Spika Sitta agawa matrekta 12 jimboni kwake | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Spika Sitta agawa matrekta 12 jimboni kwake

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Pdidy, Nov 25, 2009.

 1. Pdidy

  Pdidy JF-Expert Member

  #1
  Nov 25, 2009
  Joined: Nov 22, 2007
  Messages: 33,572
  Likes Received: 5,760
  Trophy Points: 280
  Spika Sitta agawa matrekta 12 jimboni kwake

  Na Tausi Mbowe, Urambo Tabora

  SPIKA wa Jamhuri ya Muungano, Samuel Sitta amesema wakati wa malumbano umeisha na sasa ni wakati wa viogozi na wabunge kushirikiana na wananchi katika kuwaletea maendeleo kwa lengo la kupunguza umasikini katika kaya zao.


  Spika Sitta ambaye ni Mbunge wa Urambo Mashariki alisema hayo mjini hapa jana wakati wa hafla ya kuwakabidhi matreta aina ya 'power tiller' kwa ajili ya kilimo katika kata 12 za jimbo hilo yenye thamani ya zaidi ya Sh 100 milioni.


  Akizungumza huku akishangiliwa na umati wa watu, Spika Sitta alisema kazi hiyo ni muhimu katika maisha ya wana Urambo kwa kuwa sasa wanachohitaji ni maendeleo na si suala lingine.


  “Ndugu wana Urambo wenzangu tunaweza kila siku kuzungumza bila mafanikio, wananchi sasa wamechoka na wanachotaka kutoka kwa viongozi wao si maneno tu wanahitaji tuwape maendeleo ili waweze kujikwamua katika lindi la umasikini walionalo na si vinginevyo,”alisema Spika Sitta.


  “Hivi wananchi hata kama tunaweza kujenga barabara, kuboresha miundombinu , lakini bila kipato ni kazi bure,”alisisitiza Spika Sitta huku akishangiliwa na umati huo.


  Kauli ya Mbunge huyo inaweza kuwa mwiba kwa wapinzani wake na baadhi ya viongozi na wabunge ambao kwa siku za hivi karibuni wamekuwa wakilumbana badala ya kufanya kazi waliyotumwa na wananchi waliwachagua.


  Wabunge sasa wamekuwa wakinyoosheana vidole wenyewe kwa wenyewe katika hoja ambazo si za msingi na kufikia kukashifiana huku wengine wakiwatuhumu wenzao kwa kufadhiliwa na kundi la mafisadi katika mambo yao binafsi kama harusi na hata katika kampeni zao za kutafuta nafasi za ubunge.


  Akizungumzaia kuhusu matrekta hayo, Sitta alisema matreta hayo yametolewa kwa ufadhili wa serikali ya Denmark na kwamba yatagaiwa kwa vikundi vya wanawake 38 ambapo vyenye kaya 800 zitakazonufaika kwa awamu ya kwanza ya mradi huo.


  Akifafanua zaidi Sitta alisema, mara baada ya kumalizika kwa awamu ya kwanza, balozi wa Dermak atakuja kukagua mradi huo na endapo ataridhika serikali yake itatoa tena matrekta mengine kwa ajili ya awamu ya pili ambapo zaidi ya kaya 1,600 ikiwa ni mara dufu ya awamu ya kwanza zitanufaika.


  “Kama tunavyojua sasa kipindi cha kilimo cha alizeti kimeisha, nimeagiza matrekta haya yatumike katika shughuli nyingine za maendeleo badala ya kusubiri kilimo cha alizeti na karanga pekee,” aliongeza.


  Alisema matrekta hayo yana uwezo wa kufungwa pampu na pia yana uwezo wa kutumika katika kilimo cha umwagiliaji hivyo kusaidia mpango wa serikali wa kilimo kwanza kwa vitendo.


  Awali, Mwenyekiti wa CCM Wilaya Urambo, Dewji alimpigia debe mbunge huyo na kusema kuwa haoni sababu ya jimbo hilo kuchukuliwa na wapinzani katika uchaguzi ujao kutokana na ukweli kwamba CCM imeweza kujizatiti na kwamba katika uchaguzi huo anauhakikika jimbo hilo watashinda kwa kishindo.


  Dewji alisema hali hiyo imejidhihirisha wazi katika kipindi cha uchaguzi wa serikali za mitaa na vitongoji ambapo CCM iliweza kuibuka kidedea kwa kunyakua viti vyote vya serikali za mitaa na kupoteza kijiji kimoja tu.
   
 2. TIMING

  TIMING JF-Expert Member

  #2
  Nov 25, 2009
  Joined: Apr 12, 2008
  Messages: 21,837
  Likes Received: 125
  Trophy Points: 160
  hongera mh. six, wewe ni mfano wa kuingwa
   
 3. GP

  GP JF-Expert Member

  #3
  Nov 25, 2009
  Joined: Feb 5, 2009
  Messages: 2,073
  Likes Received: 16
  Trophy Points: 135
  khaaaa, yale yale!!!.
  BANDIKO LANGU LIKO WAPI?????.
  aaarrrrgggghhhhhhhhhh.
   
 4. B

  Boramaisha JF-Expert Member

  #4
  Nov 25, 2009
  Joined: Apr 29, 2009
  Messages: 820
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  Naam, Mzee Six bila shaka anakumbuka shule aliyopata siku ile Mwalimu alipowaambia wanafunzi wa Chuo Kikuu walioandamana kupinga kwenda Jeshi la Kujenga Taifa - TANZANIA ITAJENGWA NA WENYE MOYO. Aendelee na moyo huo huo wa kujali maendeleo ya wananchi wa jimbo lake na bila shaka Mwalimu huko aliko akiangalia chini anafurahi, anamsifu na kumpa marks nyingi kwa yote anayofanya ndani ya Bunge, jimboni kwake na nchini mwetu kwa ujumla kwa manufaa ya Watanzania.
   
 5. A

  August JF-Expert Member

  #5
  Nov 25, 2009
  Joined: Jun 18, 2007
  Messages: 4,511
  Likes Received: 724
  Trophy Points: 280
  angalau huyu anachochea maendeleo ya jimbo lake na si kusubiri serikali ya ccm, na si kutoa vitu visivyo na tija, kama hela, chumvi, sukari, kapelo na fulana, sasa kinacho fuatia muanzishe Tanesco yenu hapo Urambo, watoto wenu waweze kusoma Vizuri, na serikali ikitoa fedha za Madarasa bila ceiling board muweke wenyewe msiisubiri serikali ya CCM,
   
Loading...