Spika Ndugai awaonya upinzani wasifukuze wabunge, awataka wajifunze kutoka CCM!

Wakudadavuwa

JF-Expert Member
Feb 17, 2016
16,388
2,000
Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano Jana aliwaonya viongozi wa vyama vya upinzani waache tabia yao ya usultani kufukuza uanachama wabunge wanaotofaitiana nao. Amesema hayo huku akiwakumbusha Mbunge ni mwakilishi wa wananchi na kama akifukuzwa uanachama basi atapoteza sifa ya kuwa mbunge na kuwakosesha uwakilishi wananchi.

Amewaasa wajifunzi kutoka Chama Cha Mapinduzi (CCM) jinsi wanavyoshughulikia nidhamu za wabunge wao ambao wanaenda kinyume na maamuzi ya chama. Ni CCM pekee ambayo haijawahi kumvua mbunge uanachama kwa kutofautiana na Uongozi. Hivi majuzi CUF imewafutia uanachama wabunge wake Sakaya na Maftah,katika Bunge lililopita Hqamad Rashid alifutwa uanachama akaelekea mahakamani, CHADEMA walimfukuza Zitto Kabwe na NCCR-Mageuzi walimfutia uanachama David Kafulila kabla ya kufanya usuluhishi.

Ndugai katoa somo na kwa tabia hii ni dhahiri viongozi wa vyama vya upinzani hawataki kukosolewa,wanakumbatia usultani na ufalme.
 
Allen Kilewella

Verified Member
Sep 30, 2011
13,654
2,000
CCM watawavuwaje uanachama wabunge wake wakati wabunge hao wamekubali kuburuzwa na kukubaliana na kila matakwa ya wakubwa wao? Badala ya kuwalaumu wapinzani Ndugai ambaye ni Spika wa Bunge, aliongoze Bunge kubadili Kifungu kidogo (1) kifungu (b) kwenye Ibara ya 67 ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano na Kifungu kidogo (1) Kifungu (f) cha Ibara ya 71 vinavyolazimisha wabunge watokane na vyama vya siasa na vyama vya siasa kupewa madaraka ya kumnyang'anya ubunge mtu kupitia kumtoa kwenye chama chao cha siasa.

Tatizo siyo vyama vya siasa bali katiba iliyovipa vyama vya siasa uungu wa kuumba na kuua ubunge wa mtu anayepingana na chama husika cha siasa!!
 
Wakudadavuwa

JF-Expert Member
Feb 17, 2016
16,388
2,000
CCM watawavuwaje uanachama wabunge wake wakati wabunge hao wamekubali kuburuzwa na kukubaliana na kila matakwa ya wakubwa wao? Badala ya kuwalaumu wapinzani Ndugai ambaye ni Spika wa Bunge, aliongoze Bunge kubadili Kifungu kidogo (1) kifungu (b) kwenye Ibara ya 67 ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano na Kifungu kidogo (1) Kifungu (f) cha Ibara ya 71 vinavyolazimisha wabunge watokane na vyama vya siasa na vyama vya siasa kupewa madaraka ya kumnyang'anya ubunge mtu kupitia kumtoa kwenye chama chao cha siasa.

Tatizo siyo vyama vya siasa bali katiba iliyovipa vyama vya siasa uungu wa kuumba na kuua ubunge mtu anayepingana na chama husika cha siasa!!
Kwanini umfukuze mbunge kwa kutofautiano mtazamo na uongozi?...ni lazima kuwe na tofauti hata kwenye chama haiwezekani eti leo Mbunge wa chadema akiongea tofauti na chama aitwe 'msaliti'... na chama kinamfukuza.
 
Allen Kilewella

Verified Member
Sep 30, 2011
13,654
2,000
Kwanini umfukuze mbunge kwa kutofautiano mtazamo na uongozi?...ni lazima kuwe na tofauti hata kwenye chama haiwezekani eti leo Mbunge wa chadema akiongea tofauti na chama aitwe 'msaliti'... na chama kinamfukuza.
Wewe una mtizamo gani kuhusu UKUTA. Unafikri yale mawazo ya kupambana na UKUTA kwa nguvu ile kama wale jamaa wa UKUTA wangekuwa ni CCM si wangeshafukuzwa chama. Kuvumiliana kusiwe ndani ya chama peke yake hata kwenye chama kilichoko madarakani dhidi ya vyama vingine.
 
Danthedon

Member
Feb 29, 2016
84
125
Kwanini umfukuze mbunge kwa kutofautiano mtazamo na uongozi?...ni lazima kuwe na tofauti hata kwenye chama haiwezekani eti leo Mbunge wa chadema akiongea tofauti na chama aitwe 'msaliti'... na chama kinamfukuza.
Kama hujui, ccm ndio mabingwa wa kuingiza mamluki kwenye vyama vya upinzani ili kuleta migogoro na kuvisambaratisha. Sasa kusipokuwa na nguvu ya uongozi kuwaondoa ujue ndio mwisho wa vyama pinzani Tanzania.
 
Easyway

JF-Expert Member
Oct 5, 2012
2,606
2,000
Kuna udikteta mkubwa sana kwenye vyama vya upinzani kuliko hata huo wanaouita udikteta uchwara.

Vyama vya upinzani vina wenyeviti na makatibu wakuu wa kudumu kama Mbowe. Mrema,Cheyo,maalim Seif, Mbatia nk.
Ukikosana na mwenye chama lazima ufukuzwe hakuna Uhuru wa maoni wala demokrasia.
 
Wakudadavuwa

JF-Expert Member
Feb 17, 2016
16,388
2,000
Wewe una mtizamo gani kuhusu UKUTA. Unafikri yale mawazo ya kupambana na UKUTA kwa nguvu ile kama wale jamaa wa UKUTA wangekuwa ni CCM si wangeshafukuzwa chama. Kuvumiliana kusiwe ndani ya chama peke yake hata kwenye chama kilichoko madarakani dhidi ya vyama vingine.
Ukuta ni usanii kijana! ukuta haujawahi kuwa hitaji la wananchi,kama siku wananchi wakidai mambo yao hakuna wa kuwazuia na wala hawahitaji kiongozi yeyote wa siasa kuwaongoza. maandamano ya wananchi hayaongozwi na viongozi wa vyama vya siasa. Hata hivyo jikite kwenye suala la fukuza fukuza vyama vya upinzani.
 
Wakudadavuwa

JF-Expert Member
Feb 17, 2016
16,388
2,000
Kama hujui, ccm ndio mabingwa wa kuingiza mamluki kwenye vyama vya upinzani ili kuleta migogoro na kuvisambaratisha. Sasa kusipokuwa na nguvu ya uongozi kuwaondoa ujue ndio mwisho wa vyama pinzani Tanzania.
Kwa hiyo Lowassa,Sumaye,Kingunge ni mamluki?
 
jogi

JF-Expert Member
Sep 25, 2010
25,602
2,000
Mkuu unanikumbusha Hayati Alhaji Aboud Jumbe Mwinyi, ccm walimfanyia kitu mbaya enzi za uhai wake!!!! Naamini nawe unakumbuka. Sijui walitofautiana nini!!!! lakini Udicteta ccm waliomfanyia Jumbe hata shetani anaendelea kulaani.

Kuna udikteta mkubwa sana kwenye vyama vya upinzani kuliko hata huo wanaouita udikteta uchwara.

Vyama vya upinzani vina wenyeviti na makatibu wakuu wa kudumu kama Mbowe. Mrema,Cheyo,maalim Seif, Mbatia nk.
Ukikosana na mwenye chama lazima ufukuzwe hakuna Uhuru wa maoni wala demokrasia.
 
CHUAKACHARA

JF-Expert Member
Jun 3, 2011
12,362
2,000
Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano Jana aliwaonya viongozi wa vyama vya upinzani waache tabia yao ya usultani kufukuza uanachama wabunge wanaotofaitiana nao. Amesema hayo huku akiwakumbusha Mbunge ni mwakilishi wa wananchi na kama akifukuzwa uanachama basi atapoteza sifa ya kuwa mbunge na kuwakosesha uwakilishi wananchi.

Amewaasa wajifunzi kutoka Chama Cha Mapinduzi (CCM) jinsi wanavyoshughulikia nidhamu za wabunge wao ambao wanaenda kinyume na maamuzi ya chama. Ni CCM pekee ambayo haijawahi kumvua mbunge uanachama kwa kutofautiana na Uongozi. Hivi majuzi CUF imewafutia uanachama wabunge wake Sakaya na Maftah,katika Bunge lililopita Hqamad Rashid alifutwa uanachama akaelekea mahakamani, CHADEMA walimfukuza Zitto Kabwe na NCCR-Mageuzi walimfutia uanachama David Kafulila kabla ya kufanya usuluhishi.

Ndugai katoa somo na kwa tabia hii ni dhahiri viongozi wa vyama vya upinzani hawataki kukosolewa,wanakumbatia usultani na ufalme.
Zito alikuwa msaliti! Hilo ni kosa kubwa! Ni kama kupindia nchi! Alitaka kumpindua Mbowe. Ya sakaya yanasameheka maana yeye anampenda lipumba, siyo kosa!
 
esitena tetena

JF-Expert Member
Aug 21, 2015
1,751
2,000
rekebisha heading yako. Spika "hakuwaonya" vyama vya upinzani bali ametoa ushauri wake. hawezi "kuwaonya" maana hana mamlaka ya kuwawajibisha wanapochukua hatua dhidi ya wabunge wao.
 
Wakudadavuwa

JF-Expert Member
Feb 17, 2016
16,388
2,000
Mkuu unanikumbusha Hayati Alhaji Aboud Jumbe Mwinyi, ccm walimfanyia kitu mbaya enzi za uhai wake!!!! Naamini nawe unakumbuka. Sijui walitofautiana nini!!!! lakini Udicteta ccm waliomfanyia Jumbe hata shetani anaendelea kulaani.
Ha ha ha Maalim Seif ndiye muusika mkuu kuanguka kwa Jumbe,kumbukumbu zinaonyesha!
 
Wakudadavuwa

JF-Expert Member
Feb 17, 2016
16,388
2,000
rekebisha heading yako. Spika "hakuwaonya" vyama vya upinzani bali ametoa ushauri wake. hawezi "kuwaonya" maana hana mamlaka ya kuwawajibisha wanapochukua hatua dhidi ya wabunge wao.
Kawaonya ila ni jukumu lao kufuata maonyo hayo....ni ole wao kwani kufanya hivyo kutawaadhoofisha wenyewe.
 
johnthebaptist

JF-Expert Member
May 27, 2014
41,747
2,000
Hii taarifa ni kwa mujibu wa gazeti la Nipashe,mwenye taarifa zaidii atujuze.Nimeipata kupitia yasemavyo magazeti Wapo Radio
 
Wakudadavuwa

JF-Expert Member
Feb 17, 2016
16,388
2,000
Walimsifi kuwa Ndugai ndiye suluhisho la wanaukuta kurudi bungeni,jana kawakosoa masultani wa vyama hivyo kuacha kufukuza fukuza wabunge...wameanza kushupaza shingo.Sasa hivi utawasikia ''Bora ya Dr.Tulia''
 
MAGALEMWA

JF-Expert Member
Jul 8, 2015
6,268
2,000
Walimsifi kuwa Ndugai ndiye suluhisho la wanaukuta kurudi bungeni,jana kawakosoa masultani wa vyama hivyo kuacha kufukuza fukuza wabunge...wameanza kushupaza shingo.Sasa hivi utawasikia ''Bora ya Dr.Tulia''
CCM hawaachi uCCM hata akiwa Supika
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom