Spika Ndugai: Lissu asubiri Muziki wangu

Ndugai kuwa na Moyo wa ubinadamu,mwenzako kapigwa risasi zile,binge na serikali yako wameshindwa hata kumtibu,kibaya zaidi unamtishia,jitahidi kujizuia hautapata hasara,kumbuka Mungu ndie atoae vyeo hivi,usijivune,kumbuka Leo upo uspika na ubunge ila kesho yake huijui.muogope Mungu jamani,msiwe wepesi kukufuru.
 
Huyu ni msemaji wa Simba Sports Club au Spika wa Bunge? Wanaamini wapo juu ya sheria na katiba, huu sio ufalme, hakuna mchezaji au mchezesha muziki, tuna katiba. Let's see
 
Mara wasiojulikana wanajulikana halafu raisi anamualika ikulu kwenye hard talk. Unajua mpaka sasa hajasema ni raisi!? Anasema ni serikali ya raisi. Sasa serikali ni taasisi kubwa. Yoyote yule anaweza kuwa muhusika. Na siasa ni siasa.
 
Hii ni Katika ule muendelezo wa kauli ya Spika kumtaka lissu arejee nchini kutokana na kwamba hana kibali cha kuishi nje ya nchi,la sivyo atajikuta yupo nje ya uwanja.sasa hivi spika anasema "Lissu asubiri muziki wangu" huku TL naye akijibu mapigo "usijaribu kuuzima moto kwa petroli,utapotea"
Je,nini kitatokea Lissu ataucheza muziki wa Spika au Ndugai atapotea kwa moto wa petroli wa TL? usikose toleo lijalo....
View attachment 1001634
Mzee wa bakora anataka amtwange mbunge wake bakora!
 
Kweli nimeamini kabisa pasi na shaka kuwa huyu si spika wa bunge na wananchi kwa ujumla Bali ni spika wa mtu fulani kwa makusudi ya kujilinda na pia kuficha ukweli mchungu juu ya utawala wake.
Haiwezekani spika akawa mtu WA kupambana na wabunge, kwanza wale tu wanaoonyesha kupingana ama kutokukubaliana na baadhi ya mambo ndani ya serikali, badala ya kuacha serikali yenyewe ijitetee kwa hoja ndani ya bunge, huku spika akiwa msimamizi wa vikao tu, na zaidi ya yote akionyesha kuwa upande wa wabunge na si upande wa serikali. Sasa nani ataisimamia, kuishauri na haya kuipinga serikali pale inapobidi kama bunge lote pamoja na spika wake watakuwa watu WA kusema "ndiyoooo" kwa kila lifanywalo au liletwalo bungeni na serikali?.....zaidi ya 1.5t na mambo mengine ndo yanapotezewa kwa gharama yeyote hapo.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hii ni Katika ule muendelezo wa kauli ya Spika kumtaka lissu arejee nchini kutokana na kwamba hana kibali cha kuishi nje ya nchi,la sivyo atajikuta yupo nje ya uwanja.sasa hivi spika anasema "Lissu asubiri muziki wangu" huku TL naye akijibu mapigo "usijaribu kuuzima moto kwa petroli,utapotea"
Je,nini kitatokea Lissu ataucheza muziki wa Spika au Ndugai atapotea kwa moto wa petroli wa TL? usikose toleo lijalo....
View attachment 1001634
Huyu Ndugai sasa akaimbe taarabu!
 
Lissu hawezi kufikia uwezo wa Kujieleza wa Sultan Seif Sharif Hamad

Lissu hawezi kufikia umaarufu wa Sultan Seif kimataifa

Lissu hawezi Kuwa Na Wafuasi wengi wa kufikia Sultan Seif

Lakin Sultan Seif kaanza kuzunguka kimataifa kwa robo karne (1992-2017) akichafua Taifa Kwenye macho ya Mabeberu
Kama kuna kitu kafanikiwa Sana Basi Ni mambo Mawili tu

1) Kumaliza soli Za Viatu

2) kUjaza mihuri Kwenye hati yake ya kusafiria
Hati ya kusafiria ilikua inakaa miaka 5, ila baada ya 2006 ikawa inakaa miaka 10 sasa anajaza vipi mihuri wakati amebadili hati ya kusafiria mara nyingi?
 
Hii ni Katika ule muendelezo wa kauli ya Spika kumtaka lissu arejee nchini kutokana na kwamba hana kibali cha kuishi nje ya nchi,la sivyo atajikuta yupo nje ya uwanja.sasa hivi spika anasema "Lissu asubiri muziki wangu" huku TL naye akijibu mapigo "usijaribu kuuzima moto kwa petroli,utapotea"
Je,nini kitatokea Lissu ataucheza muziki wa Spika au Ndugai atapotea kwa moto wa petroli wa TL? usikose toleo lijalo....
View attachment 1001634

Circumstantial evidences zinazidi kujidhihiri.

Hasira zote za nini?. Bunge lina medical reports kwamba kapona?. TAL ameondoka jana au mwezi juzi kwenda ulaya bila kibali cha bunge?. Kwa nini sasa?.

Mbona Mh wa kutwanga fimbo amekaa India kiroho safi kwa muda mrefu hadi kupona ndio kageuza?. Acha gubu wenzio watibiwe wapone. Wivu wa nini?

Kama hapo awali bunge lilimpa kibali cha kutibiwa huko nje na si kuzurura/ kuongea na medias kama wanavyodai why hawakumtibu?. Madai ya sasa yanaletwa na nini?.

Huko nje Lissu kama nini kipya ambacho hakijasemwa na wengine hata hasira ziwe kubwa hivi?.

Vitu vingine ni vya kupuuzia, tunazidi kujidhalilisha. Ingekuwa nafuu kutoongelea wala kutoa comments kuhusu safari yake hii.

Kujiingiza kwenye mjadala huu ni ushahidi mwingine, ni gubu, ni umbumbu na ufala.

Ni wivu wa kiingereza kizuri alichoongea huko, najua wengi wa upande mwingine Lugha ni tatizo sana.
Hata akinyanganywa ubunge ataishi tu. Tutaendea kumpenda na kumkubali tu.

Kama aliishi kwa kunyimwa haki ya kutibiwa, basi ubunge si kitu ataishi tu. Hata hvyo , wangapi mmewazulumu ubunge na wanaishi tu vizuri?.

TAL the great, mioyoni mwetu ataishi daima.
 
Ninaona viongozi wote wa Serikali ya Magufuli inahaha namna ya kumdhibiti Mh.Tundu Lissu! Niliwahi kusema, Damu ya Mh.Lissu itaw, atafuna kila mmoja kwa namna yake ya kipekee.

Mungu ni mwenye Nguvu, amekwisha ulaani utawala huu wa Kigaidi, ssa mambo hayaendi! Viongozi wamebaki wakibwata bila weledi wowote. Tundu Lissu ni sauti iliayo nyikani, itawasambaratisha vikali!
Ni aina gani ya uongozi inayoamini ktk kuteka, kutesa na kuua wananchi wasiyo na hatia!?
 
mbaya zaidi hawamuwezi mahakamani wala mjengoni,wanamuweza kwa pyu pyu pyu(kwa sauti ya Sugu)
 
Huyu jamaa ni mgonjwa ukiangalia tu utajua!
Screenshot_20190122-103524.jpeg

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom