Petro E. Mselewa
JF-Expert Member
- Dec 27, 2012
- 10,197
- 25,517
Kwa kauli yake mwenyewe aliyoitoa kupitia Sauti ya Amerika almaarufu kama VoA, Mbunge Tundu A.M. Lissu bado anaendelea na matibabu na hivyo bado ni mgonjwa. Lissu amesema kuwa mnamo tarehe 20/2/2018 takribani majuma mawili yajayo atakuwa nchini Ubelgiji kwa upasuaji wa 23 mwilini mwake.
Kama ni taarifa kuhusu matibabu na maendeleo yake, Lissu ameitoa jana mbele ya Balozi Wilson Masilingi aliyekuwapo studioni na kushiriki mazungumzo ya jana. Kama hoja ya kiti cha Spika ni kutopata taarifa ya aliko, anachofanya na matibabu ya Lissu kwa ujumla, Lissu ameweka jambo hilo wazi jana. Kufanyiwa tena upasuaji kunamaanisha kuwa Lissu anaendelea na matibabu.
Kuhusu kurudi nyumbani Tanzania, alipoulizwa Lissu akasema kuwa pale ambapo madaktari wake watamwambia yuko vyema, atarudi. Kwakuwa anakwenda kufanyiwa upasuaji mwingine, Lissu bado ni mpokea matibabu na ataendelea kuwa karibu na hospitali na madaktari wake. Kama raia mwema wa Taifa hili, na kufuatia taarifa aliyoitoa Lissu kuhusu upasuaji, naomba mshahara wake usisimamishwe ili umsaidie.