Spika wa bunge akiri uwezo wa CHADEMA

Izack Mwanahapa

JF-Expert Member
Apr 21, 2011
497
236
Spika wa Bunge la Jamuhuri wa muungano wa Tanzania amekiri uwezo walionao wabunge wa CHADEMA. Ameyasema hayo mara baada ya kupitishwa kwa mswada wa katiba mchana huu kwa kusema kuwa, "wabunge wa chadema hawajaitumia haki yao ya kuchangia mswada huu, nilittegemea mswada huu usingeisha leo, ungekaa wiki nzima kutokana na amendments ambazo wangeziwasilisha"

Hii ina maana kwamba mswada umepitishwa leo kutokana na wabunge walioshiriki mjadala ambao ni zaidi ya 300 kutotoa amendments za kutosha, hivyo kukosekana kwa mchango wa wabunge wa CDM kumedhoofisha maboresho ya mswada huo.
 
Sitaki kuchangia hii thread maana nimeapa sitotoa matusi ya nguoni kwa mtu mzima kama Makinda, ukiachilia mbali kupata ban
 
kwa hiyo wameupitisha?

Wameupitisha huku Makinda yakisema kuwa, 'jana nimekutana na kiongozi wa upinzani bungeni kutaka kujua kwa nini wamesusia. Nimesoma tena na tena kanuni, nimewauliza na wataalam wangu, wote hatujaona kabisa mahali tulipokosea katika kanuni zetu. Mwishowe tumekubaliana kutokukubaliana. Mswada huu unasubiri hatua moja, ya Rais kuweka sahihi ili uweze kuwa sheria. Wenzetu wapinzania wanamshawishi Rais asiweke sahihi, sioni kwa nini Rais asiweke sahihi. Nilitegemea kuwa mjadala ungekuwa mkali sana, na nilifikiria huenda tusingemaliza leo kutokana na ammendments ambazo wangezileta wenzetu. Kwa kweli wenzetu hawajawatendea haki watanzania. Wangeshiriki, wangetoa mawazo yao, wananchi wangewasikia, na kama tungekuwa hatujazingatia mawazo yao, hata wangeamua kuandamana, wananchi wangekuwa wamejua kwa nini wanaandamana LAKINI kwa sasa wananchi wataandamana hata bila ya kujua kwa nini wanaandamana'
 
Hivi wana zuoni na wafanya kazi woote hawana la kusema kuhusu maandamano ya kupinga muswada huu? Point is : wao kama pressure groups muhimu wana nafasi kubwa kama watasupport hii movement!
 
Wizi mtupu kama alitaka ammendments kwa nini aliwakatalia kuongea tangu mwanzo,hebu waache unafiki wa kipuuzi na sasa ngoja tujiandae kwa lolote kwani rais hawezi kukataa kuusign wakati ulitolewa na serikali yake
 
Mama Makinda kazi unayo na hili bunge la vihiyo/wengi vs walioenda shule/wachache
 
Sitaki kuchangia hii thread maana nimeapa sitotoa matusi ya nguoni kwa mtu mzima kama Makinda, ukiachilia mbali kupata ban

Kwani huwezi kuchangia bila hayo unayoita matusi?We changia bwana nchi ifaidike na mchango wako,wala haijaandikwa mahala kwamba hii thread ni special kwa matusi.Usikwepe majukumu mkuu.
 
Back
Top Bottom