Uchaguzi 2020 Spika Ndugai: Wabunge wa CHADEMA (Viti Maalum) wasipohudhuria mikutano mitatu wamejifukuzisha

idawa

JF-Expert Member
Jan 20, 2012
25,284
38,312
Spika wa Bunge Job Ndugai amesema kwa mujibu wa Katiba na Kanuni za Bunge, wabunge 19 wa viti maalumu kutoka CHADEMA endapo hawatohudhuria mikutano mitatu ya Bunge, watakuwa wamejifukuzisha ubunge wenyewe.

Spika Ndugai amesema mkutano wa kwanza ni huu wa pili Januari na wa tatu Aprili.

My take.
Toka Sasa hadi April ni mbali sana, tutashudia vituko na mgawanyiko mkubwa Sana hapa katikati...huu ni mtihani mwingine ndani ya CHADEMA.

==================================

SPIKA wa Bunge, Job Ndugai amebainisha kuwa kwa mujibu wa Katiba na Kanuni za Bunge, wabunge 19 wa Viti Maalumu kutoka Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), endapo hawatohudhuria mikutano mitatu ya Bunge, watakuwa wamejifukuzisha ubunge.

Hadi jana si Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) au Bunge hilo, walikuwa wamepokea majina ya wabunge hao 19 kutoka chama hicho cha upinzani. Akizungumza na Televisheni ya Azam jijini Dodoma juzi, Ndugai alikiri kuwa kwa mujibu wa hesabu za haraka, Chadema yenye mbunge mmoja wa jimbo, inatarajiwa kuwa na wabunge wanawake wasiozidi 19.

“Nafasi hizo ni zao ni jukumu lao kuwaruhusu wanachama wao. Pia wakiamua kugoma basi hakuna tatizo hata kidogo. Hakuna athari yoyote zaidi ya wao kupoteza nafasi ambayo Katiba imetoa kwa akinamama hao kuja bungeni kuwasemea Watanzania,” alieleza Spika Ndugai.

Alisema mtu yeyote akishakuwa mbunge haijalishi anatoka chama gani kwani anapokuwa ndani ya chombo hicho cha kutunga sheria huwasemea Watanzania.

Kuhusu ukomo na muda wa chama hicho kuwasilisha majina ya wabunge hao, Spika Ndugai alisema mtu asipohudhuria mikutano ya Bunge mitatu anakuwa amejifukuza wenyewe.

“Kwa hawa wa Viti Maalumu Chadema, mkutano huu wa kwanza unaoendelea ni wa kwanza, wa Januari ni wa pili na wa Aprili ni wa mwisho kama hawatohudhuria watakuwa wamejifukuza wenyewe kwa mujibu wa Katiba,” alieleza.

Akielezea utaratibu wa uundwaji wa Kambi ya Upinzani kwa Bunge hilo ambalo kwa sasa zaidi ya 90 ni wabunge wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), alisema kambi ya upinzani ni fursa inayotolewa kutokana na idadi fulani au vyama vya upinzani kuungana.

Alisema inapoundwa kambi ya upinzani, hupewa fursa ikiwemo kiongozi wao kupewa nafasi ya pekee ya kuuliza maswali wa kwanza katika kipindi cha maswali kwa Waziri Mkuu au anaposimama tu bungeni hupewa fursa ya kuzungumza.

“Lakini sasa kutokana na uchache wao haki hii wataikosa ila watashiriki kama wabunge wengine wa kawaida,” alifafanua Ndagai ambaye juzi alichaguliwa tena kuongoza Bunge la 12 akiwa pia na wadhifa huo katika Bunge la 11.

Kwa upande wake, Mkurugenzi wa Uchaguzi wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC), Dk Wilson Mahera alisema hadi jana ofisi yake ilikuwa haijapokea majina ya wabunge wa Viti Maalumu wa Chadema.

“Hata hivyo, niliongea na Katibu Mkuu wa Chadema (John Mnyika), aliniambia wanaendelea na vikao na wakishakamilisha atanikabidhi yeye mwenyewe majina hayo,” alieleza Dk Mahera.

Hata hivyo, alisikitishwa na kitendo cha gazeti moja linalotoka kila siku (si HabariLEO) kwa kitendo chake cha kumnukuu vibaya na kudai kuwa amepokea majina ya wabunge hao wa Chadema na kuyawasilisha bungeni.

“Kwa kweli wameniharibia, wameandika uongo, wanafanya nifikirie zaidi kushirikiana na waandishi wa habari,” alieleza kwa masikitiko.
 
Mh Ndugai hebu endesha Bunge, mambo ya CHADEMA waachie wao, we si ndo ulisema kunahitajika sijui idadi gani ili muamue Mambo yenu, sasa idadi imekamilika, na kuzidi, wananchi na chama hawaleti wabunge na huyo sijui mbunge wa wapi, CHADEMA itamtimua very soon, ongoza bunge mheshimiwa sana
 
Wabunge wapi hao?
Maajabu hayaishi Tanzania!

Si yeye mwenyewe Ndugai alinukuliwa na vyombo vya habari kuwa kutokana na matokeo ya uchaguzi mkuu uliopita, ambapo CHADEMA imeambulia mbunge mmoja pekee, hakutakuwa na kambi rasmi ya upinzani?

Sasa tunapomsikia tena Ndugai akidai kuwa wabunge Wa CHADEMA wasipohudhuria mikutano mitatu mfululizo, watakuwa wamejifukuzisha ubunge, je anawaongelea wabunge wapi hapo?
 
Spika wa Bunge Job Ndugai amesema wabunge wa Chadema wasipohudhuria mikutano mitatu ya bunge watakuwa wamejifukuzisha ubunge...
Nawewe acha upashkuna. Nataka awataje hao wabunge wa viti maalum wa CHADEMA ambao hawapo bungeni. Na atasemaje ni wabunge wakati hajawaapisha? Mbona wanatubemenda akili hawa CCM? Au anadhani na sisi wananchi ambao wanatuita wanyonge tumeshikiwa akili zetu na Magufuli kama wao/yeye? Period!
 
Spika wa Bunge Job Ndugai amesema wabunge wa Chadema wasipohudhuria mikutano mitatu ya bunge watakuwa wamejifukuzisha ubunge.

Ndugai amesema mkutano wa wa kwanza ni huu wa pili January na wa tatu April.

My take.
Toka Sasa hadi April ni mbali sana, tutashudia vituko na mgawanyiko mkubwa Sana hapa katika...huu ni mtihani mwingine ndani ya Chadema.
Watajuta kumtukana Dr. Slaa
 
Back
Top Bottom