Spika Tulia apiga 'stop' agizo DC Mbeya

mshale21

JF-Expert Member
Apr 8, 2021
2,049
4,904
Spika wa Bunge la Tanzania, Dk Tulia Ackson amesitisha agizo la Mkuu wa Wilaya ya Mbeya (DC), Dk Rashid Chuachua la kuwataka wakulima zaidi ya 1,700 kupisha eneo lenye ukubwa wa hekta 120 linalotumika kwa kilimo cha umwagiliaji katika Skimu ya Iganjo Bonde la Uyole jijini Mbeya.

Dkt. Tulia ambaye ni Mbunge wa Mbeya Mjini ametoa kauli hiyo leo Alhamisi Julai 21,2022 wakati akizungumza na wakulima wa skimu hiyo siku mbili baada ya mkuu huyo wa wilaya kutoa agizo la kuwataka kuondoka au kuomba kibali cha kuendelea kulima katika eneo hilo ambalo linadaiwa kuwa na mgogoro baina ya wananchi na wizara ya afya.

Dkt. Tulia amesema ameshtushwa na agizo hilo na amelazimika kufika kuona uhalisia na kutoa maamuzi ya kutoondolewa baada ya kukaa na pande zote mbili na kuona uhalali wa eneo na hivyo kuwatia moyo wananchi wawe watulivu wakati wakighulikia kubadili hati ya jina.

''Ndugu zangu hapa hamuondoki kwani eneo lina miaka mingi limetumika kwa kilimo cha umwagiliaji na mababu zetu sasa leo hii limeingia kwenye mgogoro na wizara ya afya nimesema ruksa na muwe watulivu wakati taratibu zinaendelea,'' amesema

Dkt. Tulia amesema, “nimekaa na watu wa pande zote nimejiridhisha na tumekubaliana hapa hamtaondoka na Jiji wataangalia namna ya kutenga eneo kwa ajili ya uwekezaji wa huduma za afya.''

Kwa upande wake, Mkuu wa Wilaya ya Mbeya, Dk Radhi Chuachua amesema eneo hilo linadaiwa kuwepo kwa shughuli za kilimo cha umwagiliaji tangu nchi ipate Uhuru hivyo wanasubiri busara za maamuzi ya Spika wa Bunge.

''Mh Spika huu ni mkutano wako tunasubiri maamuzi yako juu ya eneo hili kama liendele kwa matumizi ya kilimo au la,'' amesema

Kwa upande wake, Mwanasheria wa Skimu hiyo, Shambwee Shitambala na Diwani wa Itezi wamesema mara baada ya agizo la mkuu wa Wilaya wamefuata taratibu za kisheria sambamba na wakulima wa Skimu hiyo kupinga agizo la serikali

''Eneo hili limeanza kulimwa na wazee tangu nchi ipate Uhuru na lina ukubwa wa hekta 120 ambazo zinazalisha mbogamboga, mahindi,maharage,ikiwa ni pamoja na maeneo ya ufugaji ''amesema.

Mwenyekiti wa Skimu hiyo, Maneno Kalembwe amesema kauli za viongozi wa Serikali zinamtengenezea mazingira magumu Mbunge wao, Dk Tulia Ackson katika uchaguzi Mkuu 2025.

''Mh Mbunge sisi ni wapiga kura wako angalia historia ya eneo hili limelimwa kwa miaka zaidi ya 60 sasa leo hii Serikali inatokea wapi kuja kutaka kutuondoa kwa madai eneo hilo ni mali ya Wizara ya Afya.
 
Spika na watu wa hapo waache utoto,mashamba yanafanya nini mjini?

Ndio maana Mbeya inaitwa kijiji kikubwa kwa sababu watu wa huko huwa ni wabishi wajuaji na wasipotaka ustaarabu..

Spika nae anaingia mkenge wa eti mazingira magumu ya mwaka 2025 na kuhalalisha uhuni.
 
Amepinga kama spika au kashauri tu maana sidhani kama maagizi ya DC ni accountable bungeni
 
.
Kutokuwepo katiba mstokeo yake ni haya, Tulia ni mbunge na spika wa bunge hana mamlaka nje ya bunge, DC ni mtawala wa wilaya amepewa na rais, anayo mamlaka juu ya mbunge na spika wilayani, kwa DC anayejua mamlaka yake hawezi kutekeleza amri ya mbunge au spika, Tulia amelewa madaraka.
Kazi ya mbunge ni kutetea wana jimbo wake, hapa ni suala la ubunge na sio uspika,sema waandishi vihiyo ndio wanapotosha.
 
Spika ana madaraka mpaka huko shinani ?...
Yaani ndugu yangu, haya mambo pasua kichwa Tz ....na hapo vilevile ndo unaona umuhimu wa kuwa na Katiba mpya, ambayo itaweza jaribu kurekebisha mikanganyiko kama hiyo ya jurisdiction na mipaka ya uongozi...... kaazi kwelikweli.
.
 
Back
Top Bottom