Mr. SADC_TZ
Senior Member
- Nov 7, 2014
- 105
- 22
- Thread starter
-
- #61
mesi wa ajentina ni mrefu?
Labda atuambie Gianfranco Zola naye alikuwa mrefu?
Jaja alikuwa na mission moja tu kuwafunga lambalamba waitwao Azam FC. Kazi hiyo aliifanya na kuikamilisha vizuri sana, sasa amerudi kwao kupumzika.
Mkuu huitaji kuonyesha mapovu yako ili tujue kwamba unakerwa na ukweli..!nikuulize vizuri! je ww ni mfuatiliaji wa soka...!
Baada ya kujibu swali hili ndio ufanye ku-reply to my comment.
Tusije tukawa tunabishana kumbe mwezangu si mtu wa soka.
Yaani hata kujua nani mfupi zaidi kati ya Ngassa na Ssrernkuma...inakusumbua!
Mawazo kama haya ndio yanafanya muhindi apigiwe magoti kila akitaka kuachia ngazi.Ujinga wa kupewa medali ya ujinga.
hivi na mkongwe Danny Mrwanda wamemchukua tena au?
Stahamili mkuu! Ndiyo adha za kujadiliana na mashabiki vinyaa mitandaoni. Wakikuwa watawacha!Mjinga mwenyewe, unajiona una akili kumbe huna lolote! Shame on you Ngarna.
Mbona nasikia Azam ni bahari nyingine?Serunkuma ni mmoja kati ya washambualiaji bora na hatari katika ukanda wa Afrika Mashariki na Kati. Ni mchezaji tegemeo pia wa timu ya taifa ya Uganda inayotajwa kuwa timu bora zaidi katika eneo hili, na pia yenye wachezaji wengi wenye ushindani wa namba.
Pamoja na ufupi wake, anatarajiwa kuleta chachu ya ufumaniaji nyavu ndani ya kikosi cha Simba kutokana na kasi, wepesi, akili, shabaha ya goli na nguvu pia. Tofauti na Tambwe ambaye anamudu zaidi kama mshambuliaji namba moja, Danny anatoa option nyingi katika mifumo mbalimbali kwa sababu anaweza kushambulia kutokea kushoto au kulia, kati kama lone striker na pia kama mshambulizi namba mbili. Lakini udhaifu wake mkubwa ni uwezo mdogo wa kucheza mpira ya kichwa.
Kama Tanzania itampa mazingira kama ya Kenya, timu nyingine za Ligi Kuu lazima ziwe concerned na huyu anayeitwa kidudu mtu maana ni ukweli ulio wazi kuwa jamaa anajua, na kwa mipira ya Tanzania ya kukimbizana anaweza kuwika zaidi.
Kwa upande mwingine, napenda kuipongeza Simba kwa kusajili mchezaji baada ya kumfuatilia kwa muda mrefu badala ya kutumia usanii wa majaribio kumpa mtu mkataba. Nilitaka kusema imejifunza kutokana na makosa lakini kwa kuwa na majaribio ya huyo Mgabon naona inataka kurudi kulekule. Simba, Yanga na Azam ziache mara moja tabia ya kuwafanyia majaribio wachezaji wa kigeni na badala yake ziwe na maskauti watakaokuwa wanafuatilia mchezaji katika nchi za kigeni na anapokuja nchini apimwe tu afya na kupewa mkataba.
mtani jembe ni lini?
Ni kweli wamemsajili tena kwa dau dogo, si unajua Msongamanoni hawawezi ku-compete kwenye soko la kununua wachezaji bora na wenye gharama kubwa.
...katika hayo mambo ya JUJU waganda wako vzr sana mkuu...It takes JUJU in order to survive katika ligi hii.....! si umemuona Tambwe sasa hivi...yaani utafikiri mke wa nyumba ndogo.hata kocha Phiri hamjali....!...naona sasa aondoke arudi burundi ampishe Andunje.
Uongozi wa Aveva umeamua kutufanyia kituko kingine ndugu zangu...huu usajili wa haka kachezaji kafupi...sina uhakika nao..simply because kachezaji kaliongoza kwa magoli kwenye kaligi ka kenya sasa nao simba ndio wameona mlango wa kupitia...haka kachezaji ni kafupi kwelikweli...nilikaona pale msimbazi kalikuwa kanaingia ndani kumwaga wino.
Najiulizaga hivi kweli kataweza kuwakabili akina Canavaro na Yondani.
kusema kweli simba yangu ya nsimuu huu ni Ashki Majnuni.Ngoja niende kwa mtani Yanga (kwa mkopo)...hadi msimu huishe.
Mbona nasikia Azam ni bahari nyingine?
Ni kweli wamemsajili tena kwa dau dogo, si unajua Msongamanoni hawawezi ku-compete kwenye soko la kununua wachezaji bora na wenye gharama kubwa.
Tatizo pale Simba ni kuwa wachezaji hawasajiliwi na timu bali na viongozi. Mchezaji aweza kuchukiwa kwa sababu tu kasajiliwa na kiongozi fulani na kupendwa vilevile kisa ni aliyemsajili. Utashangaa muda huu Ivo au Tambwe hawana thamani kisa ni waliowasajili. Utashangaa wanamtafuta Kaseja ambaye hajaonekana uwanjani tangu ligi ianze ili wamteme Ivo. Wawaruhusu basi kina Tambwe na Chanogo waende Yanga na Azam ndipo waone majuto live. Uongozi huu wa Simba utakuwa majuto kwa wapenzi wa Simba mpaka watakapomaliza muda wao.