STAR TV mjipange

STAR TV mjipange

washa

JF-Expert Member
Joined
Oct 8, 2007
Posts
626
Reaction score
370
Mimi nimekuwa shabiki wa muda mrefu wa vipindi vya StarTv, hasa vipindi vya jumamosi na Jumapili asubuhi vikiongozwa na YAHAYA na DOTTO Bulendu. Wamekuwa wakiendesha vipindi vyao kwa kiwango cha kuridhisha.
Kama kawaida leo nimeamka mapema ili niangalie mjadala lakini huu wa leo unaboa ilembaya. Mwendeshakipindi amemwalika kada wa ccm ambaye amepewa kipindi ili kukinadi chama badala ya kuweka mjadala mpana. Kwanini leo hakuna mshiriki mwenye mtazamo tofauti ili kukianya kipindi kiwe na upeo.
StarTv jipangeni
 
Kwa hoja yako ni presenter wa leo au kukosekana kwa Yahaya Mohammed studioni????

Hebu kuwa specific????
 
... Kwanini leo hakuna mshiriki mwenye mtazamo tofauti ili kukianya kipindi kiwe na upeo.
Labda mtangazaji mwenyewe anasimama kama mtu mwenye mtazamo tofauti na ule wa huyo kada!
 
Kwa hoja yako ni presenter wa leo au kukosekana kwa Yahaya Mohammed studioni????

Hebu kuwa specific????

Tatizo limegawanyika katika sehemu mbili, lakwanza ni mwendeshaji wa kipindi cha leo, lakini pia tumeona tatizo linalofanana na hili katika kipindi kilichoendeshwa majuma machache yaliyopita ambapo gwiji Dotto pale alipo waalipo walika wazee makada wa ccm na watazamaji wengi walilalamika na DOTTO akakubali udhaifu na kuahidi kufanyia kazi changamoto hiyo.
Naomba ufuatilie kipindi ambacho kiko hewani, ni kama tunasikiliza hotuba............
 
kwa kwei imeboa leo!.....Mabunga ni presenter mahiri sana, ila leo kabugi kumleta huyu kada (Kaaya), tena peke yake bila kuwa na 'challenger'...jamaa full kukinadi chama na swanglish yake ya kisisiem utafikiri hajakaa Tz.... Hakika imeboa na nshachange channell kitaaaambo!
 
Huyo kada namfahamu wakati nipo mwanza, anaitwa Kaaya na alikuwa ni bwana mifugo kule Magu vijijini. Hizi siasa amekuja kuzirukia tu majuzi hakuna lolote analolijua. Huyu jamaa aliwahi kusema kuwa haoni sababu ya kujenga nyumba kwani wanawake hawawezi kujua kama ni tajiri kwa kuwa hatembei nayo, ila akiwa na gari inakupa Starters mjini. Wakati huo alikuwa amenunua 504 used.
 
mi ndo leo nmemskiliza.... Jamaa ni hopeless.....na kidhungu chake cha kuombea maji bas ndo anazid kunichefua......in short li limbukeni tu
 
Nami nimekuwa mpenzi wa StarTV kwa muda mrefu kutokana na vipindi vyake kuwa professional. Lakini hivi karibuni wameanza upuuza wa kukifanya kituo hiki kuwa mali ya CCM kwa kuonyesha vipindi vya kushabikia CCM. Nadhani hii ilitokana na Boss wa Sahara Media kuukwaa uenyekiti wa CCM (M) Mwanza.

Kweli stat TV jipangeni upya kabla hatuwasusia kama tunavyosusia TBC.
 
Mh! Kama ni hivyo kumbe sijapoteza kitu leo manake nami pia ni mpenzi mzuri wa Star Tv Tuongee asubuhi Jumamosi na Jumapili. Leo niliamua kwende kumshukuru Mungu Kanisani asubuhi sana kumbe nilikuwa sahihi tu kwenda mda huo kwani sijapoteza kitu leo Star Tv.
 
Mimi nimekuwa shabiki wa muda mrefu wa vipindi vya StarTv, hasa vipindi vya jumamosi na Jumapili asubuhi vikiongozwa na YAHAYA na DOTTO Bulendu. Wamekuwa wakiendesha vipindi vyao kwa kiwango cha kuridhisha.
Kama kawaida leo nimeamka mapema ili niangalie mjadala lakini huu wa leo unaboa ilembaya. Mwendeshakipindi amemwalika kada wa ccm ambaye amepewa kipindi ili kukinadi chama badala ya kuweka mjadala mpana. Kwanini leo hakuna mshiriki mwenye mtazamo tofauti ili kukianya kipindi kiwe na upeo.
StarTv jipangeni

...mkuu labda kuna mambo ambayo haujayaelewa vizuri kuhusu Startv,naomba nikukumbushe kwamba mmiliki wa kituo hiki bwana Diallo ni kada mtiifu wa CCM na katika chaguzi za chama ngazi ya mkoa zilizofanyika hivi karibuni,Diallo alichaguliwa kuwa mwenyekiti wa CCM wa mkoa wa Mwanza...nadhani sasa utapata picha ni kwa nini Startv inaanza kupoteza ile sifa yake ya kuendelea kuwa chanzo uhuru cha habari...changanya na ZA-MBAYUWAYU utapata jibu...
 
Mimi nimekuwa shabiki wa muda mrefu wa vipindi vya StarTv, hasa vipindi vya jumamosi na Jumapili asubuhi vikiongozwa na YAHAYA na DOTTO Bulendu. Wamekuwa wakiendesha vipindi vyao kwa kiwango cha kuridhisha.
Kama kawaida leo nimeamka mapema ili niangalie mjadala lakini huu wa leo unaboa ilembaya. Mwendeshakipindi amemwalika kada wa ccm ambaye amepewa kipindi ili kukinadi chama badala ya kuweka mjadala mpana. Kwanini leo hakuna mshiriki mwenye mtazamo tofauti ili kukianya kipindi kiwe na upeo.
StarTv jipangeni

...............Mimi huwa nawaangalia kwa kile kipindi cha kukosoa vyombo vingine vya habari hasa heading za magazeti mbalimbali...... lakini wao wenyewe wanatatizo la matangazo ya kipindi cha Watanzania tuzungumze magazeti.... kila asubuhi....... kipindi hakina uhakika kinaanza saa ngapi, na matangazo yao yanakatikakatika wao yao hawayasemi .... si unajua nyani haoni kundule.......

hehehehehe kipindi chao cha magazeti leo kimegoma kupanda hewani!..... Na wameshndwa kujiunga na waandishi wao Dodoma!...kipnd kimepoteza mvuto sanaJiiiinga sn hawa jamaaa.
 
mi ndo leo nmemskiliza.... Jamaa ni hopeless.....na kidhungu chake cha kuombea maji bas ndo anazid kunichefua......in short li limbukeni tu

Kipindi cha leo kilikuwa kibaya sana, kwanza kulikuwa na kelele utadhani kuna watu walikuwa wanapanga fanicha, huyo Kaaya ndo kachemka kabisa, watazamaji wachache wame mchallenghe kwenye simu nikaona kama anataka kulia vile!

jamaa mmoja kapiga simu akamwambia anatakiwa kueleza serikali ya chama chao itatuondoleaje matatizo tuliyonayo kama uhaba wa mafuta na kadhalika, na sio kutuambia habari za mdororo wa uchumi duniani, hakuweza kulijibu hilo swali, kwa kifupi hakuna swali alilojibu kwa ufasaha, ni kilaza wa kutosha tu.
 
Asubuhi Mkuu ulitakiwa kwenda Kanisani.Pamoja na makosa yao nasita kusema na wewe una makosa.Am jokg bwana
 
Back
Top Bottom