Spika wa Bunge la Afrika Mashariki ang'olewa

dubu

JF-Expert Member
Oct 18, 2011
3,496
3,461
10404452_655571837887127_2784835506786498902_n.jpg

Mh.Margreth Zziwa

SPIKA ANG'OLEWA: Spika wa Bunge la Afrika Mashariki (EALA) Margreth Zziwa ameng'olewa leo baada ya wabunge 36 kati ya 49 kupiga kura za ndio. Vilevile wamempa saa 24 kukabidhi ofisi hiyo.
 
-Habari za hivi punde zinasema spika wa Bunge la Afrika Mashariki mh.MARGERET ZZIWA aondolewa katika wadhifa wake baada ya kupigiwa kura za kutokuwa na imani naye.
-Kura za ndiyo zilikuwa 36 Hapana ni 2 na 1 imeharibika.
-Kura zimepigwa bilateral yeye kuhudhuria na maamuzi haya yalisimamiwa na m/kiti.
-Reporter ni KHALFANI LUINDI TOKA ARUSHA.
 
mimi hata sionagi faida ya hili lidubwasha.....among the very useless inter regional organ i had ever seen all over the world.
Sio hiyo hata African Union inafanya nini? Inapokea amri toka Umarekani na nchi za magharibi. Libya imekuja pinduliwa na majeshi ya magharibi ndani ya nyumba(Africa) yao na Raisi wake kuuwawa wamefanya nini. Kwa mujibu wa Katiba yao hawatoshirikiana na nchi ya Africa inayopinduliwa na jeshi, wakajaribu kutaka kujifanya wakali wakati Misri serikali ya Muslim Brotherhood iliongia madarakani kidemokrasia ilivyopinduliwa na jeshi walijitia kutaka kuvunja uhusiano na serikali ya kijeshi ya misri hawakuchukua muda walipoamrishwa na Umarekani na nchi za magharibi wasiingile suala hilo, wenyewe nchi mmoja mmoja zikaanza kuitambua na kushirikiana nayo bila kujali kuwa wanaenda kinyume na katiba yao. Africa hatutakua huru mpaka pale tutapojikwamua kiuchumi siyo kwenda kupiga domo maneno mengi Makao makuu ya jumuia yetu huku tunategemea matatizo yetu yamalizwe na nchi za magharibi.
 
Shyrose Bhanji alimpiga mbunge mwenzake kutoka Tanzania katika harakati zake za kumwokoa huyo Spika. She was backing the wrong horse!
 
Sio hiyo hata African Union inafanya nini? Inapokea amri toka Umarekani na nchi za magharibi. Libya imekuja pinduliwa na majeshi ya magharibi ndani ya nyumba(Africa) yao na Raisi wake kuuwawa wamefanya nini. Kwa mujibu wa Katiba yao hawatoshirikiana na nchi ya Africa inayopinduliwa na jeshi, wakajaribu kutaka kujifanya wakali wakati Misri serikali ya Muslim Brotherhood iliongia madarakani kidemokrasia ilivyopinduliwa na jeshi walijitia kutaka kuvunja uhusiano na serikali ya kijeshi ya misri hawakuchukua muda walipoamrishwa na Umarekani na nchi za magharibi wasiingile suala hilo, wenyewe nchi mmoja mmoja zikaanza kuitambua na kushirikiana nayo bila kujali kuwa wanaenda kinyume na katiba yao. Africa hatutakua huru mpaka pale tutapojikwamua kiuchumi siyo kwenda kupiga domo maneno mengi Makao makuu ya jumuia yetu huku tunategemea matatizo yetu yamalizwe na nchi za magharibi.

naona SADC ina-make sense hata kuliko AU.
 
Back
Top Bottom