Spika Ndugai amtaka Prof. Assad(CAG) kufika mbele ya kamati ya maadili vinginevyo atapelekwa kwa pingu

The Assassin

JF-Expert Member
Oct 30, 2018
4,355
17,321
Spika wa Bunge Mhe. Job Ndugai (Mb), leo tarehe 7 Jan, 2019 saa 7.00 mchana ataongea na Waandishi wa Habari Jijini Dodoma kuhusu kauli za kudhalilishaji Bunge zilizotolewa na Prof.Mussa Assad, Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali na Mhe. Halima Mdee, Mbunge wa Kawe.

Updates.
Spika Ndugai amtaka Mussa Assad, CAG afike mwenyewe kwa hiyari yake mbele ya kamati ya maadili ya Bunge tarehe 21. 01.2019 vingenevyo atapelekwa kwa pingu.

Aidha, Spika wa Bunge Job Ndugai amemtaka Mbunge wa Kawe Halima Mdee kufika mbele ya kamati ya maadili ya Bunge Januari 22, 2019
====

Hivi karibuni Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG) alisema bunge la Tanzania ni dhaifu, linashindwa kushughulikia ufisadi

Profesa Mussa Assad alisema wao(Ofisi ya CAG) wanatoa ripoti ambazo huonesha kuna ubadhirifu halafu hatua hazichukuliwi; huo ni udhaifu wa Bunge

Bunge linashindwa kufanya kazi yake inavyotakiwa

Bunge linatakiwa lisimamie na kuhakikisha kwenye matatizo hatua zinachukuliwa

Bunge likifanya kazi yake vizuri hata udhaifu unaoonekana utakwisha kabisa

Habari zaidi....

Spika wa Bunge, Job Ndugai amemtaka Mkaguzi na Mdhibiti Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG), Profesa Mussa Assad, kufika mbele ya Kamati ya Bunge, Haki, Maadili na Madaraka ya Bunge, Januari 21 mwaka huu, kujibu tuhuma alizozitoa dhidi ya muhimili huo kuwa dhaifu.

Pia wito huo umemkumba Mbunge wa Kawe (Chadema) Halima Mdee, ambaye naye ametakiwa kuripoti mbele ya kamati hiyo, Januari 22 mwaka huu, kuthibitisha madai yake aliyoyatoa kupitia mitandao ya kijamiii kuwa Bunge ni dhaifu.

Hayo ameyasema leo jijini Dodoma Spika Ndugai alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari ameeleza kuwa kama CAG anasema Bunge ni dhaifu basi atakuwa mpotoshaji mkubwa.

“Bunge tumepokea kwa masikitiko kuhusu kauli ya CAG, aliyoitoa Marekani. Kauli hiyo imelenga kutoa picha kwamba ripoti zake hazifanyiwi kazi au akishazifikisha Bungeni kazi inakuwa imekwisha, jambo ambalo si kweli.

Aidha Spika Ndugai aliongeza kuwa CAG na maofisa wake wanaingia kwenye Kamati ya Kudumu ya Hesabu za Serikali za Mitaa (LAAC) pamoja na Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Mashirika ya Umma (PAC).

Spika alifafanua kuwa ripoti hizo zikifika kwenye kamati hizo ambazo zinaongozwa na upinzani, muda wote maofisa wa CAG wanakuwepo kueleza mapungufu waliyoyabaini na hatua zinazopaswa kuchukuliwa.

Ndugai amesisitiza kuwa tangu serikali ya Awamu ya Tano ilipoingia madarakani, imekuwa ikipambana dhidi ya matumizi mbaya ya fedha za umma na hatua zimekuwa zikichukuliwa.

Kadhalika alibainisha namna ambavyo Bunge limefanya kazi kubwa katika kipindi cha miaka mitatu tangu serikali ya Rais Dk. John Magufuli, ilipoingia madarakani.

Spika ambaye pia ni Mbunge wa Kongwa (CCM), amesema kuwa mabadiliko makubwa kwenye usimamizi wa fedha za umma yamefanyika kwa ushauri wa Bunge na CAG, hivyo alishangazwa na hatua zipi ambazo CAG alitaka zichukuliwe.

“Alitaka hatua gani zichukuliwe?. Napeleka tahadhari kwa maofisa wa serikali na wananchi kutojaribu kulidhalilisha Bunge. Si kama Bunge halitaki kukosolewa lakini si kwa kulikosoa kwa matamshi ya dharau ambayo ameyatoa wakati akiwa nje ya nchi.

Ndugai alieleza: “Ni ustaarabu kutoisema nchi yako vibaya ukiwa nje ya nchi. Wapo watakaosema CAG ana uhuru kikatiba, lakini kwenye katiba hakuna aliyehuru bila kuwa na uwajibikaji.

Hata hivyo amesema kuwa ni vigumu kufanyakazi na mtu anayeliona Bunge dhaifu ambapo alimshauri CAG ajitathimini, kwani muhimuli huo hautokubali kudhalilishwa.

Pia soma > CAG Assad: Bunge letu ni dhaifu, limeshindwa kuiwajibisha Serikali kwa ufisadi
 
He he he
Sasa kuna kipi hapo cha kuzungumza.

Mbona hili jambo liko wazi kabisa, hata haihitaji shahada ya UDOM kulifahamu.
Mwenzetu humu Pasco alishalizungumzia hili mkamweka kitimoto na kamati zenu za Bunge japo yalimalizwa kimya kimya bila mrejesho baada ya kuwashinda kwa hoja.

Ndugai angekaa kimya tu aendelee kuunga mkono juhudi za mtukufu Jiwe.
Au kama vipi aandae tu maandamano ya ofisi ya bunge kuunga mkono kikokotoo.
Amuache CAG afanye kazi yake.
 
Prof Mussa Assad kuna sehemu kakosea kwenye ile kauli, Prof anajua utaratibu wa bunge kuwa baada ripoti yake kuwasilishwa bungeni ilibidi ijadiliwe mwisho wa siku kamati husika ndipo alipoitwa Katibu mkuu wa hazina kipindi miezi 2 iliyopita hapa baadae kamati ikimaliza kazi yake itapeleka ripoti kwa CAG tena then CAG ataangalia then ataipa Bunge ripoti juu ya kile kilichowasilishwa na kamati husika katika sakata hilo.
 
Leo saa 7.00 mchana Spika Job Ndugai ataongea na watanzania kupitia press kutolea ufafanuzi kauli za kuudhi na kudhalilisha bunge zilizotolewa na CAG Prof Assad na Mbunge wa Kawe (CHADEMA), Halima Mdee kwa nyakati tofauti.

Source: Clouds 360!
 
Prof Mussa Assad kuna sehemu kakosea kwenye ile kauli, Prof anajua utaratibu wa bunge kuwa baada ripoti yake kuwasilishwa bungeni ilibidi ijadiliwe mwisho wa siku kamati husika ndipo alipoitwa Katibu mkuu wa hazina kipindi miezi 2 iliyopita hapa baadae kamati ikimaliza kazi yake itapeleka ripoti kwa CAG tena then CAG ataangalia then ataipa Bunge ripoti juu ya kile kilichowasilishwa na kamati husika katika sakata hilo.
Hujui kitu kaa kimya
 
Anajitia aibu.sisi tunamacho tuna masikio.tunaona tunasikia yanayotendeka bungeni.bunge limekosa hadhi kabisa.limekuwa km kikao cha chama tna mda mwngne hata chama afadhali bali imekua km kikao cha kanisa.kwa mara ya kwanza nchi imepita ktk wakati mgumu bila kuwa na bunge.tuna mfano wa bunge
 
Back
Top Bottom