Sprinkler Guns za Umwagiliaji

ASHA NGEDELE

JF-Expert Member
Jul 5, 2011
784
326
Habari wadau/wataalamu,

Katika kutatua changamoto za gharama ya kilimo nimekutana na hii teknology ya kutumia Sprinkler guns kumwagilia eneo kubwa na kupunguza gharama ya kulipa vijana wa umwagiliaji.

Nachoomba kujua kutoka kwenu ni elimu ya;

1. Kumwagia ekari 10 (mfano), nahitaji Gun yenye uwezo upi? Nyingi nimeona zinarusha maji kuanzia 20m mpaka 45m. Zipo pia za 70m. Natakiwa nizingatie specifications gani?

2. Ili kutumia hizo Gun kwenye capacity yake natakiwa ninunue water pump ya uwezo gani?

3. Je maji ya kisima cha kuchimba na mashine yanatosha kwa umwagiliaji huu? Au lazima nilime pembeni ya mto. Mana inaonekana maji yanatumika mengi sana kumwagia eneo lote na sio mashimo yenye mmea.

4. Guns za nchi gani ni imara au hata hizi cha China hazina shida. Maduka mengi ya pembejeo mjini nimekuta wanauza between 200k na 300k na karibu zote za China.

Nitashukuru wataalamu wakinipatia majibu haya na taarifa nyengine za muhimu.
FB_IMG_1537116767033.jpg
 
Utafute mtaalam.wa irrigation kutoka ofisi ya kilimo ya wilaya/manispaa uliyopo afike shambani afamyie tathmini chanzo cha maji, shamba likoje, aina ya udongo,nk. Huwezi kupewa ushauri humu ukaufanyia kazi.
 
Mkuu hizi forum lengo kuu ni kushauriana masuala ya kilimo kutoka kwa watu wenye experience. Binafsi nalima mwaka karibu wa nne na nimepata ushauri sana humu.

Ushauri wa kumfata Afisa kilimo nimpeleke shamba ni mzuri lakini mgumu sana. Gharama ni kubwa za kumfikisha shambani
 
Kupunguz matumizi ya maji na mahitaji na ya pump capacity, nakushauri uangalie utaratibu wa kutumia "drip irrigation system". Pia, ili kupata ushauri mzuri, inabidi utoe extra info kuhusu huo mradi wako. Je unamwagilia zao gani ? Shamba lako liko maeneo/ukanda gani? Hali ya hewa hua ikoje kea wastani? Udongo wa shamba lako ni wa aina gani? etc...
 
Habari. Shamba liko Vianzi lina kichanga sana kwahio drip irrigation hazinsaidia sana kwahio napiga dumu. Nalima melons na nataka kwenda large scale from current 1-2 acres to around 5 acres.
 
Kupunguz matumizi ya maji na mahitaji na ya pump capacity, nakushauri uangalie utaratibu wa kutumia "drip irrigation system". Pia, ili kupata ushauri mzuri, inabidi utoe extra info kuhusu huo mradi wako. Je unamwagilia zao gani ? Shamba lako liko maeneo/ukanda gani? Hali ya hewa hua ikoje kea wastani? Udongo wa shamba lako ni wa aina gani? etc...

Usiishie kusema tu kupunguza matumizi ya maji bila kujua mazingira yake, binafsi Kwa kawaida kila njia in a faida na hasara zake hasara ya drops ni initial cost, na farm plan inatakiwa isibadilike sana, mfano umeplan nyanya basi we hauwezi badili zao, faida zake Ndio kutumia maji kidogo na weed control kwamba magugu hayapati maji isipokuwa mmea uliolengwa tu.

Kwa upande mwingine sprinklers faida yake ni Kwamba unaweza design shamba vyovyote na ukawa ma crops flexibility pia mbinu hii inafaa Kama maji ni mengi yanapatikana bila gharama, hasara yake ni magugu pia yanachanua sambamba na mimea yako. Ila Ndio mtaji wa mwanzo Sio mkubwa Kama drip irigation sababu unaweza ukapata sprinkler gun ya ku cover radius ya 20Metres au zaidi utajionea mwenyewe katika ekari moja utahitaji sprinkler gun ngapi.
 
Mkuu umeongea kitaalam sana, nakubaliana na ww kwa hizo economic aspect ya sprinklers vs drip. Mimi sio mtalaam wa hayo mambo, naamini unaweza kumsaidia mdau ushauri wa kitalaam zaidi.

Labda niongezee tu kwamba badhi ya vitu vya kuzingatia wakati wa kuchagua hizo sprinklers:
- precipitation rate ya sprinklers (kasi ya kunyeshea!) isizidi uwezo wa udongo kunyonya maji. Hili nadhani sio shida kwa vile udongo wako ni kichanga, hivyo kuna wide range of choice.
- Ni vyema kuchagua sprinkler ambayo inaweza ku operate kwa pressure ndogo ili kupunguza matumizi kwenye pump (tafta kwenye range ya 250-300kPa).
- Kuhusu pump, inategemea na chanzo chako cha maji kiko umbali gani (e.g. kama kisima kina urefu gani) na pia mahitaji ya mazao yako na pressure ya sprinker. Hapa ndio umakini mkubwa unapohitajika, otherwise unaweza kununua system isiyoendana na mahitaji yako, na itakua hasara kubwa.

Kama kuna mtalaam wa haya mambo amsaidie mdau kufanya hayo mahesabu, mimi huo uwezo sina, najuaga kwa mdomo tu badhi ya hizo factors.
 
Nashukuru sana mkuu umeongeza mwanga mie nimejifunza kufuatilia sana hizi technology za umwagiliaji naona watu wanavyomwagilia na hizi pump za petrol kutumia hose meme mno na usumbufu wake huwezi mwagilia shamba kubwa nikawaza hiyo sprinkler nikaona ni wazo zuri kulifanyia kazi nilishaona Aryana mashamba ya miparachichi jioni mtu anawasha pump ananyeshea muda mfupi tu anazima inasave mafuta kwamba shamba lako lite linapata maji Kwa muda Sawa ni Kama mvua tu inavyonyesha, napenda kwenye Uzi atokee irrigation engineer atupe vipimo vya sprinklers vinavyo accomodate mazao mengi pamoja na pump inayofaa. Kilimo Kwa kutumia technology kutaenda next level na swala la chakula na mazao ya biashara litaonekana linamaana sana, ifikie wakati mtu akitaka kulima zao lolote asingoje msimu wa mvua uwe unaamua tu, nimeshavuna maharage ngoja nipande mahindi.
 
Uko sahihi kabisa. Tatizo kubwa watu wengi hawapendi kutumia wataalam. Kwa project kama hii ya mdau kama kweli anataka ushauri mzuri atafte irrigation engineer, wapo kila wilaya na kwenye zonal irrigation offices. Ukitoa hela kidogo (e.g. 500k -, 1M) utapewa vipimo vyote. Kwenye gharama ya uwekezaji, ushauri wa kitaalam haukwepeki kama unataka kulima kisasa na kibiashara.
Huo mradi ni mkubwa,
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom