Kijogoodi
JF-Expert Member
- Mar 29, 2021
- 1,363
- 2,372
Naam.
Tangu mwaka 2018 pale spika Ndugai alipolipiwa kila kitu na wachina kwenda kuonyeshwa presentation ya namna bandari ya Bagamoyo itakavyokuwa ikijengwa, basi amegeuka mpiga debe wao!
Ndugai akiulizwa kwani bandari zilizopo zina kasoro gani hadi upigie debe Wachina kiasi hiki? Ndugai hana jibu ila yeye anachotaka bandari ijengwa.
Ndugai akiulizwa atoe mifano ya nchi zilizofanyiwa uwekezaji wa namna hiyo na wachina alafu zikafanikiwa hataji, akiambiwa mbona Srilanka, Mombasa, Zambia wanalia kwa uwekezaji na namna hii? Ndugai hana jibu ila anachotaka ni bandari tu ijengwe.
Ndugai akiulizwa, alikuwa wapi toka mwaka 2018 alipobaini rais Magufuli amedanganywa kutoa ukweli wote hadharani bungeni ? Alikuwa anaogopa nini wakati spika hawezi kutumbuliwa na rais? Ndugai hana jibu ila anachotaka tu wachina wapewe Bagamoyo!
Ndugai akiulizwa huo mkataba unaousema ni mzuri uko wapi uweke hadharani ili kila mtanzania ajiridhishe na matunda yatakayopatikana baada ya wachina kuwekeza Trilioni 23? Ndugai hana jibu!
Kiukweli ni aibu kubwa sana kwa nchi yetu kama mtu anaweza kufikia ngazi ya spika wa bunge alafu akashabikia na kuwa mpiga debe kwa faida ya nchi nyingine.