Ada kwa engineering yeyote pamoja na michango ni 3050400 kwa mwaka.Ili uweze kusajiliwa kima cha chini unapaswa ulipe 700000.Ukilipa chini ya hiyo utapaswa uandike barua ya kuomba usajiliwe na kuahidi utaongeza lini iyo pesa ili ifikie laki saba.Chuo kina hostel chache za girls zilizopo Kibamba na kodi kwa mwezi ni sh 15000,Kwa boys itawapasa mpange kwenye hostel za watu binafsi au mtu achukue room peke yake.Hostel za watu binafsi zipo nyingi karibu na chuo pia na mbali na chuo.Na kodi hutegemeana na idadi ya watu mliopo ndani ya room.Mnapokaa chumba kimoja watu wanne itampasa kila mtu kulipia 25000 kwa mwezi,watu wawil chumba kimoja kila mtu atalipia 35000-40000 kwa mwezi.Na unapohitaji room yako binafsi utalipia 50000-60000.Kwa room ambazo ni self kodi inaanzia 70000-100000 kutegemeana na hadhi ya chumba.Jambo la kuzingatia kama unatambua ada niya kubangaiza,Hiki chuo sio rafiki kwako.Fanya transfer mapema ili baadae usije kuhangaika.aaaHata ukilipa ada ukabaki unadaiwa sh 400 muhindi hatokuruhusu kufanya mtihani wa mwisho(UE),Na itakupasa urudie mwaka.Wahindi wanasheria za kipuuzi nyingi mfano ukichelewa kuingia ndani ya kipindi zaidi ya dakika tano,itakupasa uende library na utakuja kipindi kinachofuata.Hairuhusiwi kwa boys kuvaa tishet au sandozi na ukija umevaa utazuiliwa getini na utarudi hom ukabadilishe.Kuhusu mapindi wako vizuri sana hasa kwa civil,electrical and electronics pamoja na course za computer.Atendence huitwa na kila lecturer anapoingia kupiga pindi na mwisho wa siku asilimia za mahudhurio huangaliwa kwa kila somo ndipo utakaporuhusiwa kufanya mtihani husika.Utakapopata asilimia chini ya 75 utakuwa umesap somo husika automaticaly.Kwa wale wa mechanical duu sina cha kueleza mtakuja mshuhudie wenyewe.Note:Muhindi anapenda kuheshimiwa zaidi ya maelezo.