Spika Ndugai na Bunge lake hawana taarifa ya kifo cha Ndesamburo?

Leo video imekuwa shahidi, lakini video iliyomuonesha Bashite wakati anavamia Cloud Media haikuwa shahidi.

Hizi chuki wanazozionesha dhahiri ni ndogo sana kuliko zilizopo kwenye Mioyo yao
 
Pohamba,
Tanzania belongs to all Tanzanias! Hii nchi si ya CCM wala ya Magufuli ni yetu sote! Kilichofanyika Bungeni ni double standards! Mbona siku ile Ndugai alipoitwa 'Fwaala' alimtambua Mbunge aliyemwita hivo? Iweje Mbunge aliyemwita Mnyika 'Mwizi'
hakutambuliwa kwa madai ati Spika hana masikio mia moja ya kusikia kila kitu? Kama hawezi kusikia,kuona na kuchukua hatua kumbe kazi yake nini anapokuwa amekaa kwenye kiti???

Ila ameweza kuwasikia wabunge wakimteta nje ya Bunge.
 
Leo video imekuwa shahidi, lakini video iliyomuonesha Bashite wakati anavamia Cloud Media haikuwa shahidi.

Hizi chuki wanazozionesha dhahiri ni ndogo .sana kuliko zilizopo kwenye Mioyo yao

Video waliyoedit au kutokusikika kwa sauti ya Kulima Shonza akimtukana Mnyika ni ajabu na kweli.
 
Mle bungeni kuna mtu alitamka neno "fala"....mbona kilinuka.
Ila alipokuja mwenzetu kutamwaka neno " mwizi tukapotezea.

Hiyo ni hoja ya msingi sana na kila mpenda Haki na Demokrasia katika nji hii ameliona hilo! Mengine yote ni Unafiki, Ubabaishaji na Chuki dhidi ya CHADEMA!
 
Thinktz01,
Unayosema ni kweli tatizo ni mfumo uliooza chini ya Utawala wa CCM! Job Ndugai hakustahili hata kwa nukta kuwa Spika wa Bunge la Tanzania. Hana sifa,hana busara, hana hikma lakini pia huyu jamaa ana ugonjwa wa sonono!
Kama Spika ameshindwa kuheshimu na au kuthamini uhai na michango ya Mbunge mstahafu aliyetutoka Marehemu Philemon Ndesamburo basi Taifa hili linaongozwa na vihiyo wasiojua wajibu na mipaka yao ya kazi!!!
Hawawezi kumuenzi kwani alichowafanyia Moshi kinawatesa hadi hawapati usingizi. N.a. sidhani kama ktk miongo ya karibuni wataambulia kitu.
 
Ila na sisi watanzania tukome kuchaguwa wabunge watokanao na chama kubwa. Angalia sasa, unashindwa kuelewa kama pale ni mjengoni au ni Sokoni Kariakoo.
 
Yale yaliyotokea Bungeni leo katika azimio la kuwafukuza Wabunge wa upinzani toka CHADEMA Bi Halima Mdee na Bi Esther Amos Bulaya ni kuonyesha kwamba Bunge chini ya Ndugai hawajui kama CHADEMA wana msiba mkubwa wa mwasisi wa chama chao Mbunge mstahafu ndugu Philemon Ndesamburo!

Hii imedhihirisha kuwa CCM wanawachukia wapinzani hasa CHADEMA na wanatamani hata leo hii Wabunge wote wa CHADEMA wapukutike wote!
Haiwezekani Kamati ya Haki na Maadili ya Bunge itoe mapendekezo ya adhabu hii kwa Wabunge hawa 2 walioko kwenye msiba huu mkubwa?

Nimesikiliza mapendekezo ya Kamati iliyoungwa mkono na asilimia kubwa ya Wabunge wa CCM! Inasikitisha kwamba Spika Ndugai na Mwenyekiti wa Kamati Mzee George Mkuchika hawakugusia chanzo cha tatizo lililopelekea vurugu hizo! Mbunge wa CCM aliwasha mic na kusema MNYIKA MWIZI,lakini si Spika wala Mkuchika aliyeonyesha juhudi za kumsaka huyo Mbunge wa CCM aliyeropoka hayo maneno! Spika anasema hawezi kuwa na masikio 100 ya kusikia kila Mbunge anachosema!!!Huu ni uongo wa Ndugai na ameonysha double standard, maana hayo maneo yangelisemwa na Mbungevwa upinzani leo asingelikuwa Bungeni! Mwenyekiti anadai kuwa swala la kujua chanzo au Mbunge aliyemwita Mnyika Mwizi haikuwepo kwenye hadidu za rejea!! This is rubbish! Kamati inasema iliangalia mkada wa video ili kujiridhisha kwa makosa ya hao Wabunge,inashangaza kuwa Kamati haikuona yote yaliyotamkwa na kichaa wao Lusinde na huyo aliyemwita Mnyika mwizi!!
Namaliza kwa kushauri Bulaya na Mdee waende Mahakamani maana haiwezekani Bunge liwe ni kila kitu! Kama Polisi wanakamata Mbunge na kumsweka Rimande na kushtakiwa Mahakamani iweje Mbunge akienda kulalamika Mahakamani aambiwe Mahakama haina mamlaka hayo??
Je, hivi leo ikitokea Mbunge akapigwa na Mbunge mwenzake wakiwa ndani Bunge akapoteza uhai, Bunge kwa kutumia Kamati ya Haki na Maadili ya Bunge wana uwezo wa kusikiliza murder au manslauter case??
Mdee,Bulaya na Mnyika tafuteni Haki yenu Mahakamani, Bunge is not a final judiciary machinery!!!
Kamati ya Mkuchika huwa ni kamati katili yenye watu wenye roho mbaya za kichawi kwanza mkuchika mwenyewe ni wale wa kujua kusoma na kuandika hana vyeti na kama asingekuwa Mbunge leo kule mtwara angekuwa sangoma mchawi ni kizee kibaya sana kwa Ustawi wa chadema mda mwingi kinatamani wabunge wa chadema wapande ndege moja kisha ianguke wafe kama ile timu ya Zambia.
 
Thinktz01,
Unayosema ni kweli tatizo ni mfumo uliooza chini ya Utawala wa CCM! Job Ndugai hakustahili hata kwa nukta kuwa Spika wa Bunge la Tanzania. Hana sifa,hana busara, hana hikma lakini pia huyu jamaa ana ugonjwa wa sonono!
Kama Spika ameshindwa kuheshimu na au kuthamini uhai na michango ya Mbunge mstahafu aliyetutoka Marehemu Philemon Ndesamburo basi Taifa hili linaongozwa na vihiyo wasiojua wajibu na mipaka yao ya kazi!!!
Bila hata kumjali mbunge mwenzao Lucy ambaye ni mtoto wa marehemu mzee P.Ndesamburo.
 
kwani Ndesamburo ni nani katika taifa hili labda?

...Ni mtanzania mwenzetu, ametangulia mbele za haki kwa kuwa kila nafsi kwa hakika itaonja mauti. Tofauti yake na wewe ni kwamba yeye kaacha legacy na ndiyo maana amezikwa na maelfu ya watu na media zote zilikuwa kule Majengo Moshi; je na wewe utakumbukwa kwa lini???
 
Binge lina lengo la kuinufaisha ccm na kumfurahisha Mtakavitu. Haina habari na Watanzania
 
Back
Top Bottom