Star link yapigwa zengwe, makampuni ya simu hayaitaki

mirindimo

JF-Expert Member
Nov 2, 2009
821
1,343
93C99787-2B1D-4350-A526-91A77BB706BB.jpeg


Serikali inasema wao ndio hawajakamilisha document na Starlink wanasema wao kila kitu tayari wanaisubiri serikali.

Kama tumesahau niwakumbushe ni serikali ndio inamiliki mkongo wa Taifa kupitia TTCL ambayo haijawahi kuwa huduma nzuri ya mtandao kuzidi mitandao mingine japo wao ndio wanagawia mitandao mingine connection.

Tanzania tusahau hizi raha wanazopata mataifa mengine sisi tuendelee na haya yetu ya kuliwa bundle na internet mbovu
 
Kwa nini wanapigwa zengwe wakati nchi baadhi wameanza kufanya kazi. Nchi kama musumbiji, nigeria. Malawi nayo nadhani wameanza.

Wamuache aje hili kuwe na ushindani. Nchi yetu ina sheria zingine ngumu zinazo kwamisha mazingira mazuri ya biashara.

Ngoja mama aendelee kizirekebisha, japokuwa hawezi kuzimaliza zote kwa muda mfupi.Tumpe muda zaidi tu na itapendeza.
 
View attachment 2512148

Serikali inasema wao ndio hawajakamilisha document na Starlink wanasema wao kila kitu tayari wanaisubiri serikali...
Yaani hiii wizara yetu,inawaambia Starlink,hawajakamilisha document!

Kati yetu na Eron musk,nani ana mifumo Bora ya kiutendaji?hii ofa ya eron musk,ilibidi ipokelewe haraka,apewe vibari hata kama hajakamirisha haya makabrasha.

Tatizo hapa Kuna watu serikalini Wana hisa kwenye makampuni ya simu na yanayotoa huduma za internet sasa Starlink ikija,wanaogopa kukosa mapato na ushindani.krnge kabisa
 
Star link haiwez kuingia Tanzania na Nape yupo pale yaan Aache kampun za Airtel tigo zantel Vodacom anazopata chochote aende Kwa Elon ambae uhakika wa kupata hamna

Wakuu wana ina hisa kwa hizo kampuni so si rahis but kwa positive side watakuwa wamepata competitor bora na hivyo kuwa force wa improve service zao
 
Wakuu wana ina hisa kwa hizo kampuni so si rahis but kwa positive side watakuwa wamepata competitor bora na hivyo kuwa force wa improve service zao
Kuimprove service zao inahitaji investment zaidi na itapunguza faida kwa muda kitu ambacho hawapendi unless otherwise faida ikipungua watuongezee tozo ili Mambo Yao yasiyumbe.
 
Tokea Nape ameingia hiyo Wizara hatuoni meno ya TCRA, zamani TCRA walikuwa wanawaadabisha Makampuni ya simu kwa kosa la kutosajili laini
 
Watu mnaongea kirahisi rahisi tu na kutaka kuonewa huruma sijui nani awaonee huruma.

Wote mnafahamu utendaji wa idara husika za hapa tz na ndio hizohizo zimepewa dhamana ya jambo hilo la Elon musk la internet

Kuna mambo yakiwemo ya urasimu, ulaji nk mambo serious ambayo nguvu iliyo nyuma yake aidha mnaijua au la!

Aisee safari ipo tena ndefu tu kwa namna hii ya kujifanya kutia huruma na kulialia mitandaoni!
 
Back
Top Bottom