makufuli
JF-Expert Member
- Jun 18, 2016
- 426
- 253
Unamaana wanaovuliwa wamekataa kuburuzwa ndani ya vyama vya upinzani,na kimsingi kuna usultani ndani ya vyama vya upinzaniCCM watawavuwaje uanachama wabunge wake wakati wabunge hao wamekubali kuburuzwa na kukubaliana na kila matakwa ya wakubwa wao? Badala ya kuwalaumu wapinzani Ndugai ambaye ni Spika wa Bunge, aliongoze Bunge kubadili Kifungu kidogo (1) kifungu (b) kwenye Ibara ya 67 ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano na Kifungu kidogo (1) Kifungu (f) cha Ibara ya 71 vinavyolazimisha wabunge watokane na vyama vya siasa na vyama vya siasa kupewa madaraka ya kumnyang'anya ubunge mtu kupitia kumtoa kwenye chama chao cha siasa.
Tatizo siyo vyama vya siasa bali katiba iliyovipa vyama vya siasa uungu wa kuumba na kuua ubunge wa mtu anayepingana na chama husika cha siasa!!