Spika Ndugai athibitisha kupokea barua ya kujiuzulu kwa Mbunge Mwita Waitara na kusema Jimbo la Ukonga lipo wazi

neema shamuhenya

JF-Expert Member
May 24, 2018
312
216
Spika wa Bunge, Job Ndugai amesema amepokea barua kutoka kwa aliyekuwa mbunge wa Ukonga, Mwita Waitara ya kujivua uanachama wa CHADEMA na kujiuzulu wadhifa huo.

Ndugai amesema hayo leo Jumatatu, Julai 30 akiwa Ikulu jijini wakati wa hafla ya Rais John Magufuli kutoa hati za viwanja vilivyopo Dodoma kwa mabalozi 62 wa nchi mbalimbali na mashirika matano ya kimataifa kwa ajili ya kujenga ofisi na makazi.

“Kwa kuwa nimeambiwa ninaonekana nchi nzima, napenda nitangaze kuwa leo asubuhi nimepokea barua kutoka kwa mbunge wa Ukonga, Mwita Waitara kuwa amejivua uanachama wa chama chake na kujiuzulu ubunge’ amesema Ndugai ambaye alikaribishwa kutoa salamu kutoka Dodoma.

Ameongeza ataiandikia barua Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) ili taratibu zifuate. “Kilichobakia ni kuiandikia Tume ya Taifa ya Uchaguzi kuwa rasmi jimbo la Ukonga liko wazi’ ameseam Ndugai. Waitara alitangaza kujivua uanachama wa Chadema na kujiunga na CCM Jumamosi iliyopita.
 
Very fast. Ila kma Angekuwa anatoka CCM to chadema lazma kungekuwa na ka mgogoro na kigugumiz
 

Kwahiyo hapo tena tunakwenda kutupa kodi za wavuja jasho kumtafuta mrithi wa Mwita,pengine akagombea yeye tena.

Halafu tutajiuliza ni nani ametuloga?
 
Kama ndivyo, nashauri tz wabunge wote wateuliwe na mh sana. Hatutapinga maana hata sasa wanakula na kipofu huku wamemshika mikono
 
Hii sheria za kurudia uchaguzi mbunge akiachia jimbo ndo inawashaua. Katiba mpya tungependekeza mbunge aliyeshika nafasi ya pili ndo achukue jimbo kuliko kurudia uchaguzi tunapoteza pesa nyingi sana
 
Hii sheria za kurudia uchaguzi mbunge akiachia jimbo ndo inawashaua. Katiba mpya tungependekeza mbunge aliyeshika nafasi ya pili ndo achukue jimbo kuliko kurudia uchaguzi tunapoteza pesa nyingi sana
kwa sababu wanahamia CCM lakini wangekuwa wanahamia CHADEMA mambo yangekuwa vzr kabisa mathalani NYARANDU alivyohamia CHADEMA hatukusia mawazo kama hayo??//
 
Back
Top Bottom