Spika Tulia apiga 'stop' agizo DC Mbeya

Spika Tulia apiga 'stop' agizo DC Mbeya

Spika wa Bunge la Tanzania, Dk Tulia Ackson amesitisha agizo la Mkuu wa Wilaya ya Mbeya (DC), Dk Rashid Chuachua la kuwataka wakulima zaidi ya 1,700 kupisha eneo lenye ukubwa wa hekta 120 linalotumika kwa kilimo cha umwagiliaji katika Skimu ya Iganjo Bonde la Uyole jijini Mbeya.

Dkt. Tulia ambaye ni Mbunge wa Mbeya Mjini ametoa kauli hiyo leo Alhamisi Julai 21,2022 wakati akizungumza na wakulima wa skimu hiyo siku mbili baada ya mkuu huyo wa wilaya kutoa agizo la kuwataka kuondoka au kuomba kibali cha kuendelea kulima katika eneo hilo ambalo linadaiwa kuwa na mgogoro baina ya wananchi na wizara ya afya.

Dkt. Tulia amesema ameshtushwa na agizo hilo na amelazimika kufika kuona uhalisia na kutoa maamuzi ya kutoondolewa baada ya kukaa na pande zote mbili na kuona uhalali wa eneo na hivyo kuwatia moyo wananchi wawe watulivu wakati wakighulikia kubadili hati ya jina.

''Ndugu zangu hapa hamuondoki kwani eneo lina miaka mingi limetumika kwa kilimo cha umwagiliaji na mababu zetu sasa leo hii limeingia kwenye mgogoro na wizara ya afya nimesema ruksa na muwe watulivu wakati taratibu zinaendelea,'' amesema

Dkt. Tulia amesema, “nimekaa na watu wa pande zote nimejiridhisha na tumekubaliana hapa hamtaondoka na Jiji wataangalia namna ya kutenga eneo kwa ajili ya uwekezaji wa huduma za afya.''

Kwa upande wake, Mkuu wa Wilaya ya Mbeya, Dk Radhi Chuachua amesema eneo hilo linadaiwa kuwepo kwa shughuli za kilimo cha umwagiliaji tangu nchi ipate Uhuru hivyo wanasubiri busara za maamuzi ya Spika wa Bunge.

''Mh Spika huu ni mkutano wako tunasubiri maamuzi yako juu ya eneo hili kama liendele kwa matumizi ya kilimo au la,'' amesema

Kwa upande wake, Mwanasheria wa Skimu hiyo, Shambwee Shitambala na Diwani wa Itezi wamesema mara baada ya agizo la mkuu wa Wilaya wamefuata taratibu za kisheria sambamba na wakulima wa Skimu hiyo kupinga agizo la serikali

''Eneo hili limeanza kulimwa na wazee tangu nchi ipate Uhuru na lina ukubwa wa hekta 120 ambazo zinazalisha mbogamboga, mahindi,maharage,ikiwa ni pamoja na maeneo ya ufugaji ''amesema.

Mwenyekiti wa Skimu hiyo, Maneno Kalembwe amesema kauli za viongozi wa Serikali zinamtengenezea mazingira magumu Mbunge wao, Dk Tulia Ackson katika uchaguzi Mkuu 2025.

''Mh Mbunge sisi ni wapiga kura wako angalia historia ya eneo hili limelimwa kwa miaka zaidi ya 60 sasa leo hii Serikali inatokea wapi kuja kutaka kutuondoa kwa madai eneo hilo ni mali ya Wizara ya Afya.
Vipi kule Loliongo na Ngorongoro? au ndo yale ya morogoro road nyumba zivunjwe lakini Mwanza ziachwe kwa sababu ni wapiga kura?
 
Hivi kati ya DC na mbunge, nani ana mamlaka kubwa zaidi kuliko mwenzake ndani ya wilaya ?
 
Nafikiri spika amenza kampeni kimya kimya!
 
Wamasai walikuwepo pale toka mwaka juzi ausio 😀 😀 wameguswa wapiga kura wako tu unaazna kuliaa utadhani wamebomolewa nyumba wakati ardhi ni ya serikali.. STANDARD za ovyooo kabisaaa
 
Spika Tulia hoyeee!
 
Laana ya kuwadhulumu wamasai inawatafuna mmoja mmoja.

Huko Mbeya ndio wana haki kuliko wamasai Ngorongoro au kwakua wamasai wao hawana mtu mzito kwenye mifumo wa kuwasemea??

Tendeni haki kwa nafasi zenu mlizopewa.
 
Haya maamuzi katoa kama nani?
Hii nchi ni ajabu sana, DC hayuko ktk mhimili anaosimamia spika sasa hapo ndio inakuja tatizo kumpa amri DC
 
Laana ya kuwadhulumu wamasai inawatafuna mmoja mmoja.

Huko Mbeya ndio wana haki kuliko wamasai Ngorongoro au kwakua wamasai wao hawana mtu mzito kwenye mifumo wa kuwasemea??

Tendeni haki kwa nafasi zenu mlizopewa.
Kwa bahati mbaya watanzania bado hatuguswi na matatizo yanayowafika watu ambao hatuna ukaribu nao. Tunajibu kirahisi "hayatuhusu". Yakiwafika wa karibu nasi ndipo tunazinduka.
 
.
Kutokuwepo katiba mstokeo yake ni haya, Tulia ni mbunge na spika wa bunge hana mamlaka nje ya bunge, DC ni mtawala wa wilaya amepewa na rais, anayo mamlaka juu ya mbunge na spika wilayani, kwa DC anayejua mamlaka yake hawezi kutekeleza amri ya mbunge au spika, Tulia amelewa madaraka.
Ni muwakilishi wa wananchi
 
Spika na watu wa hapo waache utoto,mashamba yanafanya nini mjini?

Ndio maana Mbeya inaitwa kijiji kikubwa kwa sababu watu wa huko huwa ni wabishi wajuaji na wasipotaka ustaarabu..

Spika nae anaingia mkenge wa eti mazingira magumu ya mwaka 2025 na kuhalalisha uhuni.
Acha mji upumue. Dunia inakoenda inahitaji sana mashamba mjini kuliko maghorofa ya vioo. Wizara ya afya wanataka kufanyia nini flood plain kama siyo uharibifu wa mazingira.
 
Back
Top Bottom