Sports Bar ya Clouds TV Shikamoo

barafuyamoto

JF-Expert Member
Jul 26, 2014
32,323
29,586
Habari zenu!
Katika Tv hasa upande wa michezo hususani soka, Clouds Tv kupitia Sports bar na Sports Xtra, wanajitahidi sana!
Hawa jamaa HAWASUBIRI kuletea habari na BBC au chaneli za mbele, huwa wanaenda kwenye matukio.
Kombe la dunia walienda Brazil, huwa wanaenda wao wenyewe kwenye matukio. Uchaguzi wa FIFA pia walienda!
Kipindi cha leo nimependa documentary ya Mbwana Samatta huko Ubelgiji.
Tv zingine muige, hasa mnaodai mmeleta mapinduzi, Azam Tv, kitu Azam mnamiss ni ubunifu na materials ya kutangaza! Vifaa mnavyo!
 
Azam TV Ni Jipu Lililoiva Na Nikurekibishe Tu Sports Xtra Ilikuwa Zamani Siku Hizi Utani Na Soga Vimezidi.
 
shaffih dauda n mganga njaa na nimojawapo ya watu wanaotuharibia soka nchini hivi aliwahi kwenda tp mazembe kumhoji Thom ulimwengu, kwa ngasa South Africa ?
 
Sportsbar sio tu ni journalists bali wajasiariamali
watoto wa mjini
kila wanachoenda kukifanya ujue wama maslahi nacho

Samatta wana mgao wao...wao ndio publicity wake...
wanafanya kazi ya kumtangaza

umewahi jiuliza why hujawahi ona chochote kumhusu
Thomas Ulimwengu?...
 
Tatizo la watanzania hawataki kuona umepata mafanikio makubwa wanataka mafanikio ya kawaida Kama vile azam tv Ana studio nzuri vifaa vyote lakini hawana miundombinu basi hawa watapendwa lakini akitokea mtu anayefanya kila kitu utaskia siyo bure kuna maslahi embu jiulize nafsi yako inataka nini na siyo iulize imetoa wapi
 
Sports extra na Sports bar ni vipindi bora vya michezo bongo vinaburudisha watazamaji na wasikilizaji sana, sijui mlikua mnataka wafanyaje
 
shaffih dauda n mganga njaa na nimojawapo ya watu wanaotuharibia soka nchini hivi aliwahi kwenda tp mazembe kumhoji Thom ulimwengu, kwa ngasa South Africa ?
Wabongo hatukosagi maneno... Sasa ulitaka akamhoji ulimwengu au ngasa kwa lipi haswa?!! Lazima kuwe na jambo la maana ili kumtengenezea documentary mtu husika, kwasasa hakuna asiemjua popa Africa coz ndo mchezaji bora Africa, sasa ebu nambie ngasa ndo mdudu gani kwasasa?! Ngasa alipewa publicity ya kutosha kipind anawika mpaka akiwa kwenye majaribio West ham shafii huyu huyu ndo alikuwa anamfatilia na kutupa update zake au umesahau?
 
Subiri man u afungwe sport bar husiki tena akifungwa arsenal,chelsea or utajua tu kua sport bar ipo
 
Waongo sana wale jamaa, haswa shaffi dauda, final ya atletico na real madrid uefa, mpira ulivyoisha ronaldo alimpa moja ya shabiki wake jersey, hakuna mtu aliekuwa akimfahamu huyo shabiki, kumbe alikuwa rafiki yake mkubwa aliyesababisha ronaldo kufikia pale, sasa shaffiii sasa, anasema kwa faida ya watazamaji, huyu ni kakaake wakuzaliwa tumbo moja, aliyesota bla bla bla kibao, wananichoshaga, afadhali yule dogo mwembamba na miwani huwa anafacts anapoongea.....
 
Sasa bora kipi? Wamtangaze au wakae kimya?
Sportsbar sio tu ni journalists bali wajasiariamali
watoto wa mjini
kila wanachoenda kukifanya ujue wama maslahi nacho

Samatta wana mgao wao...wao ndio publicity wake...
wanafanya kazi ya kumtangaza

umewahi jiuliza why hujawahi ona chochote kumhusu
Thomas Ulimwengu?...
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom