Mponjoli
JF-Expert Member
- Feb 29, 2008
- 668
- 158
Wadau naomba kuwasilisha.
Kiongozi wa juu wa serikali kwa cheo cha Spika wa Bunge ni mtu muhimu sana kwa wananchi na ni vyema tukaendelea kujulishwa na uongozi wa bunge kuhusu aliko.
Imekuwa muda mrefu hakuna taarifa rasmi kuhusu mahali aliko, kama anaumwa au la, anaendeleaje, afya yake imeimarika, au yuko mapumzikoni...
Nadhani ni vizuri tukajenga utamaduni wa vyombo vya umma kutoa taarifa kwa wananchi kwa mambo ya kitaifa. Mfano kiongozi wa muhimili mmojawapo wa dola hajaonekana kwa muda mrefu, bunge likiendeshwa na Naibu Spika bila taarifa zozote rasmi. Inatakiwa wananchi tuendelee kujulishwa kila kinachoendelea maana ni kiongozi wetu.
Nawasilisha