LIVE ON Star TV: Kwanini Uwajibikaji kwa Viongozi si suala hiyari? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

LIVE ON Star TV: Kwanini Uwajibikaji kwa Viongozi si suala hiyari?

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Yahya Mohamed, Apr 29, 2012.

 1. Yahya Mohamed

  Yahya Mohamed Verified User

  #1
  Apr 29, 2012
  Joined: Oct 28, 2010
  Messages: 270
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 35
  Salaam wanajamvi,

  Natumai sote tumeamka salama kwa uwezo wake Mola: Jumapili ya leo tutazungumzia suala zima la uwajibikaji Viongozi wetu kwa nini si suala la hiari?

  wageni

  Mh. Mrema
  Bw. Kibamba
  Bw. Kasongi

  Mjadala utaongozwa hapa JF na MOD na pia katika Luninga Yahya - DAR na Range Mza


  Karibuni
   
 2. dosama

  dosama JF-Expert Member

  #2
  Apr 29, 2012
  Joined: Dec 25, 2010
  Messages: 786
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 35
  Mrema ndani, kibamba nae ndani
   
 3. Mungi

  Mungi JF Gold Member

  #3
  Apr 29, 2012
  Joined: Sep 23, 2010
  Messages: 16,986
  Likes Received: 443
  Trophy Points: 180
  Zitto yupo?
   
 4. dosama

  dosama JF-Expert Member

  #4
  Apr 29, 2012
  Joined: Dec 25, 2010
  Messages: 786
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 35
  Tatizo viongozi wetu wapo kichama zaidi kama yupo kwa maslai ya chama hata afanye nini haguswi.

  Bado hatujafikia hatua ya kutofautisha maslai ya chama na taifa na wanajisahau sana.
   
 5. dosama

  dosama JF-Expert Member

  #5
  Apr 29, 2012
  Joined: Dec 25, 2010
  Messages: 786
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 35
  Sijamwona
   
 6. Duble Chris

  Duble Chris JF-Expert Member

  #6
  Apr 29, 2012
  Joined: May 28, 2011
  Messages: 3,487
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 135
  vipi yule jamaa wa ADC na leo yupo ????
   
 7. N

  NGOWILE JF-Expert Member

  #7
  Apr 29, 2012
  Joined: Sep 8, 2011
  Messages: 454
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 0
  Wa dodoma:

  Tatizo ni kwamba watu wengi wameteuliwa kirafiki na sio kitaaluma. Viongozi wengi ni mawakala wa Chama Tawala katika ngazi wanazotumikia na wapo kwa maslahi binafsi na ya chama kulika wananchi.

  Haya yote yanatokana na mamlaka makubwa aliyonayo raisi wa nchi kikatiba. Suluhisho la yote ni kuweka kwenye katiba suala la uwajibikaji liwe kisheria na sio kibinafsi.

  Katiba iseme vigezo vya uteuzi kitaaluma na wananchi wapewe nafasi ya kuwajibisha kupitia uwakilishi wao kama baraza la madiwani na Bunge.

  Mwisho viongozi wetu wawe wazalendo kwa kufaham kwamba hii nchi sio ya vyama vya siasa bali ni ya watanzania wote. Waache unafiki kwa kukitetea chama badala ya kuwatetea watanzania.
   
 8. Jumakidogo

  Jumakidogo R I P

  #8
  Apr 29, 2012
  Joined: Jul 16, 2009
  Messages: 1,859
  Likes Received: 17
  Trophy Points: 0
  Watawala wamekuwa mfano wa wacheza maigizo. Binafsi sikuona sababu ya rais kuitisha kikao cha CC kwa ajili ya kujadili masuala ya mawaziri wabadhirifu wakati yeye ndiye aliyewateua, na rungu kashika yeye. Angewafukuza kwanza kisha hiyo CC ingekuwa baadaye. Sasa pamoja na kikao hicho, hakuna waziri yeyote aliyetumia busara ya kuonyesha mfano wa kujiuzulu. Hii ni hatari.
   
 9. Kurunzi

  Kurunzi JF-Expert Member

  #9
  Apr 29, 2012
  Joined: Jul 31, 2009
  Messages: 4,006
  Likes Received: 328
  Trophy Points: 180
  Yahya Baba kama mkuù wa Nyumba akiwa dhaifu nyumba lazima itatetereka Rais wetu amekuwa dhaifu kiasi ambacho mawaziri wameshajua udhaifu huo wanatenda kama wanavyotaka wanajua watalindwa na rais hawezi kuwawajibisha.

  Tunakumbuka Rais alipoingia madarakani alikujwa kwa mbwembwe nyingi kutembelea kila wazara yako wapi unasanii tu.
   
 10. O

  OMUSILANGA JF-Expert Member

  #10
  Apr 29, 2012
  Joined: Jan 25, 2012
  Messages: 384
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Ndiyo kaka Yahaya!

  Uwajibikaji umepungua kabisa kuanzia ngazi ya juu hadi chini kwa sababu huu wizi/ubadhirifu mapesa mengi ya serikali ambazo ni kodi za wananchi maskini ni chaini kubwa sana, ndo maana vyombo ya Dola kama PCCB vinafyata mkia.

  Suala la viongozi kuajibika halipo,kinacho onekana ni ombwe la uongozi ndo maana Rais analalamika, Waziri mkuu analalamika,wabunge wanalalamika,wananchi tunalalamika wakati rasilimali zetu zinakwapuliwa daily. Waungwana wanasema hivi Mjinga akijitambua, Mwerevu upo matatani. Hii political tsunam inayotokea sasa hivi is just the beginning, much more will come. Kama viongozi wanashindwa kuwajibika, wananchi watachukua hatu.

  Mfano jana tumeona Mbunge wa Geita nusura apate kichapo toka kwa wananchi na wapiga kura wake. Mwanafalsafa Plato alipata kusema "KAMWE BINADAMU HATAWEZA KUPATA UNAFUU WA MATATIZO YAKE MPAKA PALE WATAWALA WATAKAPO KUWA WENYE HEKIMA NA BUSARA".

  Naomba kuwasilisha.
   
 11. l

  longb Member

  #11
  Apr 29, 2012
  Joined: Apr 18, 2012
  Messages: 21
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  huyu jamaa wa ADC katiba yake hairuhusu kuwajibisha viongozi wa chama sijui anafuta nini kujadili hoja hii.
   
 12. Gwalihenzi

  Gwalihenzi JF-Expert Member

  #12
  Apr 29, 2012
  Joined: Oct 21, 2011
  Messages: 5,117
  Likes Received: 51
  Trophy Points: 145
  Serikali yoyote inayoundwa kimtandao haiwezi kuwajibika kwani viongozi wake huwa wanateuliwa kwa vigezo vya mtandao na sio uwezo wao kiutendaji. Mpaka hapo CCM itakapo gundua hilo mambo yataendelea kuwa hivyo hivyo.
   
 13. The Listener

  The Listener JF-Expert Member

  #13
  Apr 29, 2012
  Joined: Feb 5, 2012
  Messages: 977
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 35
  Mrema alijiuzuru kwa kutetea maslahi ya wananchi kwa kuona namna nchi ilivyokuwa ikitafunwa na wachache. Leo hii kuna makosa mengi yanafanywa na viongozi wetu lakini utamaduni wa uwajibikaji bado ni tatizo.

  Mabadiliko ya katiba yetu yaimarishe sehemu hii ya uwajibikaji ili tujenge utamaduni wa kuwajibika. Utaratibu wa kumuhamisha mtumishi aliyeharibu sehemu moja kwenda sehemu nyingine si sehemu ya uwajibikaji.

  Nadhani kuna haja ya kila mmoja wetu kujua majukumu yake kwani inaonekana kwamba kuna watumishi wengi hawajui majukumu yao
   
 14. Kurunzi

  Kurunzi JF-Expert Member

  #14
  Apr 29, 2012
  Joined: Jul 31, 2009
  Messages: 4,006
  Likes Received: 328
  Trophy Points: 180
  Mrema anasema nchi inatakiwa kufanyiwa overhaul kwani haitoshi kuwajubika kwa mawaziri pekee kwani matandao wa wizi ni mipana sana na ametolea mfano halmashauri wa Kishapu.

  Yeye binafsi alipoona serikali yake haiwajibiki issue ya Chavda alikaa pembeni.
   
 15. MNAMBOWA

  MNAMBOWA JF-Expert Member

  #15
  Apr 29, 2012
  Joined: Oct 17, 2011
  Messages: 1,984
  Likes Received: 57
  Trophy Points: 145
  watanzania tupo nyuma ya pazia ,, wanasiasa wanatufumba macho.
   
 16. M

  Mkulima aka peazant Member

  #16
  Apr 29, 2012
  Joined: Dec 18, 2011
  Messages: 21
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  nafikiri ni katiba mbovu inayompa mamlaka makubwa raisi ambayo kama tukimpata rais fisadi,mla rushwa,mhun automaticaly system itakuwa ya kifisadi,wala rushwa,wahun ikiwa inalindwa na rais mtukufu soln ni kuwa na katiba inayompunguzia rais mamlaka kama ya uteuzi na katiba inayorudisha mamlaka kwa uma kwa vitendo na si nadharia.Ahsanten
   
 17. M

  Mkwanda Senior Member

  #17
  Apr 29, 2012
  Joined: Apr 6, 2012
  Messages: 123
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  "Mimi ni mbunge wa CCM Siwezi kuunga mkono hoja inayoletwa na upinzani!"~ Kigangwala 2012.

  Sasa ukiwa na mbunge anayeishi wth this ideology kichwani mwake hata kesho akiwa kiongozi ataweza kuwajibika? Kaka Yahya uwajibikaji kwa viongozi unaanzia mbali sana!
   
 18. E

  EL MAGNIFICAL JF-Expert Member

  #18
  Apr 29, 2012
  Joined: Jan 11, 2011
  Messages: 939
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 35
  Tatizo kubwa la viongozi wetu wanatumia udhaifu wa katiba yetu kufanya ndio kigezo cha wao kutowajibika, lakini wakae wakijua wanachochea moto wa hasira ktk jamii ya mtanzania.

  Tabia hii ndio inayofanya watu wasiofungamana na siasa kuona kama siasa ni mchezo mchafu.

  Ifike mahala viongozi wawe na uchungu na taifa hili la sivyo itafikia kipindi wananchi tutajiona mahakama na tutawawajibisha wenyewe.
   
 19. M

  MwanzoMugumu Member

  #19
  Apr 29, 2012
  Joined: Jan 27, 2012
  Messages: 24
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Ndugu zangu uwajibikaji ni mgumu sana kwa Taifa kama la Tanzania watu (viongozi) wamejifunga kimtandao.

  Inamuwia vigumu sana waziri A kuondoka wakti anajua waziri B anafanya kitu kilekile naye hajaguswa. Pili kiongozi haoni sababu ya kuwajibika kwani hana hofu juu ya mamlaka iliyomteua. Vyeo wanapeana kishikaji kwahiyo kuna dhana ya tufe pamoja.

  Lakini niwape moyo tunaanza kwenda vizuri, tupige kelele kwanza kabla hatujachukua hatua nyinginezo.
   
 20. magosha

  magosha JF-Expert Member

  #20
  Apr 29, 2012
  Joined: Apr 25, 2012
  Messages: 641
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 35
  Viongozi wanapewa madaraka kwa kujuana ndo maana hata kuwajibika wanataka mpaka walazimishwe na unakuta wamewekwa pale kwa masilahi yao na yule alowaweka ili waibe na kutafuna mali ya umma hivyo kuwajibika ni ngumu sana.
   
Loading...