Star tv mijadala. | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Star tv mijadala.

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Mpevu, Dec 20, 2010.

 1. Mpevu

  Mpevu JF-Expert Member

  #1
  Dec 20, 2010
  Joined: Nov 23, 2010
  Messages: 1,816
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 0
  Waungwana,
  Mimi binafsi nimekuwa nikifatilia mijadala mingi na yenye tija kwa taifa hili kupitia luninga ya Star, ambapo baadhi ya mijadala hiyo nimepata kuchangia.
  Ninadhani sasa,, ya kwamba iwafikie waendeshaji wa kipindi hicho cha TUONGEE ASUBUHI kwamba watujulishapo juu ya mjadala/midahalo wakusudiayo kuirusha hewani siku hiyo ya j2 basi itapendeza zaidi kama wawe wanatupa taarifa humu jamvini walau 5-days kabla ya kipindi ili kama wanahitaji michango TULIVU na yenye TIJA toka humu iweze kuwasaidia na kuisaidia jamii kiujumla.
  Tutoapo michango kwa 1/2/3-days before wengine huwa hatuna utulivu wa kuchambua/kunyambua vema na kujenga hoja nzuri, na badala yake huwa tunatoa michango ya papo hapo while huenda ni topic yenye ujenzi kwa taifa na jamii kiujumla.
  Naomba kuwasilisha na iwafikie wadau hao nguli wa tasnia ya habari nchini.
   
 2. Mtembea_peku

  Mtembea_peku Senior Member

  #2
  Dec 20, 2010
  Joined: Dec 15, 2010
  Messages: 135
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  wazo zuri sana ,litajenga na kuboresha c kipindi tu bali mstakabal mzima wa taifa.
   
 3. Henge

  Henge JF-Expert Member

  #3
  Dec 20, 2010
  Joined: May 14, 2009
  Messages: 6,765
  Likes Received: 78
  Trophy Points: 145
  Ni kweli mda wanaotoa kwa ajili ya kujadili mada hizo huwa ni kidogo hapa jf, nadhani mkuu ameipata hii!
   
 4. AMARIDONG

  AMARIDONG JF-Expert Member

  #4
  Dec 20, 2010
  Joined: Jun 24, 2010
  Messages: 2,506
  Likes Received: 48
  Trophy Points: 0
  SAFI IKO POA SANA HATA MiMI NAIFUATILIAGA
   
 5. c

  chelenje JF-Expert Member

  #5
  Dec 20, 2010
  Joined: Oct 18, 2010
  Messages: 554
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Mkuu habari za Tosamaganga au Tanangozi au Ipogolo??????? hiyo red mkuu...
   
 6. Yahya Mohamed

  Yahya Mohamed Verified User

  #6
  Dec 21, 2010
  Joined: Oct 28, 2010
  Messages: 270
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 35
  Nitoe shukrani zangu za kipekee kabisa kwa niaba ya Msimamizi wa Vipindi Star TV kwa WanaJF wote ambao wamekuwa nasi bega kwa bega kushiriki nasi kwa kuchukua muda wao kutafiti masuala muhimu kabisa yenye Tija kwa Taifa kwa kutoa mawazo ambayo kwa kweli ni haki ya msingi ya kila Mtanzania ili kuisaidia serikali yetu na kuikumbusha wajibu wake katika kumletea Mtanzania Ustawi mzuri.
  Tumekuwa tukitoa mada wikiendi kwa uzoefu imeonyesha ni muda ambao wanaJF wengi wanakuwa busy katika mtandao. Lakini wazo la kutoa mada mapema ni jema na tumelipokea na kwa kuanzaia naomba kuwasilisha mapema mada ya Ijumaa wikii na Jumapili:

  '' Kwa nini watanzania wananyimwa fursa ya kuwa na Nishati ya uhakika ya Umeme'' IJUMAA WIKI HII - 24.12.2010

  '' Kuna Ulazima gani wa matumizi ya Nguvu kupita kiasi kwa Jeshi la Polisi katika kukabiliana na Watuhumiwa/Wahalifu'' Jumapili BOXING DAY

  Merry x-mas Wadau

  Naomba kuwasilisha

  Yahya M
   
 7. Mpevu

  Mpevu JF-Expert Member

  #7
  Dec 21, 2010
  Joined: Nov 23, 2010
  Messages: 1,816
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 0
  Ahsante kwa kutuzingatia,
   
 8. Mpevu

  Mpevu JF-Expert Member

  #8
  Dec 23, 2010
  Joined: Nov 23, 2010
  Messages: 1,816
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 0
  '' Kwa nini watanzania wananyimwa fursa ya kuwa na Nishati ya uhakika ya Umeme'' IJUMAA WIKI HII - 24.12.2010

  Muongozaji,
  Taifa letu hili ni changa na lenye changamoto lukuki katika ukiaji wake, tunazo changamoto hasi na chanya.
  • Taifa halina misingi/mipango endelevu juu ya janga hili la umeme.
  • Taifa haliwezi kusonga mbele kimaendeleo pasipokuwa na nishati kamilifu na yenye kuvutia hata wawekezaji.
  • Kwa nyakati tofauti taifa limeshuhudia tatizo la nishati bila ufumbuzi wa kudumu, tunarithisha tatizo hili kwa vizazi pasipo kulitafutia ufumbuzi yakinifu.
  • Nishati ya umeme inadidimiza wananchi kwa kushindwa kuendeleza hali zao za ujasiriamali na kukuza uchumi wa taifa letu.
  • Maendeleo yahitaji nishati, hapa namaanisha maendeleo ya rasilimali watu-KIELIMU, maendeleo ya nchi-KIVIWANDA etc,,vyote vyategemea nishati hii adhimu ya umeme. kinyume chake kumekuwa na mipango mibovu na isiyo na dira ya janga la umeme kuwa ni historia walau tu kwa kizazi hiki.
  • Katika kipindi hiki cha mitikisiko ya uchumi duniani, tungetegemea kutoweza kuona janga la umeme kuikumba nchi yetu...bali matokeo yake tumeruhusu kuuyumbisha uchumi wa nchi tena kwa tatizo la nishati.
  nadhani ifike wakati sisi wananchi wa kawaida tuangaliwe vema na wakuu wetu wa nchi,
   
 9. Yahya Mohamed

  Yahya Mohamed Verified User

  #9
  Dec 23, 2010
  Joined: Oct 28, 2010
  Messages: 270
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 35
  Kwa niaba ya mwendeshaji wa Mjadala wa Kesho,
  Mchango wako umefika Mpevu
  Yahya M
   
 10. m

  mams JF-Expert Member

  #10
  Dec 23, 2010
  Joined: Jul 19, 2009
  Messages: 616
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 35
  Kwa hili Startv wanastahili pongezi na hususan ktk uchambuzi wa umuhimu wa katiba mpya. Kama statiopn nyingine zitaiga basi itakuwa ni ukombozi kwa Watz
   
 11. Henge

  Henge JF-Expert Member

  #11
  Dec 23, 2010
  Joined: May 14, 2009
  Messages: 6,765
  Likes Received: 78
  Trophy Points: 145
  ' Kuna Ulazima gani wa matumizi ya Nguvu kupita kiasi kwa Jeshi la Polisi katika kukabiliana na Watuhumiwa/Wahalifu'' Jumapili BOXING DAY
  Wenzetu wa jeshi la polisi hawana elimu yakutosha kuhusu haki ya mtuhumiwa, Kisheria mtuhumiwa anahaki zake, anahaki ya kusikilizwa, badala ya kutumia mabuvu na nguvu nyingi hata mahali ambapo hapana umuhimu wa kutumia, Naomba jeshi la polisi wapewe elimu na jinsi ya kukabiliana na mtuhumiwa na si kutumia mabavu. UNAJUA MKUU URITHI WA MJERUMANI NA MUARABU UNATUHARIBU SANA.
   
Loading...