Standard Chatered Mikocheni Kulikoni

Mchaga

JF-Expert Member
Apr 11, 2008
1,378
204
Nikiwa mteja wa hii benki napenda kutoa masikitiko yangu kwa tawi lenu lilopo maeneo ya mikocheni.

Kwa kipindi cha mara nne ndani ya mwezi 1 nimekwama kutoa pesa kwani huwa nakumbana na ujumbe wenye utata mkubwa.

Mara ya mwisho mwezi huu wa January nilikwenda mida ya saa 11 asubuhi ambapo mashine ya ATM ilikuwa inaonekana haina tatizo lolote lakini nilipoweka kadi yangu nilipigwa na butwaa niliposhindwa kutoa pesa.

Ukiangalia salio lipo lakini ukitaka kutoa pesa unakwama hii imenitokea mara nne kwangu binafsi ni KERO KUBWA. Hoyce na Lucy tatueni tatizo hili maana tunatoka mbali kufuata ATM mikocheni ambapo ukikwama inakubidi kwenda posta. Halafu kwa nini hamfungi mashine Mlimani City?

NI HAYO TU...ASANTENI
 
Hoyce na Lucy ndio matechnician wao au?
Jaramba wao ni watu wa uhusiano, kwa namna moja au nyingine wanahusika.

Hawa ndi nawafahamu hivyo ni channel nzuri ya kufikisha malalamiko yango, unamfahamu technician nimfahamishe?
 
Fungua Acts NBC au CRDB wana ATM kila mahali Dar!

uwiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiii NBC hapana wana ka ATM kao makumbusho pale OIL COM kila wakati kinakuwa kinasikitika hakina hela, Jana tu siku nzima kilikuwa kinasikitika, halafu projection zao sijui zinakuwaje kila weekend most of the ATM zinakuwa hazina hela mi nimteja wa siku nyingi namshauri mwenzangu huyu wala asinuse NBC atapata pressure bure ATM mpaka uende muda wa kazi na sehemu iliyokaribu na ofisi ili ukishindwa uingie ndani loooo.
 
Jaramba wao ni watu wa uhusiano, kwa namna moja au nyingine wanahusika.

Hawa ndi nawafahamu hivyo ni channel nzuri ya kufikisha malalamiko yango, unamfahamu technician nimfahamishe?

Sasa Kama Unawafahamu, ya nini kuleta humu? Si ungewacontact direct moja kwa moja?
 
ATM za Ma-Banki yote ni WIZI MTUPU: Mimi nina accts NBC, NMB, CRDB, StanChat, Exim, na StanBIC lakini kuna siku nilikuta ATM zote za haya mabenki "ZINASIKITIKA..." na bahati mbaya ilikuwa Jumapili. Nilianzia Mbezi mpaka Mjini x 2 bila mafanikio!

I suspect kuwa
- there is an infrastructure issue (poor connectivity)
- Incompetency issues (staff entrusted to take care of ATM)
- financial control issues (bankers can correct me on that)
- technological issue (????_????)
- social/culture issues (we never plan ahead... ndiyo maisha ya Ki-Tanzania)
 
Just select medium. utapata jibu...

Thanks nimepata jibu; i was thinking medium (as you selected) would have approached this "context wise" - yaani ATM problem, ambayo ni tatizo technical na sio Hoyce and Lucy; nisamehe sana

Hata mimi kuna wakati nilikuwa napenda sana kuonekana najua kila mtu ninapo-complain nikashauriwa kuwatumia nuwajuao na si kuweka tatizo kwenye mfuko wa nylon wakati najua mlango wa solution
 
mambo ya ulimwengu wa kwanza mnataka yaje huko wakati nyinyi mnaendekeza uwizi wenu,sisi tupo ulimwengu wa kwanza kwahiyo msijishebedue hii ni kawaida kwa bongo land, kama vipi nyinyi mnaolalamika tokeni huko bongo mje huku mamtoni kwa shangazi.

Watu mpo bongo bado mnataka uduma za kimamtoni never ever,nabado si mnafuga ugonjwa(ccm) mpaka mkose umeme na maji ndo mtie hakili yaone kwanza yalivyo mnakosa uchungu na nchi yenu.
mnajua babu zetu waliko itoa leo hii inachezewa na nyinyi mnachekelea eti ATM mmeona ATM tu!!?
 
Labibah ungekuwa mzalendo kweli tungekuona ukipigana vita vya akina Zitto na Dr Slaa hapa nchini. Badala ya kuona wengine wajinga. Njoo ulete mabadiliko badala ya kujishebedua kwenye nchi za watu.
 
mambo ya ulimwengu wa kwanza mnataka yaje huko wakati nyinyi mnaendekeza uwizi wenu,sisi tupo ulimwengu wa kwanza kwahiyo msijishebedue hii ni kawaida kwa bongo land, kama vipi nyinyi mnaolalamika tokeni huko bongo mje huku mamtoni kwa shangazi.

Watu mpo bongo bado mnataka uduma za kimamtoni never ever,nabado si mnafuga ugonjwa(ccm) mpaka mkose umeme na maji ndo mtie hakili yaone kwanza yalivyo mnakosa uchungu na nchi yenu.
mnajua babu zetu waliko itoa leo hii inachezewa na nyinyi mnachekelea eti ATM mmeona ATM tu!!?
Kaazi kweli kweli.....
 
..watu wengine wakipata kanafasi ka kutoka nje, inakuwa taabu. nawafahamu wengi tu ambao wakati mwingine hawapendi hata kuwa introduced kwamba wako nje ya nchi! Joob true true.
 
Operations za Mabenki Tanzania zinaitaji kuwa reviewed upya maana watu kama NMB wana software ambayo ni current ikiwa mounted kwenye operation software nzuri tu inayotumika na benki chache sana ulimwenguni ambazo zina cuting edge kwenye operations zake.

Tatizo linabaki kwenye resources and capacity planning yetu, huwezi kuniambia kuwa wanaweka pesa kila siku halafu waisjue kiasi gani kinaitajika kwenye kila ATM yao tatizo ni kutoweza kutumia hizo resources tulizonazo effectively bali tunafanya kazi ili kazi iende na si kulizisha wateja wetu.

Ukiwauliza even catchment area ya branch na ATMs zao hawawezi kukwambia exactly ni wapi na wanaexpect turn over ya withdraws wakati wa weekend kwenye ATMs hawawezi kukwambia kwa kuwa sisi ni wavivu wa kutumia data tulizonazo.

Unaweza kusema wanaogopa wezi kubomoa hizo ATMs na kuiba pesa lakini kuna issue ya risk assessment and dealing with it, bora nini wateja wako wapate tabu au wewe umaximize return kwa kuwasumbua.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom