoni, mtu mmoja aliyepata za ndani ni kwamba Star TV imelipwa na CCM kufanya upendeleo wa makusudi katika habari na uchambuzi wake. Mtu huyu ameenda mbali zaidi akasema wamehakikishiwa na CCM kwamba hata wakipigwa faini na TCRA kama walivyofanyiwa Magic FM na TBC CCM wako tayari kulipa faini!

Ni jambo lililo wazi kwamba Star TV inamilikiwa na kada wa CCM Diallo, hilo halina ubaya na ana uhuru wa kikatiba kufanya hivyo. Kinachosikitisha ni kujifanya wako balanced wakati sisi watazamaji tunag'amua. Katika nchi zilizoendelea baadhi ya vyombo vya habari huwa vina declare interest katika uchaguzi kwamba wanaunga mkono chama au mgombea fulani. Kwa hiyo nawashauri star TV watutangazie wazi kwamba katika mchakato huu wa uchaguzi wanaunga mkono CCM bila kificho, tutawaheshimu kwa hilo na hiyo ni sehemu ya demokrasia ya kweli.

Nawasilisha
 
Mbona hauongelei Kahama fm na Radio 5 zinamilikiwa na akina nani.
 
​Wote tunaelewa hawana cha kutwambia tunajua kabisa::::STAR TV=DIALO=CCM!!!!!!!!!!
 
unatafuta mini huko wenzako hata Star TV no kitu gani hicho
 
Kuna Mtanazaji wake yupo Dar,Jina Kmt Huyu Kwenye Kufacilitate Mada uwa Anatamani yeye Indie awe kama Mchambuzi.Purely based guy working for CCM.
 
CCM haijalipa chochote kwa Start TV kufanya upendeleo. Kinachofanyika ni kwamba, kwa kuwa mmiliki wa Start TV ni kada wa CCM, Mhe Diallo, tena ni mwenyekiti wa CCM mkoa wa Mwanza. Je, hapo kama una akili timamu utaelewa ni kwanini CCM imebebwa sana na hii televisheni wakati huo huo UKAWA wakiwekwa kapuni.
 
Na pia chanel za tz. Local zipo zaidi ya 10 ivyo sio razima uangalie star tv. Tu angalia chaneli zingine. Au mmelazimishwaa. Na inaonekana nyi ndo mnaangaliaga tv kwa jilani ivyo unakosa mamlaka ya limot.
 
Unajua nani mmiliki wa star tv?? Ukishajua nani mmiliki hutalalamika wanalolifanya.

Sijalalamika, kama umeona hapo kwenye uzi nimetaja kwamba ni kada wa CCM, ninachotaka atanabaishe wazi upande wake ili tujue na hatutamchukia kwa hilo.
 
Kampeni gani wasizomuonesha John Pombe Magufuli wao wanamuonesha Lowassa wajilekebishe inatoa taswira mbaya pia ni rahis kuleta mifarakano katika jamii.
 
Na pia chanel za tz. Local zipo zaidi ya 10 ivyo sio razima uangalie star tv. Tu angalia chaneli zingine. Au mmelazimishwaa. Na inaonekana nyi ndo mnaangaliaga tv kwa jilani ivyo unakosa mamlaka ya limot.

Kwa hiyo kwa kuwa ziko nyingi moja ikifanya makosa ya kitaaluma tuiache? Argue kama mtu mzima
 
Nimeliona hilo, lakin ndo wanampaisha kisiasa
 
Ni vema unayelalamika ukawasiliana na wahusika wa chombo husika ili kupata ufafanuzi kwa sababu vyombo hivi vinafanya kazi kibiashara zaidi, ndiyo maana hata magazeti ukiangalia mlengo wa habari kila chombo kinaegemea chama au mgombea fulani, sababu ya chombo kuegemea upande mmoja na siyo upande mwingine kila mmoja anazijua.

Ndiyo maana hivi sasa magazeti kama MAWIO na RAIA MWEMA huhitaji kuuliza habari zake zina mbeba mgombea gani. Na kila chombo kuna kundi la watu linafurahia habari zake. Kitu cha kuumizi vichwa ni chombo kipi kinawafuatiliaji wengi ambao kila mara watakuwa wana jazwa taarifa za aina moja, maana kila mtu anaupenzi wa chombo fulani cha habari. Mgombea anayanadiwa na vyombo ambavyo mtandao wake ni mdogo ataumia zaidi ya yule anayenadiwa na chombo chenye mtandao mkubwa zaidi, kwa sababu mpokeaji taarifa atakuwa analishwa taarifa za mgombea ambaye chombo husika kinamnadi.
 
mimi hata kingamuzi chao cha contnental nimekiuza. Hawafai kabisa hawa. Na station yao ya star tv nimeifuta kwenye kingamuzi changu.
 
mimi hata kingamuzi chao cha contnental nimekiuza. Hawafai kabisa hawa. Na station yao ya star tv nimeifuta kwenye kingamuzi changu.

Kuanzia leo siangalii tena mkuu hii station isije leta mambo ya rwanda
 
Back
Top Bottom