Star TV LIVE: Mapitio ya Mjadala wa Bajeti

Mkuu Yahya, kile kipindi cha THE TANZANIA WE WANT cha mdahalo kiliishia wapi?
Ningetamani muwaweke jukwaani, Nape, Mnyika, Mtatiro then iwepo session ya Mbatia, Zitto na Mwigulu.
Pia iwepo ya Lusinde, Komba, Msigwa na Machari
 
Tatizo pia ni uwezo wa spika, Mama Makinda anaonekana ameshindwa kuliongoza Bunge, heshima ya bunge inashuka siku baada ya siku.

Kuna jambo moja ambalo tumefumbia macho. Spika Anne Makinda ni mjumbe wa CC ya CCM. Hiki ndicho chombo cha juu kabisa cha CCM na mwenyekiti wake ni Rais! Hivyo Spika hawezi kuongoza bunge au kuruhusu hoja inayokinzana na mipango/maagizo ya CC ya CCM. Kwa namna yoyote ile, Spika hawezi kuwa 'fair' kama ataendelea kuwa mjumbe wa CC. Na ninaamini muda si mrefu huu mkanganyiko unaeweza kuwa a good case study ya mkorogo wa utawala Tanzania.
 
Back
Top Bottom