Staa wa The Shield amuua mke wake

MstahikiMeya

JF-Expert Member
Jan 8, 2014
1,654
0
Aliyekuwa staa ya series maarufu ya The Shield, Michael Jace ametiwa mbaroni kwa kosa la kumuua mke wake. Staa huyo alijisalimisha polisi baada ya kumuua kwa kumpiga risasi aliyekua mke wake,April Jace, imerepotiwa.

Muigizaji huyo mwenye umri wa miaka 48 alikiri kumpiga mke wake risasi mara kadhaa baada ya ugomvi mkubwa uliotokea pale mke wake April, aliporudi nyumbani.

April alikua anarudi na watoto baada ya kuwachukua kutoka kwenye mazoezi ya kikapo.

Imesemekana kua muigizaji huyo alikua na hasira juu ya matumizi ya pesa aliokua akifanya mke wake licha ya hali yao ya kifedha kuwa mbaya.

Imeripotiwa kua hali yao ya kifedha ilikua mbaya mpaka kufikia kushindwa kulipia ada ya pango ya mwezi, sababu ambayo polisi wanahisi ilimfanya muigizaji huyo kupandwa na hasira na kuamua kumtolea mkewe.

Muigizaji huyo anajulikana zaidi kwa kuigiza kwenye series ya The Shield, Southland, Burn Notice pamoja na The Mentalist.

Muigizaji huyo ambae alizaliwa New Jersey nchini Marekani pia amewahi kuonekana kwenye filamu za Forrest Gump na Planet of the Apes ya mwaka 2001.

 

Attachments

  • michael-jace-and-wife.jpg
    File size
    19.9 KB
    Views
    983

Mamaya

JF-Expert Member
Jul 4, 2011
3,946
2,000
mambo ya ufoooo sarooooooooooo mpaka majuu, kina mushi wapo wengi
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Similar Discussions

Top Bottom