Nilifikiri ni mimi peke yangu....
Mkuu umekula maharage ya wapi mbona hueleweki?
Kwa sababu uchunguzi unaendele sitaweka data zote humu ila muhimu kushirikishana uzoefu kwa waliokumbwa na masaibu kama hayaHii haina mantiki yeyote na wala haieleweki mara mdada, ushungi helezimekwama. Ww ni mgeni kwa matumizi ya ATM.
Jamani wizi huo upo, kuna ndg yangu kaibiwa hela zote kwenye account yake ambapo alienda kutoa hela kwenye atm na akamkuta dada mmoja mfupi kiasi, mweupe, mwembamba na alikuwa kavaa ushungi, huyo dada alikuwa anahangaika kutoa hela kwenye atm jirani na aliyoitumia ndg yangu. Anadai yy aliingiza kadi yake kwenye mashine akatoa kiasi cha fedha alichohitaji na kadi ikatoka, pasipo kuangalia akaweka kadi yake kwenye wallet. Baada ya siku kadhaa kaenda kutoa hela kwenye atm na kadi ambayo si yake bila mwenyewe kujua, alipoingiza password ikagoma so akaingia ndani kulalamika, si ndio kushangaa kadi si yake, kuomba bank statement akakuta pesa zishalambwa, na alipoomba kuona picha akaambiwa camera ni mbovu, alipoomba benk wamlipe kaambiwa ukiibiwa kupitia kwa macashier wa bank unaweza kulipwa lakini ukiibiwa kwenye atm au simbanking hulipwi kwani huo ni uzembe wako. Tukio hili limetokea moro
aiseeNimewahi kusoma mahali inakuwa hivi;
wewe unapoenda kwenye ile ATM yeye anakuwa ameshaifanyia mchezo mchafu ili utakapotoa ishindikane kwenye hatua za mwisho kabisa.
Wewe unapotoa yeye anakuwa ametega tu anakusikilizia akitegemea utakaoshindwa ni lazima utakimbilia ndani kuomba msaada.
Na kweli, ile dakika moja tu ya wewe kuingia ndani tu yeye anakuja kutoa kiasi ulichoomba wewe huku akitumia password yako ileile. Anacheza na
itakua umeme ulivyorud pesa ikatoka akajifaidia mlinziMie kwa kumbu kumbu zangu katika hizi mashine niliwahi poteza laki mbili sijui niseme kwa ujinga wangu? Nilichomeka kadi nikaomba laki2 wakati nasikia mashine ikihesabu umeme ukakatika. Ikatoka kadi tu pesa haikutoka ikabidi nimuulize askari mlinzi pale yale mazingira na kama yatakua na athari kwangu. Akawa amenijibu kuwa haina shida na itakuwa haikutoa pesa kutoka ktk account yangu. Nikaondoka na siku ile niliamua kubadili pesa ya kigeni niliyokua nayo kwa ajili ya matumizi. Nilisafiri na baada ya kama wiki tatu nilirudi na nilipoingia katika atm machine kutoa pesa niligundua balance iliyokuwepo ilikua imepungua laki mbili kwa salio langu la mwisho kutoa pesa.