Star TV LIVE: Jicho letu ndani ya Habari

Yahya Mohamed

JF-Expert Member
Oct 28, 2010
270
317
Mjadala wa Leo utaangazia namna vyombo vya habari vilivyoandika taarifa za UCHAGUZI mdogo wa Arumeru na nafasi ya vipashio habari mbadala JF pamoja na blog nyingine Kama mjengwa, fullshangwe na issamichuzi.
Karibuni kwa maoni yenu katika mjadala huu.
 
Wa DODOMA. Vyombo vingi vilijitahidi kuripoti uhalisia kakini vile vya serikali vilikipendelea chama tawala na kuvibagua vyama vya upinzani.Baadhi ya waandishi wa habari waliripoti kwa intrest (maslahi) za vyama vilivyowapeleka Arumeru. Hi ni kusema kwamba waandishi wengi walikuwa kwa maslahi binafsi. Kwa mfano kuna blog moja baada ya Lusinde kutoa matusi ikaripoti hivi'lusinde aiangamiza CHADEMA'
 
Gazeti la Mwanahalisi limekosa mvuto limejikita zaidi kwenye mambo ya udaku.
 
Vyema.

Navipa pongezi nyingi sana vyombo vya habari vya binafsi, kama Star TV, ITV, Radio One na magazeti mengi kama Mwananchi, Tanzania Daima, Rais Mwema n.k. Kwa kweli hivi vilijitahidi sana kutangaza habari hizo bila upendeleo (ingawa baadhi vinamilikiwa na makada wa vyama vya siasa).

Lakini sikitiko langu linaenda kwa vyombo vya habari vya dola; hapa namaanisha TBC1, Habari Leo, Daily News na TBC Taifa. Hivi vilijisahau na kuwa kama vyombo vya habari vya Chama Cha Mapinduzi (CCM). Ingawa vinaendeshwa kwa kodi zetu watanzania!! Kwa kweli vyombo hivi vilinisikitisha sana; na cha ajabu, jana kuna mfanyakazi mmoja wa TBC1 amejotokeza hapa JF na kuwaita wakaazi wa Arusha, "wahuni" kisa waliwazuia waandishi wa TBC1 kufanya kazi ya kuripoti tukio la Godbless Lema kuvuliwa ubunge pale Arusha. Huyu Dotto Athumani, hajajiuliza kwa nini wakaazi hao wazuie waandishi wa chombo cha dola?! Na wala hawajazuia vyombo vingine vya habari kama, Uhuru, Radio 5 n.k.

Hapo inajionyesha kwamba ni dhahiri TBC ilifanya kazi yake ya kutangaza uchaguzi mdogo wa Arumeru Mashariki kwa upendeleo tofauti na chombo hicho cha dola kinavyoposwa kufanya.

Hongereni sana vyombo vya habari vya binafsi, endeleeni hivyo hivyo, ninyi ndiyo mmechukua jukumu la TBC.
 
Gazeti huwa halisomwi kama hadithi. Ni vema ukaanza na vichwa vya habari na ukimaliza anza na habari zinazokuvutia zaidi. Magazeti yalijitahidi sana kutuletea taarifa sahihi ila baadhi ya tv zilificha kabisa taarifa na wlikuwa wakionyesha taarifa za mkutano wa kwanza kabisa wa kampeni ambao kikmsingi ulijaza sana wananchi
 
Kwanza napenda kutoa pole kwa familia na ndugu wa aliyekuwa gwiji wa filamu Tz KANUMBA kwa kifo chake.

Vyombo vingi vilioandika habari juu ya uchaguzi wa ARUMERU na nyinginezo mara nyingi vilitawaliwa na ushabiki pamoja na utashi wao kwanza wa kisiasa; baadaye sana ndipo ilifuatiwa na uhalisia wa habari husika. Inasikitisha kuona vyombo hivyo vikiandika taarifa hizo kwa minajili ya ushabiki kwanza. Ingawa blog zilijitahidi kidogo katika kutoa taarifa hizo kiuhalisia mdogo.
Kiujumla MEDIA zinakiuka sana kanuni na taratibu za kiuandishi hapa Tz.

Mungu amlaze pema marehemu KANUMBA. AMINA
 
Kumbe waandishi uwa wanakubaliana habari fulani tuzitoe habari fulani tusizitotea kwa maslahi yao binafsi.
 
vyombo vimejitahidi kuripoti habari za Arumeru. Japo kila mwandishi ana "uzalendo" wa aina yake kwa chama anachokipenda. Muhimu tuepuke utamaduni wa kutukanana majukwaani kisha tunaanza kuulinda. Matusi hata ukiyarudia yanabaki matusi na unakuwa umetukana mara ya pili.

Mdadisi -DSM
 
Kwakweli tv station ya taifa imekua tatizo kwa kiasi kikubwa,yaani inasikitisha kuona hii tv ya taifa inaegemea upande mmoja wa chama tawala.tumeongea sana lakini wausika wameweka pamba masikioni.inauma.
 
Waandishi kemeeni tabia za wafuasi wa Chadema kuwatisha waandishi wa habari kwenye mikutano yao.
 
Naamini chachu kubwa ya habari ni wanahabari! Wengi huwa hatuwepo kwenye maeneo ya matukio! Nadhani walikuwa wanajigawa wenyewe kimakundi kufuatilia chama flani na kutoa habari za chama flani... hata ukiangalia habari zao walikuwa wanaegemea upande mmoja!

Sasa hivi nadhani wanahabari wapo kibiashara zaidi..!! Ndio hatukatai kwamba wanatumia gharama ila pia waangalie mambo yaliyo na tija kwa taifa zaidi!
 
Naamini chachu kubwa ya habari ni wanahabari! Wengi huwa hatuwepo kwenye maeneo ya matukio! Nadhani walikuwa wanajigawa wenyewe kimakundi kufuatilia chama flani na kutoa habari za chama flani... hata ukiangalia habari zao walikuwa wanaegemea upande mmoja!

Sasa hivi nadhani wanahabari wapo kibiashara zaidi..!! Ndio hatukatai kwamba wanatumia gharama ila pia waangalie mambo yaliyo na tija kwa taifa zaidi!
 
Yahya, vyombo vya habari huwa vinachelewa kutoa report kuliko mitandao ya kijamii, kama gazeti liko nyuma ya wakati naelewa lakini sielewi kwa nini radio na tv ziwe nyuma ya wakati.

nikitizama uchaguzi kama wa marekani hata wa urais unaona wale jamaa wanakua wanaupdate jumla ya votes kwa kila mgombea, hapa tv zetu zinaweka tu matokeo ya kituo kimojakimoja.

mnaweza mkawa na system ya kutoa running totals ili mi nikiangalia nijue jumla zilizohesabiwa na jumla alizopata kila mgombea, hapa sisemi mtangaze matokeo nooo ila mtuambie ni kura ngapi zimehesabiwa, vituo vilivyobaki kuhesbabiwa, vituo vilivyobaki kuhesabiwa
 
Msomaji na mfuatiliaji wa magezeti pamoja na vyombo vingine vya habari lazima atakuwa anafahamu juu ya sera ya chombo cha habari na mlengo wake katika kutoa habari hilo linafahamika ila kinachonikera mimi ni upotoshaji unaofanywa na hivyo vyombo kuna gazeti ambalo lilidai limefanya utafiti nakuandika ccm itashinda asilimia kadhaa binafsi naamini kabisa hilo gazeti halikufanya utafiti wowote na ndio maana matokeo yaliliumbua.Binafsi nilipongeze gazeti la Mwananchi tena uzuri na mwandishi wake yupo hapo studio kwa kweli mnafanya kazi nzuri na ndo gazeti pekee linaloweka taarifa zao kwenye mtandao kwa wakati na wapongeza kwa hilo wengi wetu tunasoma hizo habari kwenye mtandao.
 
Waandishi wanakula kwa kalamu zao, hivyo ni vizuri wakaangalia zinazouza, tusilaumu tuuu. Jamii Ndio ielimishwe juu ya vipaumbele then waandishi watabadilika
 
Back
Top Bottom