Spika Ndugai awe Muungwana, ajiweke pembeni

kavulata

JF-Expert Member
Aug 2, 2012
12,301
12,600
Imani huzaa Imani na hofu huzaa hofu.

Kwasasa Rais hana Imani tena na Spika, ana hofu na Spika na kundi lake ambalo hajui wako wangapi, ni akina nani, wako wapi na wanapanga nini na nini lini na wapi dhidi yake. Hofu hii imesababishwa na mtu mzito sana kwenye nchi anaepigiwa salute na vyombo vya ulinzi na usalama nchini. Kwavyovyote vile Mh. Spika hayuko peke yake kwenye agenda yake na sio kweli kwamba hakujua matokeo ya kuyasema Yale hadharani mbele ya kamera. Waswahili wanasema anaekumulika mchana usiku anakuchoma.

Chondechote Mh. Spika inawezekana unayo hoja ya msingi sana unayoifahamu kuhusu mihimili mingine ambayo inakwenda kuidhuru Tanzania au Tanganyika huko mbeleni lakini ulivyoiwasilisha inakinzana na Katiba yetu na mila na desturi ya CCM na watanzania. Katiba yetu ambayo wote mnaifahamu na kuapa kuilimda imempa mama Samia urais kamili wa Tanzania kama vile ilivyompa JPM urais bila yeye mwenyewe kutarajia. Na katiba yetu imempa Rais nguvu nyingi na kubwa sana za kutenda anazoweza kuzitumia atakavyo bila kuhojiwa na chombo chochote nchini. Nguvu hizi za Rais kikatiba na Chama ndizo zinazosababisha mtafaruku mkubwa kwa kile alichokifanya Mh.spika, kila mtu anamshangaa kwa alichosema na kuhoji kwakuwa sio Cha kawaida kufanywa na Spika wa Chama kimoja na Rais hadharani. Kama kingefanywa na wapinzani isingekuwa hoja yoyote Ile.

Rais wetu ni mgeni, mzanzibar na mwanamke, hivyo inaweza kumuwia vigumu kujua kama spika amefanya yote haya kwa sababu yeye ni mgeni, mzanzibar au ni mwanamke? Hapa umekisea sana sana sana. Angekuwa Mimi ndiyo Rais Samia makazi yangu rasmi yangekuwa Ikulu ya Dar es salaam zaidi kumuepuka mh.spika.

Kulinda heshima ya Spika na nia njema yake ni heri apishe kiti Cha spika ili Tanzania isonge mbele, Tanzania ni kubwa kuliko mtu mmojammoja, kama Rais na Spika hawaaminiani wataendeshaje nchi?

Mh. Spika kama angekuwa madhubuti na nia njema kwa taifa na Rais angeyasema Yale kwenye vikao vya bunge, vikao vya Chama au angeomba audience na Rais kuzungumza yale.

Kaa pembeni ulinde hadhi yako
 
Huyo mamayenu Sio Mungu na Tanzania Sio mali yake
Spika Naye Anahaki yakutoa maoni yake
hana kosa lolote
 
Back
Top Bottom