Spika Sitta Kaweka Heshima ya Nchi? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Spika Sitta Kaweka Heshima ya Nchi?

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Bill, Oct 5, 2009.

 1. Bill

  Bill JF-Expert Member

  #1
  Oct 5, 2009
  Joined: Oct 5, 2007
  Messages: 4,167
  Likes Received: 1,251
  Trophy Points: 280
  Spika Sitta ameweka heshima ya nchi-Raza [​IMG] [​IMG] [​IMG]
  Source : Majira, Monday, 05 October 2009 08:15 Na Tumaini Makene

  MFANYABIASHARA maarufu wa Zanzibar, Bw. Mohamed Raza, ameibuka na kusema kuwa bila Bunge la Tanzania chini ya Spika Samuel Sitta kusimama kidete katika mambo kadhaa yanayoendelea hivi sasa nchini, Watanzania wangekuwa watumwa wa matu wachache wenye pesa.

  Pia katika hali ambayo inaweza kuzua mjadala mkubwa ndani ya CCM na bila shaka nchi nzima, Bw. Raza alisema kuwa haoni sababu ya chama hicho kutoa karipio kwa wabunge ambao wameamua kusimama kidete kupinga ufisadi wala kuunda kamati ya kuwachunguza, akisema hiyo ni kazi bure kwani mambo yanayosumbua yanafahamika.

  Mbali na hilo, Bw. Raza ambaye alisema alivuka bahari jana kuja kuongelea masuala matatu ya kitaifa, hasa katika wakati huu ambapo taifa liko katika maombolezo ya miaka kumi ya kifo cha Baba wa Taifa, Hayati Mwalimu Julius Nyerere, aliwataka watu kadhaa wakiwemo makada wa CCM wanaotuhumiwa kwa ufisadi kupisha katika nyadhifa zao na kukaa pembeni.

  Bw. Raza alisema kuwa kwa sasa Bunge la Tanzania ndio kimbilio cha kilio na uhai wa Watanzania.

  Alisema kwa kusimama kwao kidete kupinga ufisadi na kuikosoa serikali, wabunge wakiongozwa na Sitta wameweka heshima kubwa kwa nchi na walipaswa kupongezwa na kupewa heshima hapa hapa nyumbani, ikibidi kwa kuitisha maandamano nchi nzima.

  "Mheshimiwa Spika kada wa CCM yule na wabunge wanaopinga ufisadi wameweka heshima kwa nchi yetu. Sasa tunashuhudia wanapewa tuzo za heshima na nchi kama Marekani kwa kupinga ufisadi kwa nguvu zote bila kificho, wanapongezwa kwa mapambano yao. Kwa nini tusiwaenzi?" alihoji.

  "Tulipaswa kuandaa maandamano nchi nzima kuwapongeza sio kutoa karipio, karipio la nini ati. Sasa imeundwa kamati ya kuwachunguza, ya kazi gani hiyo. Mbona wanampatia kazi Mzee wa watu Mwinyi bila sababu ya msingi. Masuala yaliyosababisha yote hayo yanafahamika," alisema kada huyo.

  Bw. Raza alikuwa anabeza kazi iliyoundwa kuchunguza mahusiano ya wabunge wa CCM na serikali yao iliyoungwa na Halmashauri Kuu ya taifa (NEC) ya CCM, ikiongozwa na Rais Mstaafu, Ali Hassan Mwinyi na wajumbe wawili, Makamu Mwenyekiti wa CCM (Bara), Pius Msekwa na Spika wa Zamani wa Bunge la Afrika Mashariki, Abdulrahan Kinana.

  Alisema ni wakati mwafaka sasa kwa viongozi kuchukua hatua katika masuala hasa yanayohusiana na ufisadi na uhujumu uchumi yanayoendelea nchini, badala ya kuishia kuunda tume ambazo zinatumia pesa nyingi lakini inapofikia wakati wa kuchukua maamuzi kunakuwepo na kigugumizi.

  "Tume nyingi tu zinaundwa zinatoa taarifa, lakini ikifika pahala pa kutoa maamuzi, watu wanashikwa na mshipi. Sasa kitu cha busara, wale wote ambao wanatuhumiwa kwa ufisadi ni bora wakapisha katika nyadhifa walizonazo. Kuanzia walioko bungeni, ndani ya Kamati Kuu (CC) na Halmashauri Kuu (NEC) wote waondoke.

  "Haiwezekani. Bunge ndicho chombo kinachosimamia serikali. CC na NEC zina nguvu ya kuongoza nchi, kote huko kuna watu wamejaa tuhuma za ufisadi, vyombo hivyo vinapaswa kuwa safi. Wapishe. Kuna watu wana tuhuma nyingi tu, wanaongoza kamati za maadili za chama, wapishe hao wakae pembeni, Mtu mzima akituhumiwa hukaa pembeni yakhe," alisema.

  Alisema kuwa katika kipindi hiki cha miaka kumi bila kuwepo kwa Mwalimu Nyerere, Tanzania inapitia misukosuko ambapo maadili miongoni mwa viongozi na wananchi kwa ujumla yameshuka kwa kiwango cha kutisha.

  Alisema inashangaza kusikia au kuona kiongozi anatembelea wananchi akiwa ndani ya gari la kifahari lakini wananchi wale hawapati huduma za msingi ambazo ziko ndani ya wajibu wa kiongozi huyo.

  "Unajua inashangaza, labda ninyi hamfiki vijijini, mimi nimetembea kote huko Unguja na Pemba, kuna matatizo ya skuli, vituo vya afya, maji, lakini unamuona mkurugenzi wa maji au afya akiwa na gari la mamilioni ya pesa anakwenda kuwatembelea wananchi ambao hawana hata uhakika wa kupata maji au dawa katika vituo vya afya. Watu wanataabika kutafuta maji kilometa kadhaa. Taabu kweli.

  "Mara unasikia shirika limejenga nyumba kwa milioni kama 800 halafu nyumba hiyo itauzwa kwa mkurugenzi kwa milioni chache kama 70 hivi, kwa nini inakuwa hivi. Tunaishia kuunda tume, kama hatuwezi kuchukua maamuzi, basi bora tume hizo zisiundwe," alisema Bw. Raza.

  Huku akikwepa kutaja majina ya watu kama waandishi wa habari walivyokuwa wakitaka katika maswali yao kwake, aliwataka wananchi kutokaa kimya katika masuala ambayo yanafanywa na viongozi na kurudisha maendeleo ya taifa nyuma. Pia aliwataka kuwaunga mkono, ikibidi kuwaombea wale wote, wakiwemo wabunge wanaopinga vita ufisadi.

  Akizungumzia suala la Muungano, Bw. Raza alisema unapaswa kuimarishwa kwa kuzingatia mambo ya msingi kama vile kuridhiana, kuheshimiana, kuvumiliana na kuaminiana.

  Alisema ni suala la ajabu badala ya viongozi kuketi pamoja na kuyazungumza mambo ya muungano, kama walivyokuwa wakifanya waasisi wa Muungano, Mwalimu Nyerere na Hayati Abeid Karume, wamebaki kutoleana kauli ambazo zinatishia mstakabali wa mahusiano baina ya pande zote mbili.

  "Watu wamesikia harufu ya mafuta tu hata hayajapatikana tayari imefanywa kuwa ajenda kubwa. Wanagombea mafuta ambayo hayajapatikana. Na kamwe suluhisho la Muungano haliwezi kuwa serikali moja, huu ulilengwa kwa ajili ya serikali mbili, basi. Tena wengine wanaotoa kauli hizo za ajabu ni makada wa CCM na viongozi wa serikali," alisema.

  Katika suala la vurugu zinazoendelea Tanzania Visiwani , juu ya uandikishaji vitambulisho vya makazi, alisema kuwa kila mmoja anastahili kupata haki hiyo bila kujali itikadi ya kisiasa, rangi, kabila wala dini, ilimradi sheria iliyowekwa kwa mujibu wa katiba imefuatwa.

  Alisema ilikuwa inasikitisha kuona vurugu zikiendelea hata wakati wa Mwezi Mtukufu wa Ramadhani, hivyo akaitaka Tume ya Uchaguzi na mamlaka nyingine husika kuagalia mambo kama hayo wakati mwingine
   
 2. Domenia

  Domenia JF-Expert Member

  #2
  Oct 5, 2009
  Joined: May 26, 2009
  Messages: 462
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  Wapi?
   
 3. Pdidy

  Pdidy JF-Expert Member

  #3
  Oct 5, 2009
  Joined: Nov 22, 2007
  Messages: 33,546
  Likes Received: 5,755
  Trophy Points: 280
  Jamani aweke mara 60???moto wa aliowaonyesha nec inatosha heshima kwake ....
   
 4. Domenia

  Domenia JF-Expert Member

  #4
  Oct 5, 2009
  Joined: May 26, 2009
  Messages: 462
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  Ulikuwepo?
   
Loading...