St. Francis Mbeya kwawaka moto........................ | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

St. Francis Mbeya kwawaka moto........................

Discussion in 'Jukwaa la Elimu (Education Forum)' started by Rutashubanyuma, Jan 19, 2011.

 1. Rutashubanyuma

  Rutashubanyuma JF-Expert Member

  #1
  Jan 19, 2011
  Joined: Sep 24, 2010
  Messages: 158,786
  Likes Received: 419,796
  Trophy Points: 280
  St. Francis Mbeya kwawaka moto


  na Christopher Nyenyembe, Mbeya


  [​IMG] UONGOZI wa shule ya sekondari ya wasichana ya St Francis iliyoko mjini hapa, umewatimua walimu wake wote waanzilishi.
  Habari ambazo Tanzania Daima imezipata jana na kufanya jitihada za kukutana na walimu walioachishwa kazi baada ya kugoma kusaini mkataba mpya, walidai sakata la kuvujwa kwa mkataba wao umefanywa na uongozi wa shule hiyo bila kuwashirikisha.
  Baadhi ya walimu wapatao sita waliofanikiwa kutinga kwenye ofisi za Tanzania Daima jana mjini hapa, walieleza kusikitishwa na hatua iliyofikiwa na uongozi wa shule hiyo inayomilikiwa na Kanisa Katoliki Jimbo la Mbeya kuwatimua bila kujali mchango wao huku wale wa mkataba wa kudumu wakitakiwa wawe wameondoka kwenye nyumba walizopewa ifikapo Januari 28 mwaka huu.
  Walimu hao ambao majina yao tunayo walidai baada ya mkataba wao kusitishwa na kudaiwa kuingia mkataba mpya huku wakiwa wanapaswa kulipwa mafao yao pamoja na penseni kwa kuwa uongozi wa shule hiyo uliridhia kuwalipa haki zote pale ilipowaomba kutoka serikalini, lakini hadi siku walipoachishwa kazi walikuwa hawajalipwa stahili zao.
  “Kitendo cha kutuachisha kazi bila kutulipa stahili zetu ni cha uonevu mkubwa, haiwezekani tusaini mkataba mpya kabla ya kulipwa haki zetu za mkataba wa zamani. Hilo tumelikataa ndio maana wameamua kutuachisha kazi na kutakiwa kukabidhi vifaa na nyumba zao ifikapo saa sita Januari 7 na sisi wa mkataba wa kudumu tuwe tumekabidhi nyumba saa sita kamili Januari 28,” alisema mmoja wa walimu hao waanzilishi.
  Huku wakionyesha kusikitishwa na uamuzi wa uongozi wa shule hiyo na kulalamikia ukiukwaji mkubwa wa haki zao na vitisho, walidai kuwa ndio walioweza kuifikisha shule hiyo hapo ilipo na kuiwezesha kuwa shule bora nchini, lakini wanashangazwa na kitendo cha kutimuliwa bila kujali juhudi zao.
  Tanzania Daima ilikwenda hadi shuleni hapo ili kuonana na mkuu wa shule hiyo aliyefahamika kwa jina moja la Sister Sabaya lakini mlinzi wa getini alipopiga simu alirudi na majibu kuwa uongozi wa shule hiyo uko kwenye kikao na walimu.
  Mkuu wa shule hiyo, Sabaya alipopigiwa simu yake ya mkononi iliiita bila kupokelewa lakini baada ya muda mfupi alipiga na kuelezwa la kutafutwa na mwandishi wa habari ndipo alipojibu, “Samahani mimi sio mwajiri, mwajiri ni askofu msifike hapa shuleni wala ofisini kwangu, msitusumbue,” akakata simu.
  Jitihada za gazeti hili zilikwenda moja kwa moja hadi kwenye makao makuu ya askofu wa jimbo hilo, Evaristo Chengula ambapo ilidaiwa na padri mmoja kuwa yuko safarini Mwanza na Padri Sanga ambaye anadaiwa kuwa ndiye mratibu wa elimu wa kanisa hili naye amekuwa safarini jijini Dar esa Salaam.
   
 2. Rutashubanyuma

  Rutashubanyuma JF-Expert Member

  #2
  Jan 19, 2011
  Joined: Sep 24, 2010
  Messages: 158,786
  Likes Received: 419,796
  Trophy Points: 280
  Waalimu hawa waelewa BWANA yu pamoja nao wasighafilike atawalinda njia zote watakazopita.................................

  Na hao wamiliki wa shule hawajui maana ya St. Francis...laiti kama wangelijua wasingefanya huu uonevu na dhuluma ya wazi wazi kabisa.
   
 3. Pearl

  Pearl JF-Expert Member

  #3
  Jan 19, 2011
  Joined: Nov 25, 2009
  Messages: 3,042
  Likes Received: 22
  Trophy Points: 135
  yap nimeskia jana kiukweli ngoma ikivuma sana hupasuka xul hii iliyosifika haswa sasa imeshaharibika kabisa!
   
 4. Wayne

  Wayne JF-Expert Member

  #4
  Jan 19, 2011
  Joined: May 27, 2009
  Messages: 663
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 35
  Mkulu
  Ngoja tusikie mwajiri anasema nini kabla ya ku-conclude..hope ur okay with that
   
 5. mama D

  mama D JF-Expert Member

  #5
  Jan 19, 2011
  Joined: Nov 22, 2010
  Messages: 1,755
  Likes Received: 35
  Trophy Points: 145

  jamani tusitoa majibu kabla ya kuujua ukweli lazima tusililze pande zote mbili kabla ya kusema waalimu wameonewa au uongozi umetenda haki!!
   
 6. Utingo

  Utingo JF-Expert Member

  #6
  Jan 19, 2011
  Joined: Dec 15, 2009
  Messages: 7,121
  Likes Received: 185
  Trophy Points: 160
  sababu ya kutimuliwa/kutosainishwa mkataba mwingine ni nni?
   
Loading...