Spyware ni nini ?? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Spyware ni nini ??

Discussion in 'Tech, Gadgets & Science Forum' started by Yona F. Maro, Dec 5, 2006.

 1. Yona F. Maro

  Yona F. Maro R I P

  #1
  Dec 5, 2006
  Joined: Nov 2, 2006
  Messages: 4,237
  Likes Received: 33
  Trophy Points: 0
  “One of the biggest challenges a computer owner can face is getting rid of adware or spyware...” Reuters, Feb. 9, 2004
  Spyware defined:
  • Spyware is any application that tracks your online behavior without your knowledge or consent.
  • Spyware is now the #1 threat to online privacy, replacing viruses.
  • Ninety percent of internet-connected PCs are infected with a form of spyware.
  • Spyware ranges from somewhat innocuous (adware) to malicious (Trojans, system monitors, dialers, and keyloggers).

  Impact of spyware:
  • Unidentified spyware can expose private information, slow Internet access, reduce computer productivity or cause PC corruption, and result in increasing pop-up ads.
  • Spyware easily bypasses anti-virus software and firewalls by disguising as a legitimate download, then surreptitiously installs on your system without your knowledge.
  • Many spyware programs intertwine with system functions or desirable programs, making it almost impossible to remove spyware manually.

  Spyware infection can happen when:
  • You use the Internet for even a few minutes to visit web sites.
  • You download shareware or freeware applications.
  • You swap or share music or photo files with other users.
  • Your computer is used by others.


  Spyware Stories
  “Spyware is like adware, except that it has gone completely over to the dark side, scanning your hard drive for personal information or attempting to link your surfing habits to your name or e-mail address.” PC World, July 23, 2003
  • Last July, a keystroke logger was installed on several public Internet terminals in 13 copy shops in Manhattan. The person who installed the program stole more than 450 online banking passwords from unwitting customers during a two-year period.

  • Attempting to mitigate his own financial losses, a 19-year-old online trader used tracking software to gather online brokerage account username and login information from his victims' computers.
  *****************
  Well, now you have the story – what can you do about it?
  There are several software available to scan and selectively remove spyware. One of them that is effective and has received good reviews is ‘Adware’ by Lavasoft. Next time we will go into more detail on spyware and get into how to install and run the ‘Adware’ spyware remover software.
   
 2. Yona F. Maro

  Yona F. Maro R I P

  #2
  Jun 21, 2007
  Joined: Nov 2, 2006
  Messages: 4,237
  Likes Received: 33
  Trophy Points: 0
  Spyware ni programu yenye muundo wa malware inayoweza kuichukuwa computer yako a kutoa siri za computer yako kwa watu wengine wenye kutaka taarifa hizo . Spyware huwa inatawanywa kupitia baadhi ya tovuti mtu anazotembelea na ujanja unaotumika zaidi ni wa programe yenyewe kujiingiza bila thini yako kwanjia ya download na zingine huja na programe haswa za bure na zile cracks

  Hapa chini kuna ishara 7 za kuonyesha komputa yako imeshambuliwa na spyware au programe zinazohusiana na spyware

  1 ) Browser yako haswa internet explorer inajibadili home page kama ilikuwa ni www.pwani.co.nr inaweza kuwa ni www.msanii.co.nr bila taarifa na bila wewe kuiambia ibadili hiyo home page

  2 ) Kama umekosea kuandika URL tovuti katika browser yako au ukitafuta kitu mfano katika msn search inakupeleka katika tovuti za ajabu ajabu ambazo wewe hukuandika .

  3) vitu vipya haswa matangazo yanajiweka katika favorites zako na bookmarks zako haswa smileys na promotion mbali mbali haswa za bidhaa za bure na offer za kucheza kamari

  4 ) wakati mwingine browser yako inakuwa na toolbar ya ziada ambayo hukumbuki kama uliwahi kuinstall mara nyingi ni ya screensavers na zingine za popups

  5 ) ukiwa unatembelea tovuti mbali mbali katika mtandao unakutana na popups za ajabu ajabu kama za porn na matangazo mengine ambayo hayahusiani na shuguli unayoifanya , lakini baadhi ya tovuti zina popups zao wenyewe kama yahoo na google , la zaidi mfano ukitembelea tovuti za masoko kama ebay unapata upinzani toka katika tovuti zingine kwa mtindo wa popups

  6) computer yako inaanza kuwa na tabia za ajabu haswa ukitembelea tovuti au ukifanya shuguli zingine

  7 ) Computer yako inaaza kuwa slow kutokana na hizi spyware ( lakini angalia zaidi system yako inaweza kuwa ni RAM vitu vingine )

  Kama unaamini computer yako imeasirika na spyware bora upate antipyware haraka iwezekanavyo ili uweze kuendelea na shuguli zako kama kawaida
   
 3. Yona F. Maro

  Yona F. Maro R I P

  #3
  Jan 27, 2009
  Joined: Nov 2, 2006
  Messages: 4,237
  Likes Received: 33
  Trophy Points: 0
  SPYWARE NI NINI ?

  Computer yako ina pop up blockers , ina pop up killers na kadhalika lakini
  unaona popup nyingi sana zinakuja , saa nyingine computer yako haina hata pop up
  blockers lakini popup windows zinakuja tu bila kuitwa , zinakutelea website
  mbali mbali ambazo wewe hukuchagua zifunguke , lakini zinafunguka kwa lazima au
  kilazima .  Kwanza nitaeleza popup window ni nini ( pop up window ni kurasa za tovuti (
  webpages ) ambazo hufunguka juu ya page Fulani , kwa kufunguliwa au bila
  kufunguliwa , mfano tembelea site hii www.darmoto.8m.net hapa kuna page ingine
  itakuja hiyo ndio popup window .

  Kwanini watu wanatengeneza popups ? ni kwa sababu katika kurasa nyingine kuna
  nafasi kidogo ya matangazo so wanatumia popups kutangaza bidhaa fulani au
  huduma Fulani .  Kwasiku hizi sio popup zote ni nzuri , ukiona website inafungua popup zaidi ya 3
  kwa mpigo ujue hiyo sio pop ya kawaida , hiyo ni spyware .  Je spyware ni nini ?

  Spyware ni programme ndogo ndogo zinatengenezwa kwa ajili ya kutangaza huduma za
  website Fulani au compuni Fulani , hasa za ngono au casino , na wakati mwingine
  kupepeleza computer za watu Fulani au shirika Fulani , spyware nyingi
  zinapatikana katika chatrooms hasa za IRC au msn na Yahoo chatrooms ndio
  zinaingia kwa hapo .

  Lakini sana zinatumika katika uchunguzi na upepelezi kutumia spyware mtu wa
  marekani anaweza kuamuru computer yako hapa tz ifanye anachotaka yeye .  Spyware haionekani wakati inapoingia sawa na virus , vile vile spyware haiwi
  detected na antivirus lazima uwe na spyware remover ndio utowe spyware sio
  antivirus.  Utajuje kama kuna spyware katika computer yako ?

  1- inafungua popup windows zaidi ya 3 mara kwa mara , hata kama hujafungua
  site Fulani yenyewe itafungua tu

  2- computer yako inakuwa slow kupita kiasi , hasa katika kufungua site
  Fulani kama yahoo.com na hotmail , jua kwamba yahoo ndio site inayofunguka kwa
  haraka kuliko site yoyote duniani , mara nyingi teste kwa kutumia yahoo spead ya
  internet .

  3- utaona computer ina freeze ukifungua baadhi ya page , hii ni kwa sababu
  spyware huwa ina dial kama simu , kwahiyo ukifungua site Fulani mfano yahoo ,
  spyware itataka kudial wakati wewe unatumia broadbad au dsl na sio dial ,
  mchanganyiko hutokea .

  4- ukifungua page kama yahoo , ina kuredirect na kukupeleka mfano seach.com
  na nyingine ambazo wewe hutaki .

  5- ukifungua page mfano google ukiseach kitu Fulani , utaona majibu yanakuja
  lakini katika seach engine nyingine na sio google .  Nitatowaje Spyware ?

  Kuna programme nyingi watu wanatengeneza na ambazo ni nzuri lakini nyingi
  haziendani na matakwa ya watu wengi , nyingi haziko tested na nyingi sio rahisi
  kutumia hazieleweki , ila chukuwa zote , kwa sasa hivi adware na windows care ndio programme
  nzuri zaidi kwa ajili ya kutowa spyware katika computer yako , unaweza kupata
  adaware kupitia hapa Tucows Download kuna aina nyingi zaidi ila mpaka ujaribu na uone zinazofanya kazi kwamimi nimetumua hizo  Kwa mtumiaji wa kawaida tu , unaweza kuchukuwa adaware 2008 Profesinal , Windows care kuanzia ver 2 au professional na kuna spywareboot ingawa kuna aina mbali mbali za programu za kuondolea spyware hata antivirus ambazo ni all in one nazo zina uwezo wa kukuondolea spyware katika computer uki download programu hizo utakuta maelezo yake jinsi
  ya kutumia na kutowa spyware katika computer yako au ukishanstall angalia katika help au unaweza kusearch katika google utapata maelezo zaidi  Nifanye nini nisipate spyware na virus ?

  1 Siku zote katika utumiaji wa computer yako hakikisha una firewall , kwa
  ajili ya kuzuia intruders wasiweze kupata upenyo katika computer yako au website
  yako na kadhalika , kuna firewall za aina nyingi kama mcafee firewall hata
  Norton , panda na kadhalika , lakini nzuri na rahisi kuliko zote ni zonealarm
  version 4 na kuendelea , kwa kutumia zone alam unaweza kuchakuwa programme ipi
  unapenda kutumia na ipi hutumii lakini hizo nyingine hazina function hizo

  2 Kama unatumia antivirus hakikisha unafanya update kila baada ya siku 3
  au 4 , ili kuweka tools na definition za kisasa zaidi , hizi updates unaweza
  kuzidownload na hata kuweka kwa floppy kwa watumiaji wa nyumbani mfano Norton
  nenda Symantec This Page Has Moved hapa utapata definition za kisasa , kwa mcafee
  tembelea site yao pia ila nying rahisi ni kudownload scanner moja inaitwa
  stinger kutoka mcafee

  3 Usitumie programme yoyote ambayo huijui au ambayo hujawahi kusikia
  sehemu yoyote , tafadhali uliza watu wa technical support wataweza kukushauri
  zaidi kuhusu matumizi ya program mbali mbali kutokana na kazi yako au taaluma
  yako

  4 Usitembelee site za kuhusu ngono au za bingo na casino ( camari )
  spyware nyingi hata virus wengi wanatokana na site hizi , ingawa kuna tovuti za kamari ambazo ni salama au za bahati nasibu

  5 Usipende kutumia floppy , cd ,au flash kwa computer zaidi ya 4 ( kama huja scan na kama huamini computer hizo haswa kama imetoka nje ya officer ) , kama
  ni kazini na nyumbani ni hivyo tu usiitumie na internet café pia , kati ya
  computer 4 utakazotumia 2 zitakuwa na virus au spyware , hiyo ni lazima kama
  huna updates za kisasa huwezi kujua kama virus iko mpaka ianze kufanya maajabu .

  6 Pia kusoma makala na issue mbali mbali kuhusu utumiaji wa computer na
  program mbali mbali kufanya hivi utajua jinsi ya kutatua matatizo mengi
  ,computer za siku hizi sio lazima kuita fundi wa computer ni wewe mwenyewe tu na
  roho yako haina maajabu yoyote ya kukufanya utishike .

  7 Cha mwisho jiunge na club mbali mbali wa vijana wa computer kama

  techtz : Tanzania Technical Support Forum

  Katika group hizo kuna watu wengi wanaweza kukusaidia kwa kujibu maswali yako na
  kero zako kuhusu computer , maisha , na mambo mbali mbali tena kwa lugha ya
  kiswahili .

  Mwisho kabisa ukiona kitu chochote usichoelewa katika computer yako uliza usichoke kuuliza utaeleweshwa na kusaidiwa kwa ukaribu zaidi


  Kwa msaada zaidi unaweza kuniandikia
   
 4. Kaa la Moto

  Kaa la Moto JF-Expert Member

  #4
  Jan 27, 2009
  Joined: Apr 24, 2008
  Messages: 7,666
  Likes Received: 166
  Trophy Points: 160
  Asante mkuu kazi yako ni njema
   
 5. K

  Koba JF-Expert Member

  #5
  Mar 13, 2009
  Joined: Jul 3, 2007
  Messages: 6,144
  Likes Received: 495
  Trophy Points: 180
  ...natafuta ant spyware ya bure,iko wapi?
   
 6. Yona F. Maro

  Yona F. Maro R I P

  #6
  Mar 13, 2009
  Joined: Nov 2, 2006
  Messages: 4,237
  Likes Received: 33
  Trophy Points: 0
 7. Y

  Yassin JF-Expert Member

  #7
  Mar 13, 2009
  Joined: Jul 23, 2008
  Messages: 326
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0
  Asante sana mkuu kwa maelezo yako mazuri
   
 8. Tumsifu Samwel

  Tumsifu Samwel Verified User

  #8
  Mar 13, 2009
  Joined: Jul 30, 2007
  Messages: 1,406
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 135
  heshima kwako mkuu
   
 9. UncleUber

  UncleUber JF-Expert Member

  #9
  Apr 19, 2013
  Joined: Apr 25, 2011
  Messages: 4,945
  Likes Received: 100
  Trophy Points: 145
  salute to you Shy
   
  Last edited by a moderator: Jan 4, 2016
Loading...